Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema Tanzania imejipanga kutumia balozi zake zote zilizopo katika mataifa mbalimbali duniani, ili kuzifikia fursa za Kimataifa zilizopo katika mchezo wa Ngumi na kuwezesha mchezo huo kukua Kimataifa.
Mhe. Balozi Kombo ameyasema hayo wakati akizundua Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa ya Mchezo wa Mgumi, yaliyofanyika katika Klabu ya Mambo Beach, jijini Dar es Salaam, wakati wa mkesha wa kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025.
Mashindano hayo yaliyokuwa na kaulimbiu isemayo “Mfalme Amerudi”, yaliandaliwa na Kampuni ya King Class Sports, ambapo jumla ya mapambano 12 yaliweza kufanyika, mawili kati ya hayo yakiwa ni mapambano ya Kimataifa.
Mhe. Balozi Kombo amesema mkakati wa kushirikisha Balozi za Tanzania duniani kutangaza mchezo wa ngumi na michezo mingineyo, utawawezesha wanamichezo wa Tanzania kufikia fursa zilizopo zikiwemo mafunzo, ufadhili na ushiriki katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa ya michezo.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mfano wa kuigwa nchini kwani ni mhamasishaji mkuu katika kutetea maslahi na maendeleo ya wanamichezo wa Tanzania, hatua iliyowezesha kukuza vipaji na taaluma ya michezo kuanzia ngazi ya jamii hadi ya Kitaifa na Kimataifa.
Ameipongeza kampuni ya King Class Sports kwa jitihada zake za kuendeleza mchezo wa ngumi na amewataka wadau wengine katika jamii kujitokeza kuendeleza michezo ili kukuza uwezo wa Kimataifa wa Tanzania katika michezo, huku wakiunga mkono juhudi za Rais Samia za kuendeleza michezo kwa manufaa ya Watanzania.
Tanzania iliibuka mshindi katika mapambano yote mawili ya Kimataifa ambapo ilipambana na Malawi na Afrika Kusini. Pambano Kuu la Kwanza la Kimataifa, lililojulikana kama "Knockout ya Mama", lilimuhusisha Ibrahim Class wa Tanzania aliyepambana vikali na Simpiwe Vetyeka wa Afrika Kusini, na kuibuka mshindi.
Aidha, pambano la pili, lilikuwa ni Pambano la usaidizi, ambapo Nassib Ramadhani wa Tanzania alikabiliana vikali na Yamikani Mtambo wa Malawi, na kuibuka mshindi.
Mapambano mengine ya ngumi yaliyofanyika wakati wa mashindano hayo, yalihusu uteteaji wa Mkanda wa Taifa la Tanzania (Tanzania Champion Belt) ambapo Mabondia walioshiriki, walipambania kulinda nafasi zao na kushindania Mkanda wa Taifa, huku wakionesha umahiri na vipaji vikubwa walivyonavyo.
King Class Sports ni kampuni binafsi inayomilikiwa na Bondia wa Kulipwa Ibrahim Class, ikilenga kukuza ngumi za kulipwa nchini na kuhamasisha wanamasumbwi kuzifikia fursa za kimataifa za mchezo wa ngumi na kunufaika nazo.

Attachments
-
IMG-20250102-WA0154(1).jpg703 KB · Views: 2 -
IMG-20250102-WA0156.jpg448.2 KB · Views: 4 -
IMG-20250102-WA0158.jpg512.8 KB · Views: 4 -
IMG-20250102-WA0152.jpg348.6 KB · Views: 4 -
IMG-20250102-WA0149.jpg465.8 KB · Views: 2 -
IMG-20250102-WA0150.jpg554.5 KB · Views: 1 -
IMG-20250102-WA0142.jpg711.9 KB · Views: 1 -
IMG-20250102-WA0144.jpg685.7 KB · Views: 2 -
IMG-20250102-WA0146.jpg654.3 KB · Views: 5