Mkuu Joka,
Mbona unapindisha mchana kweupeee ninachosema mimi ni kuwa, tunaweza kuwa marafiki wa Iran kama ambavyo tulivyo marafiki wa USA bila kuegemea upande wowote ktk bifu lao....so far ndipo tulipo sasa hivi Tzania kama nchi!!
Hizi story za kusema tusiwe rafiki wa yeyote mpaka wa sort out tofauti zao umezitoa wapi? Hivi Bush alikuwa anafanya nini bongo mwaka jana!? Unachosema wewe kimsingi ni kuwa, tuwe rafiki wa USA na sio Iran (kitu ambacho nadhani si sahihi), na huko ndiko kuchukua sides kwenye/kujiingiza ktk bifu lao.
Hizo habari za proxy war kupigwana Tzania umeziokota wapi mkuu!? Vita ya Iran na US inapiganwa huko huko middle east hasa Palestine, Lebanon na sasa Iraq...hizo scare tactics zako zitafanya kazi hapa hapa JF kwa watu dizaini ya Ubungoubungo, lakini wajanja tunaelewa kuwa hizo ni story tu!. Moja wapo ya hizo proxy war za Iran na USA ni hiyo onslaught ya Gaza iloisha juzi, ambayo "kimsing" ni another loss kwa Israel.
NB: Bongo inaweza kuwa rafiki wa Iran bila kutengeneza uadui na USA, vile vile inaweza (kama ambavyo ilivyo sasa) kuwa rafiki wa USA bila kutegeneza uadui na Iran......longolongo zaidi ya hapo ni majungu, udini, fitina, uzushi na uzandiki uso kipimo!
Wkend Njema!