Tanzania kushiriki Jukwaa la Uongezaji thamani madini Uingereza

Wizara ya Madini

Govt Institution
Joined
Apr 12, 2025
Posts
50
Reaction score
20
Leo tarehe 19 Mei, 2025 Ujumbe wa Tanzania kutoka Wizara ya Madini, ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, umewasili jijini London nchini Uingereza kwa ajili ya kushiriki Jukwaa la Uwekezaji kwa Sekta ya Madini lililobeba agenda ya Uongezaji Thamani Madini (Minerals Beneficiation And Value Addition).

Jukwaa hilo ni fursa kubwa ya kuvutia wawekezaji wa kujenga viwanda nchini Tanzania na kuondokana na utegemezi wa kusafirisha madini ghafi jambo ambalo litasisimua ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa Watanzania.

Ujumbe huo umepokelewa vizuri na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Mbelwa Kairuki, ambapo mazungumzo mafupi kuhusiana na vikao vinavyotarajia kuanza tarehe 20.05.2025 hadi 22.05.2025 yamefanyika.
 
Muwe mnatushirikisha na sisi wachimbaji wa aina zote tujionee,sio nyie mtuwakilishe peke yenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…