Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra) imetoa mwongozo mpya itakayoweza kubadilisha namna ambavyo Watanzania wanavyopata huduma za simu.
🗯️ Mwongozo mpya utoaji wa mawasiliano ya moja kwa moja toka kwenye simu kwenda kwenye satellite, iliyotolewa julai 2025, huruhusu simu za mkononi kuunganishwa moja kwa moja na satellite na kupunguza utegemezi wa kutumia minara ya kawaida ya simu.
🗯️ Mfumo huo umeidhinishwa na mkurugenzi wa Tcra Dk Jabir bakari, unasisitiza kuwa mamlaka imedhamiria kuwezesha upelekaji wa huduma za moja kwa moja kwenye simu ila Kuhakikisha ulinzi wa mitandao ya IMT Duniani.
🗯️ Lakini chini ya miongozo hiyo waendeshaji wa huduma za satellite hawataruhusiwa kufanya kazi pekee yao badala yake wanatakiwa washirikiane na watoa huduma wa ndani wenye leseni kama vile Vodacom, Yas au Airtel.
🗯️ Ushirikiano huo Utaweza kuanisha kwa uwazi kupitia masharti ya kiufundi na kibiashara, umiliki wa spectrum utasalia kwa Kampuni za simu huku setilaiti yoyote ya kigeni lazima ipate haki toka TCRA kabla ya kutoa huduma ndani ya nchi.
Credit: Citizen