Tanzania kushirikiana kijeshi na Iran

Inasemekena Tz kuna Uranium na Iran anahitaji sana hiyo resource

Inaoenkana kila anayetaka kuwa Rais Tz ni muhimu kuwa karibu na Iran

......of all the countries!!!.....Iran!!.......give me a break!!......damn

Naamini Tanzania ni nchi isiyofungamana na nchi yoyote na tuna uhuru wa kuangalia lenye faida nasi, kama hiyo uranium mnunuzi atakuwa Iran basi tutamuuzia kwani ipo tofauti gani kati ya Iran na Marekani haizidi Marekani ameshauwa sana kuliko hao Wairani.
 
Ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni...kwa mtazamo wangu hili suala la kuanza uhusiano wa kijeshi na Iran ni lakuangalia kwa makini. Tusijiingize kwenye games ambazo hatutakuja kuziweza mana hawa jamaa wa Iran policy zao haziko compatible na siasa yetu ya kutofungamana na upande wowote.
 
YNIM,

..USA na Iran ni maadui wakubwa na kuna vita baridi inaendelea kati yao.

..sasa kabla hawa wakubwa[usa & iran] hawajapatana, au kumaliza tofauti zao, kama mwandishi anavyoshauri, ni bora wa-Tanzania tukaepukana nao.

..ni hatari kwa Tanzania kujitia kimbelembele cha kumkumbatia mmoja kati ya wababe hawa waziwazi.

..hawa wababe hawa common border kwa hiyo vita watakayopigana ni proxy war.

..tuwe makini na tuinusuru nchi yetu isije kuwa Angola, Zaire, Vietnam, au Afghanistan, ambazo zilikuwa uwanja wa mapambano kati ya USA and former Soviet Union.

NB:

..tena kama tunaambiwa kuna Uranium ndiyo inabidi tuwe makini zaidi na mashirikiano yetu kama Iran.

..Congo/Zaire walikuwa na wakati mgumu sana wakati wa cold war kutokana na uwepo wa uranium ktk ardhi yao.
 
dogo weekend hii...badala ya kuwa sehemu sehemu unakula maisha wewe unashinda JF.....ngoja mwenzio niingizane Luckie Lounge....
 

Ahh. .. Ustadha Tausi..i mean Baunsa..

Nilikuwa sijapitia huku..kumbe hata huku unaendeleza pumba zako ..LOL..Unasema unabanana..unabanana na nani? Mimi sina kawaida ya kubanana na watu wenye mtindio. Hiyo ndo filosofia yangu. Nakupa ukweli wako halafu nakuacha..

Hivi, unadhani kuna mtu ana ufagio na pumba zako zaidi ya hao mapakacha wenzako wenye akili butu..? Nilikuacha kule kwenye ile thread utukane matusi yooote uliyofundwa na wazazi wako na ufungiwe peke yako lakini mamods( haswa huyu kimbelembele Silencer) wakakuogopa na kunifungia na mimi ili kukufurahisha ..

Haya sasa, nakupa bonus ofa, kamwambie baba yako Silencer na kingereza chake cha dictionary anifungie tena ili ufurahi na kukenua..

Bua ha ha ha..
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni chizi, tena alokuroga kesha kufa....lol! Kama ni karata basi wewe galasa...

Naona hili la mafungamano na Wairani lisikupe tatizo moyoni kwani mara nyingi hii mikataba inayofanywa na wakubwa wetu haitufungi na wala hatuna bidii ya kuifatilia. Naona mtaumiza vichwa kwa kukosa usingizi wakati hii si mikataba bali ni mbinu za kupata kufutiwa madeni na mwahala mwa pesa ya haraka kwani hao mabwana wetu tunaowaona wao ndio awliostaarabika na wasafi misaada yao na pesa zao zina njia ndefu kuzipata.

Cha kushangaza ni kuwa Wabongo ubongo wetu umelemazwa na uzungu na kutiwa chuki na uarabu lakini hao wazungu pesa wanayotambia inatoka huko kwa Waarabu na viongozi wetu wanalijuwa hilo na ndio maana wanajisogeza nao kwa Waarabu. MSIPOTEZE USINGIZI hakuna Muirani atakaekuja hapa bali ni SIASAtu.
 

YNIM,

..uhusiano na urafiki tunaozungumzia hapa ni ktk masuala ya KIJESHI.

..kama Iran wanataka kutusaidia kulima mbirimbi,mboga-mboga etc i am cool with that. kuna mradi wa kilimo maeneo ya Rufiji uko funded na wa-Iran.

..Marekani nao kama wanataka kutusaidia kupambana na malaria i am also cool with that.

