Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
Ikiwa GB 10 unauziwa kwa 25,000/=, na zenyewe unatumia ndani ya siku kadhaa tuu ukiwa kwenye 4G, je ukiwa kwenye 5G si ni siku moja bando linakuwa limeisha?
Mabadiliko ya teknolojia yanapaswa yaendane na mabadiliko ya sera za bei za data. Nchi nyingi zilizozindua hii teknolojia ya 5G hawatumii haya mabando ya kununua kwenye simu bali wanatumia teknolojia ya FIBER.
5G kwenye hizi bando za kupimiwa kwenye kibubu haiendani kabisa. 5G inapaswa uitumie ukiwa na zile unlimited data packages ndiyo utaenjoy. Kama ni kustream basi unastream ukiwa hauna stress kwamba bando litakata.
Wengi wetu kwa sasa tumesha-switch kutoka 4G back to 3G kwa gharama za sasa za mabando, imagine bando la wiki unatumia kwa siku 1 tena masaa kadhaa tu. Sasa mnaleta hii 5G kwa hizi bado si ndo balaa?
Sema kwa kuwa mko busy na tozo na ndiyo priority yenu basi mambo ya msingi kama haya mtaziba masikio yenu nta.