BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali ya Tanzania imesema itawafutia hadhi ya ukimbizi wakimbizi wa Burundi wanaoishi mkoani Kigoma, iwapo wataendelea na msimamo wa kutojiandikisha na kurejea kwao kwa hiari katika kipindi chote chapili ambacho serikali ya Burundi nayo imeingilia kati kuhamaisha.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya ujumbe wa Serikali ya Burundi kutembelea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu na Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma, ambapo lengo ni kuwapa ushuhuda wa amani na usalama uliopo nchini kwao na kuwahamasisha kurudi nyumbani kwenda kuijenga nchi yao.
Akizungumza jana Novemba 30, Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wakimbizi nchini, Sudi Mwakibasi amesema hatua ya kwanza tayari imefanyika kwa wao kujiorodhesha kwa hiari ambapo wakimbizi 144,704 wamesharejea tangu kuanza kwa mpango huo 2017.
Mwakibasi amesema awamu ya pili ni ya kutoa hamasa ambapo ilianza serikali ya Tanzania kuongea na wakimbizi hao kwa zaidi ya vikao vitatu kabla ya hatua ya sasa ambapo serikali ya Burundi imefika kutoa hamasa na ufafanuzi wa vikwazo kadhaa.
Amesema baadaye jumuia za kimataifa zitaingilia kati kutoa hamasa na kuwashawishi ili waweze kurejea nchini kwao kwa hiari kabla ya hatua ya tatu na ya mwisho ya kuwafutia hadhi ya ukimbizi wakimbizi hao.
Kiongozi wa ujumbe wa Burundi Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya Jamhuri ya Burundi, Nibona Binasinze amewahakikishia Warundi wote kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia wale wenye mahitaji maalumu na changamoto kadhaa hasa mitaji, ardhi na mkazi katika hatua ya awali watakaporudi.
Naye mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani (UNHCR), Wilaya ya Kibondo, Henok Ochalla amesema kwa watakaondoka kwa hiari watapewa mabati wanayaotumia na chakula na wanaangalia uwezekano wa kuwapa stahiki zao za kifedha.
Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nduta, Samweli Kuyi amesema kambi hiyo ina wakimbizi 77,038 ambapo kiwango cha urejeaji wa wakimbizi hao kiko tofauti na matarajio yalivyokuwa.
Kuyi amesema kuanzia Junuari 2022 hadi Novemba 2022 jumla ya wakimbizi 3,984 wanaotoka kwenye kaya 1,508 wamerejea kwa hiari nchini Burundi, ambapo idadi hiyo ni sawa na wastani wa wakimbizi 90.5 kwa wiki na wakimbizi 362 kwa kila mwezi.
“Tofauti na makubaliano yaliyofanyika katika kikao cha utatu kati ya Serikali za Tanzania, Burundi na UNHCR kilichofanyika nchini Burundi mwaka 2021 na makubaliano yalikuwa kurudisha wakimbizi 1, 400 kwa wiki,” amesema Kuyi.
MWANANCHI