Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Huu ni uzi maalum wenye lengo la kuelezea na kubadilishana mawazo juu ya maana na umuhimu wa Tanganyika kuelekea kura ya maoni. Tutajadili mengi ikiwa ni pamoja na:

1. Asili ya Tanganyika.

2. Mchakato uliotumika kuifuta Tanganyika:
A) Sheria mbalimbali zilizopitishwa kuifuta Tanganyika.
B) Mbinu zilizotumika.
C)Malengo yaliyokusudiwa.

3. Asili ya Tanzania.

4. Faida na hasara zilizojitokeza baada kufutwa kwa Tanganyika - faida na hasara kwa Tanganyika yenyewe, zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ujumla-kisiasa, kiuchumi na kijamii.

5. Umuhimu wa kuizindua Tanganyika - Faida na hasara za kuizindua Tanganyika kwa Zanzibar, Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ujumla - kisiasa, kiuchumi na kijamii:

A) umuhimu on the macro level
B) umuhimu on the meso level
C) umuhimu on the micro level

5. Nini kitatokea mbeleni iwapo Tanganyika haitazinduliwa, hasa tukizingatia mshirika mmoja wa muungano (zanzibar) tayari ana autonomy yake (kupitia katiba ya zanzibar ya 2010),huku mshirika mwenzake akiwa hana autonomy yake ambayo ni haki ya kikatiba na kidemokrasia. Ikumbukwe kwamba tofauti na kabla ya 2010 ambapo zanzibar ilikuwa ni sehemu ya jamhuri ya muungano na Tanzania ilikuwa ni nchi moja, kufuatia mabadiliko ya katiba ya zanzibar (2010), hivi sasa Tanzania ni nchi mbili zenye serikali mbili;

6. Kwanini SERIKALI MBILI AU MOJA NDIO KUVUNJA MUUNGANO.

7.Options zilizopo mezani za kudumisha muungano uliopo na zipi ni practical, zipi sio practical na kwa sababu zipi.

Na mengine mengi.

MUHIMU:
Tutaweka itikadi zetu za vyama pembeni kwani mkataba wa muungano haukutaja TANU, ASP wala chama chochote cha siasa. Hii ilifanywa kwa makusudi ili kuupa muungano mwonekano wa kitaifa. Siasa za vyama zilijipenyeza kinyemela baadae a ndio chanzo cha mgogoro unaotusumbua leo. Tutalifafanua hili kwa undani zaidi kwa nia ya kuirudisha historia ya muungano katika muktadha unaostahili.

Tutawaletea mjadala huu muda sio mrefu. Mwelimishe mwenzako juu ya haja na umuhimu wa kauli yetu mbiu kuelekea kura ya maoni.


Kauli Mbiu Yetu Kuelekea Kura Ya Maoni Ni:

TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA.


Nape Nnauye, MwanaDiwani, Dr W. Slaa, Mwigulu Nchemba, Kitila Mkumbo, Mzee Mwanakijiji, ZeMarcopolo, Kurugenzi ya Habari, Tumaini Makene, Ben saanane, JokaKuu, Jasusi, Kobello, Mtanganyika, Ritz, zomba, Makusudically



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
UTANGULIZI: ASILI YA TANGANYIKA

Wadau na wale wote wenye kuamini katika kauli mbiu ya "TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA, mjadala wetu utakuwa na sehemu kuu zisizopunga sita, na baadae nitazianisha sehemu hizo. Katika sehemu hii ya utangulizi, kuna haja ya kuweka masuala kadhaa sawa:

1. Kufuatia kauli ya Waziri Mkuu Pinda ambae alihoji wananchi wanaitaka Tanganyika ipi, huku akisisitiza kwamba Tanganyika ya mkoloni ilikaa kwa miaka mitatu tu na baadae kugeuka kuwa Tanzania, kauli hii imeleta mchanganyiko mkubwa ndani ya jamii, huku baadhi ya wananchi wakishindwa kuelewa asili ya Tanganyika.

2. Suala la kwanza hapo juu (kufuatia kauli ya Pinda), pia limepelekea kwa tatizo lingine kujitokeza. Nalo ni baadhi ya wananchi kuanza kushawishika kwamba jina "Tanganyika" asili yake ni "mkoloni" na sio mtanganyika, tofauti na jina "Tanzania" ambalo asili yake ni sisi wenyewe. Swali linalofuatia ni je, sisi wenyewe ni kina nani kama sio watanganyika?

Nia ya sehemu hii ya utangulizi ni kurekebisha upotoshaji wa aina mbili uliojitokeza kama nilivyoainisha hapo juu. Suala la upotoshaji wa Waziri Mkuu Pinda, Mdau mwenzetu Nguruvi3 huko nyuma alilijadili vizuri sana na kuliweka sawa. Sasa kwa vile nguruvi3 alifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa, nina muomba akipata nafasi aje humu kutupa elimu ile muhimu. Kwa sasa mimi nitajikita katika hoja ya pili hapo juu - yani upotoshaji kwamba jina "Tanganyika", asili yake ilikuwa ni mkoloni, na sio wenyeji, sijui tuwaite nini zaidi ya watanganyika kama tutakavyoona sio punde, napenda kurekebisha upotoshaji huu kama ifuatavyo:

Katika karne za mwanzo za imperial expansion pamoja na expansion of trade baina ya africa na maeneo ya ulaya, uarabuni na uchina ya sasa karne kadhaa kabla ya ukoloni, Wageni mbalimbali waliokuwa wanatembelea eneo lililokuja kujulikana baadae kama Tanganyika, walikuta eneo hili likiwa limegawanyika kutokana na himaya mbalimbali za uchifu kama historia inavyoelezea. Na katika maeneo haya, mengi yalikuwa na majina ambayo yalitungwa na wenyeji. Majina hayo ni kama vile Tabora n.k. Matukio kadhaa ya kihistoria yakafuatia baada ya interest za wageni hawa kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya bara ambalo leo linaitwa africa, na nisingependa kupoteza muda mwingi kujadili hayo kwani yapo wazi katika historia.

