Tanzania kushirikiana na Uganda kuimarisha ulinzi na usalama

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission - JPC), kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda uliofanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, wajumbe wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo mashirikiano ya Kidiplomasia na Kisiasa, masuala ya ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji.

Kadhalika, Viongozi hao wamejadili maendeleo ya miundombinu ikiwemo sekta za ujenzi, usafirishaji na nishati ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi na kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Uganda.

Vilevile, wamejadiliana namna vitambulisho vya Uraia vya Tanzania na Uganda vinaweza kutumika kama nyaraka rasmi vya utambulisho wakati wa kusafiri kati ya nchi hizo mbili, lengo la hatua hii ni kuhakikisha kwamba vitambulisho vya taifa vinavyotolewa na pande zote mbili vinatambulika pamoja na kuwarahisishia wananchi wa nchi hizo mbili kusafiri kwa urahisi.

Kikao hicho ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uganda, pamoja na kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kidiplomasia kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Soma pia Tanzania na Uganda zasaini makubaliano kuimarisha ushirikiano wa kimkakati reli ya SGR

1773480714520.png
Chanzo: ITV
 
Uganda Hawa waliowaleta wanajeshi wao kuja kuua ndugu zetu hapo October 29
Nilimsikia raisi wao yule babu akiongea kwenye kile kikao Cha chai Cha wauwaji kule Arusha .ndiyo maraisi wa afrika mashariki wote ni wauaji tu.
Museven alikuwa anapngea kuhusu GZ Hadi nikaona aibu
Nikasema Hawa wote akili zao zinafanana
 
Back
Top Bottom