Tanzania kutoa misaada kwa nchi jirani ni kusimamia sera yake ya mambo ya nje

Tanzania kutoa misaada kwa nchi jirani ni kusimamia sera yake ya mambo ya nje

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Katika siku za karibuni tumeshuhudia Tanzania ikikabidhi "misaada" ya kibinadamu kwa nchi zilikumbwa na majanga ambazo ni Malawi ambayo ilikumbwa na kimbunga Freddy pamoja na Uturuki ambayo ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililopelekea uharibifu mkubwa wa mali na mazingira.

Nchini Malawi misaada ambayo ilikabidhiwa na Waziri wa mambo ya Nje Dkt Sttergomena Tax kwa niaba ya rais Dkt Samia Suluhu na kupokelewa na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera ni fedha taslim na vifaa mbalimbali wenye ya thamani ya Dola za Marekani Milioni Moja.

Msaada huo pia unajumuisha chakula, vifaa vya kuokolea, vifaa vya kujihifadhi, Helikopta 2 za kijeshi zitakazotumika kupeleka misaada katika uokoaji pamoja na wanajeshi 100 watakaoshiriki kusambaza msaada huo; Mahema 50; Blanketi 6,000; Tani 1,000 za unga wa mahindi na fedha taslim kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

Nchini Uturuki, Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa Dola za Kimarekani milioni moja (1,000,000) kama msaada kwa Nchi hiyo, msaada ambao ulikabiliwa na Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki Luteni Jenerali Yacoub Mohammed.

Msemaji wa Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga ameeleza kuwa sera ya mambo ya Nje ya Tanzania imejikita katika misingi ya kuimarisha mahusiano na mataifa jirani pamoja na jumuiya ya Kimatifa kwa ujumla hivyo misaada iliyotolewa kwa nchi za Malawi na Uturuki zimebebwa na misingi hiyo ambapo pale rafiki anapokumbwa na matatizo ni vyema kumsaidia.

Pia soma:
 
Back
Top Bottom