..mahusiano ninayoyapinga mimi ni mahusiano ya KIJESHI na mataifa hayo mawili.

..hakuna suala la udini hapa. Tanzania ina mahusiano ya kijeshi na Egypt na Algeria, nchi za Kiislamu, na sina matatizo nayo. mwenendo wa serikali za mataifa hayo ni tofauti na ule wa Iran.

..mwisho, article uliyoileta kuhusu Iran inatisha, lakini ndiyo ukweli wenyewe kuhusu Iran. hakuna haja ya kunisakama kwamba natisha wana-JF, wakati wewe mwenyewe umeshindwa kuleta taarifa zinazowa-humanize wa-Iran.
 
Inasemekena Tz kuna Uranium na Iran anahitaji sana hiyo resource

Inaoenkana kila anayetaka kuwa Rais Tz ni muhimu kuwa karibu na Iran

......of all the countries!!!.....Iran!!.......give me a break!!......damn


Labda upo sahihi!!

Iran needs Uranium

'Iran running short of uranium supply'

Link:
'Iran running short of uranium supply' | Iran news | Jerusalem Post


Iran in scramble for fresh uranium supplies
Link:
Iran in scramble for fresh uranium supplies - Times Online


Report: Iran's uranium supply could run out within months
Link:
Report: Iran's uranium supply could run out within months - Haaretz - Israel News

Does Tanzania have it?

Tanzania Prepares Policies For Uranium Mining
Link:
Tanzania Prepares Policies For Uranium Mining

UK firm buys Tanzania uranium licences
Link:
UK firm buys Tanzania uranium licences
 

Msaada wa kilimo jeshini. Msaada wa kilimo jeshini. Okay! Msaada wa kilimo jeshini.

Wanaweza kutuonyesha hiyo Memorandum of Understanding iliyoripotiwa kusainiwa?

Hakuna kitu nakisubiri kwa hamu kama muswada wa Freedom of Information Act unao languish wizara ya Mkuchika toka 2007. Lakini unaweza kupitishwa na waandishi wakashindwa kuutumia. Press ya vilaza.

Hawasemi ilikuwaje mpaka akatoa ufafanuzi leo kwa habari ya wiki mbili zilizopita, alibanwa na mwandishi au alikuwa na routine press conference, alikuwa kwenye kilabu cha pombe akaulizwa na some curious friend, what was the occasion? Masharti ya huu mkataba ni nini? Hizo reports alizokuwa ana clarify ni zipi hizo? So far nimeona ni magazeti ya Iran na ya Uchina yamenukuliwa na Mwanakijiji yakisema uhusiano ni wa kijeshi. Sasa Waziri sijui anasema Wairani waongo? Hakuna wakutuhabarisha hivi vitu.

Yani kuna mtandao wa Wachina ndio umeripoti lile dili siku liliposainiwa, na some Iranian outlet. Sisi aaaah, hatuna presha na maisha. Tumenukuu Wachina na Wairani wanaandika kuhusu dili letu la kijeshi. Sijui kilimo, sijui kijeshi. Sijui JKT. Who knows. Na JKT hivi ni nini hasa, zamani nikikuwa nafikiri ilifutwa pamoja na utaratibu wa JKT ya lazima wa wanafunzi. Sasa hii JKT hii, nani anaenda JKT siku hizi, kazi yake nini hasa, kutulisha? Kwa mujibu wa sheria gani?
 
Kati ya Waziri wa Tanzania au wa Iran mmoja wao amelidanganya taifa lake:

Hivi ndivyo imeripotiwa:


Lakini vyombo vya Iran na vingine vya kimataifa viliripoti hivi:


more News:

So:

Yawezekana:

a. Waziri wa Iran alikuwa anadanganya
b. Waziri wa Tanzania alikuwa anadanganya
c. Hawa wote hawajui walichokubaliana
d. Hawa hawakukutana kabisa na hawaakuzungumza lolote!

Vyovyote vile ilivyo; Kama Mwinyi kadanganya basi na yeye ajiandae kuomba msamaha tumsamehe.
 
Issue ya Iran ina angle mingi sana.....kitu ambacho bongo inafanya na Iran so far ni pouwa tu, ila unataka kubebea bango kwa sababu zako binausi! carry on and yes you can... goodluck.

Kuwa na uhusiano sio tatizo, ila hao tunaoweka nao uhusiano wanataka nini au wana nia gani na huo uhusiano?
 
Mwanakijiji,'
Let me be biased. Nadhani aliyedanganya ni waziri wa Tanzania. Tuna utamaduni huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…