Kampuni ya Ndege ya Tanzania inatarajiwa kupokea ndege mpya aina ya Boeing B787-8 Dreamliner, yenye uwezo wa kubeba abiria 262.
Tukio la mapokezi ya ndege hiyo mpya linatarajiwa kufanyika leo Agosti 19, katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Zanzibar.
Your browser is not able to display this video.
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Makame Mbarawa amesema kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi atashiriki kuipokea ndege hiyo.
Kama mnakumbuka May 2024 ATCL ilitoa taarifa ikikanusha ndege hiyo kupelekwa Malaysia kwaajili ya matengenezo makubwa yaani Check-C sababu wataalamu wa kufanya matengenezo hayo wapo nchini, na kwamba ilikuwa imepelekwa huko kutokana na matatizo ya engine, na ilikuwa imekwama muda mrefu sababu ya ugumu wa upatikanaji wa spea ambazo zina uhitaji mkubwa.
Ikumbukwe pia ndege hizi za Boeing (aina ya Max) licha ya kuwa ni za kisasa zimepigwa marufuku katika nchi nyingi kutokana na kuwa na hitilafu katika mifumo yake ya utengenezaji.
Kampuni ya Boeing inaonekana kuwa na makandokando mengi, upande mmoja ndege zinapigwa marufuku kutokana na kuwa na hitilafu, upande mwingine kwenye aina nyingine spea zake ni mtiti kupata kiasi kwamba inachukua zaidi ya mwaka kufanya matengenezo, kwanini bado tunazikimbilia? Ni njia nyingine ya kufanya upigaji kwa kisingizo cha matengenezo?
Pesa za maokoto zipo haina shida, hizo mbovu ndizo sisi tunazitaka ili tuwathibitishie watesi wetu kuwa pesa za matengenezo tunazo na zikishindikana tutanunua nyingine.
Nimerekebisha Mkuu, bado ndege za boeing zina shida huku zinapigwa marufuku, huku ndege inapakiwa kwa mwaka mzima ili kupata spea, kumbuka kuna gharama za kupaki hapo kwa muda huo wote kabla ya kutoa gharama za matengenezo
Nimerekebisha Mkuu, bado ndege za boeing zina shida huku zinapigwa marufuku, huku ndege inapakiwa kwa mwaka mzima ili kupata spea, kumbuka kuna gharama za kupaki hapo kwa muda huo wote kabla ya kutoa gharama za matengenezo
Kabla hujafanya investment huwa ni lazima kufanya detail study and analysis kujua kuhusu Kila kitu ikiwemo spare parts Kwa biashara ya usafiri wa anga.
Kama hili halikufanyika, basi kulikuwa na shida hapo ATCL
Lakini mtoa mada mbona hizo Ndege za Boeing ukienda pale ATCL zipo na zinatumika Kwa zile route za nje ya Nchi.
Na hata route za ndani zenye abiria wengi zinatumika.
Mfano kwenye route ya Mbeya-dsm kwenye peak day huwa zinatumika, na hata DSM - Mwanza zinatumika.
Nadhani ni suala la Management kuwa na utaratibu mzuri wa vipuri pamoja na kuzingatia service
Tangu jana kuna mashindano ya kutangaza ujio na mapokezi ya ndege ya Air Tanzania, Boeing 787-8 ambayo hadi leo haijakabidhiwa kwa mnunuzi. Hizi haraka haraka za waziri kutangaza wakati Boeing hawajatangaza ukamilifu wake wala kuikabidhi kwa Air Tanzania zinatoka wapi?
Wacha zinunuliwe zinasaidia hata kuitangaza nchi yetu huko ughaibuni,ila management ya hili shirika inatakiwa itizamwe kwa jicho la umakini sana,maana itakuwa haina maana kumiliki madege yote hayo halafu kila mwaka tunahesabu hasara...