Tetesi: Tanzania kuwa nchi ya nane kwa idadi ya watu DUNIANI

Tetesi: Tanzania kuwa nchi ya nane kwa idadi ya watu DUNIANI

Habar

Population au idadi ya watu ni suala pevu na lenye mashiko

View attachment 1696468

Linaipa nchi

-bargaining power kwenye soko la dunia
-fulsa ya biashara
-nguvu ya jeshi kwakua na millitary man power
-kupata talent mbalimbali
-n.k

Ifikapo mwaka 2074 tanzania tutakua nchi ya 10 kwa idadi ya watu syo AFRICA bali duniani

View attachment 1696461



Nigeria itakua nchi ya ni ya tatu ikiizidi USA just behind india and China
Wakati DRC ikiwa ya saba na ethiopia ya 8
Actually mwishoni mwa karne ya 21 nchi 20 zenye population kubwa zitatokea Africa

View attachment 1696467



Wakati hapo ifikapo 20100
Tanzania itakua nchi ya 8 kwa idadi ya watu!!...
Hope tutakua tishio duniani kiuchumi,kijeshi na kiushawishi

We unaonajeView attachment 1696469
View attachment 1696470
Israel ikowapi?, Italy ikowapi?, Britain (wingereza) ikowapi? Japan ikowapi? ina maana dunia nzima kuna nchi 20 pekee, Ukiacha hivo, Africa yenyewe inazaidi ya nchi 50.
Au unataka kumaanisha kwamba nchi zote hizo ulizoacha kwamba wao ndo hawajui, hawapendi au ndo hawana mpango wa kuzaliana?
na je wametumia/umetumia kigezo gani kuainisha nchi hizo tajwa hapo juu kwamba kufkia miaka tajwa ndo nchi zitakazokuwa na idadi kubwa ya watu kuliko zingine?
China haikua nchi yenye idadi kubwa ya watu kama ilivyo sasa, enzi za mao ze dong miaka ya 1939-1949 alihamasisha wachina kuzaliana kwa wingi na ulikuwa ni mpango mahususi wa china, ili kuongeza nguvu kazi ya kustawisha taifa.
Hivi sasa Japan nao wameshaanzisha mfumo wa namna ya kuongeza idadi ya watu nchini mwao na ni mpango mahususi wa Japan, nao yawezekana baada ya miaka 10 ijayo ikawa ni nchi yenye watu wengi zaidi duniani kama china au kuliko china.
kuna nchi nyingi mno hujaziainisha hapo, tena zenye mipango na mikakati kama japan, kiasi kwamba zingeorozeshwa hapo, tz ingefyata mkia kwa idadi ya watu kwa miaka tajwa ijayo.
Hivyo basi, niseme tu umetuletea takwim za kupikwa, hizo ni tetesi za uongo hazina mashiko.
 
kupanda kwa population ni Jambo zuri,ikiwa tuta balance mambo.hasa haya mawili economy & technology,kinyume Cha hapo tutakuta.
 
Kwa huu umasikini ulizopo na hao watu wakiwa wengi hapa itakuwa hapo itakuwa chaos watu wazae kwa mpango.

Hapo ni sawasawa na familia masikini yenye watoto 12 lakini haiwezi kuwahudumia au kuwapa mahitaji muhimu hivyo umasikini wao kuongezeka kila siku.

Ila kama tukiweza kuwatumia hao watu wengi kuzalisha na kuvuna rasimali zetu wenyewe i think tutakuwa kama USA.
Vinginevyo itakuwa ni balaa.
 
Hapana mkuu ishu siyo sifa ishu n kua in headlines duniani
Nani asiyejua china leo??? Au india??
But tanzania nchi nyingine watu hawaijui

With headlines nchi inajitangaza ,kupata wataliii na kuwa target ya uwekezaji
Umenisikitisha sana ndugu mtanzania!.

Sasa tukianza mjadala hapa hatutaumaliza but hivi unaweza kulinganisha China na Tanzania kweli?

Although hata tukiwa 9bil people na hatutakuwa na impact yoyote, sababu afrika hatujawa na uwezo wa uzalishaji wa bidhaa au kilimo kinachoweza kutupa nguvu.

China yenyewe kwa wingi wao inaweza kujitengenezea self income kutokana na country productivity, pia
India kwa sasa inakimbiza katika industry ya IT na mpaka sasa baadhi ya App tunazotumia tunanunua kwao wao pia wanauwezo kujitengenezea self income kama china.
 
Tanzania tuko vzuri kwenye Sector ya kufyatuana, pia na nchi yetu asilimia 90 ni mapori hayana watu
Hakuna mahali penye Pori sasa hivi, labda hifadhi za serikali . Nenda kaguse kila mahali pana wenyewe
 
Mimi sidhani kama itakuwa sifa au hizo unazosema 'powers' bali ni majanga zaidi.
Jarida la "The Economist" la wiki hii, katika makala ya "Africa's recovery from Covid-19 will be slow", linaandika;

"Africa has a young and fast growing population. The median age is 19.5; by 2035 it will be adding more people of working age to the global population than everywhere else put together. A long, sluggish recovery would make it harder for the largest-ever generation of young Africans to find jobs, heaping pressure on ageing leaders".

Tunaongeza watu kuliko uchumi unavyokua.

Matokeo yake, faida za kukua kwa uchumi hazionekani, zinafutwa na kuwa negated na ongezeko la watu.
 
Hakuna mahali penye Pori sasa hivi, labda hifadhi za serikali . Nenda kaguse kila mahali pana wenyewe
Katika miaka 20 iliyopita, tumetoka kuwa nchi ya watu milioni takriban 30, mpaka sasa tumefikia kuwa watu takriban milioni 60.

Tukiendelea na kasi hii ceteris paribus, bar Malthusian checks, katika miaka 20 ijayo tunaweza kufikia idadi ya watu milioni 120.

Halafu watu wanashangilia ongezeko la watu?
 
Jarida la "The Economist" la wiki hii, katika makala ya "Africa's recovery from Covid-19 will be slow", linaandika;

"Africa has a young and fast growing population. The median age is 19.5; by 2035 it will be adding more people of working age to the global population than everywhere else put together. A long, sluggish recovery would make it harder for the largest-ever generation of young Africans to find jibs, heaping pressure on ageing leaders".

Tunaongeza watu kuliko uchumi unavyokua.

Matokeo yake, faida za kukua kwa uchumi hazionekani, zinafutwa na kuwa negated na ongezeko la watu.
Yes, hiyo ndiyo nilimaanisha haswa, maana afrika hatufiki kwa malengo.
 
Huwezi kuwa superpower kwa idadi kubwa ya watu tena wasio na elimu.
Bali unaweza kuwa superpower kwa idadi ndogo tu ya watu wenye elimu bora na maarifa mengi kichwani.

Hivyo basi,Tanzania inatakiwa iwe na mfumo mzuri wa elimu unaoendana na dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.
Kuwa na idadi kubwa tu ya watu hilo halisaidii.
 
Huwezi kuwa superpower kwa idadi kubwa ya watu tena wasio na elimu.
Bali unaweza kuwa superpower kwa idadi ndogo tu ya watu wenye elimu bora na maarifa mengi kichwani.

Hivyo basi,Tanzania inatakiwa iwe na mfumo mzuri wa elimu unaoendana na dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.
Kuwa na idadi kubwa tu ya watu hilo halisaidii.

Ciongelei kuwa super power nachoongelea n advantage ya population kubwa
 
Back
Top Bottom