Lakini lipo tukio moja muhimu ambalo linastahili kuangaliwa kwa kina, nalo ni lile la "Mkutano Mkuu Wa Berlin" (The Berlin Conference) ambao uliitishwa na chancellor Bismark wa Ujerumani 1884/5. Mkutano huu ulilenga kugawanisha maeneo mbalimbali ya africa ya leo kwa mataifa makubwa ya wakati ule, hasa Uingereza, Ujerumani yenyewe, ufaransa, Ureno, italia. Lengo lilikuwa ni kuepusha mapigano na magomvi baina ya mataifa haya ambayo yote yalikuwa na nia moja tu: kutumia africa kwa manufaa ya uchumi wa mataifa yao nyumbani kwa njia ya kuchukua malighafi kutoka africa, exploit nguvu kazi ya waafrika kuzalisha mazao yaayohitajika mataifa makubwa, na kutumia africa kama masoko ya bidhaa zao. Katika mgawanyo huu wa maeneo mbalimbali, Eneo lililokuja kuitwa Tanganyika likachukuliwa na mjerumani ambae mbali na eneo hili, pia akapewa maeneo mengine ya karibu ambapo yote kwa pamoja, akayaita "Deustche Ost Africa" kwa maana ya "German East Africa". Suala la mipaka iliyowekwa ni suala ambalo nisingependa kulijadili kwa kina kwani lipo wazi katika historia ya msingi.

Kufuatia vita vya kwanza vya dunia ambayo kimsingi ilitokana na mjerumani kutaka kujitwalia maeneo ya wenzake kwa vile alikuwa ni late comer in the scramble and partition of Africa, vita hivi vilimalizika kwa mjerumani kushindwa. Uamuzi uliofuatia wa umoja wa mataifa wa wakati ule (The League of Nations), ukawa ni pamoja na kumpokonya mjerumani maeneo aliyopewa 1884/5 kama adhabu ya uchokozi wake kwa mataifa mengine lakini pia kama njia ya kumvunja nguvu kiuchumi ili asiwe na uwezo tena wa kusababisha vita na maafa kwa wenzake. Kuelekea mwaka 1920, German East Africa ikagawanywa kwa mataifa mengine makubwa huku eneo ambalo lilikuja kuitwa Tanganyika, likawekwa chini ya uangalizi (sio ukoloni) wa mwingereza.

Kwa vile jina la German East Africa lilitungwa na wajerumani, mataifa makubwa yaliyopewa maeneo haya kuyasimamia wakalazimika kuyapa majina mapya kwa nia ya kukamilisha mchakato wa kuyatawala.

JINA TANGANYIKA: LILITOKA WAPI?

Tofauti na mjerumani ambae alijulikana kwa mtindo wake wa kutawala usio na demokrasia (direct tule), mwingereza yeye aliheshimu demokrasia, hivyo kutawala kwa "indirect rule" ambapo machifu wa kienyeji walipewa baadhi ya mamlaka kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika makoloni husika.

Wawakilishi wa serikali ya uingereza katika eneo lililokuja kuitwa Tanganyika baadae, wakashauri majina yafuatayo ndiyo yatumike kutambulisha eneo husika:

1. New Maryland - serikali ya uingereza ikalikataa.

2. Smutsland - likakataliwa.

3. Victoria - likakataliwa.

4. Ebumea - likakataliwa.

5. Windsorland - nalo likakataliwa.

Sababu ya msingi ya serikali ya uingereza kukataa majina haya ni kutokana na utamaduni wake wa kutawala kwa "indirect rule" kwa nia ya kupanua demokrasia, hasa baada ya kuonja joto ya jiwe kipindi cha kabla katika makoloni yake mbalimbali ambapo sera zake hazikuwa tofauti sana na za mjerumani. Kwahiyo Serikali ya Uingereza ikapendekeza kwamba eneo husika lipewe jina litokanalo na asili yake. Katika mashauriano ya hapa na pale, majina kama Tabora na Kilimanjaro yalipendekezwa, lakini hayakupita. Hatimaye jina "Tanganyika" likapendekezwa na kupendezesha wengi. Hii ilikuwa ni mwaka 1920. Asili ya Jina hili ilitokana na wenyeji wa maeneo ya magharibi waliokuwa wanaishi katika maeneo ya ukanda wa ziwa TANGANYIKA. Jina hili lilitungwa na wenyeji muda mrefu uliopita, na wageni walilikuta likitumika tayari. Kwahiyo kufuatia eneo lile kupewa uzito sana kiuchumi na mjerumani, na pia kufuatia uwepo wa rasilimali muhimu ile ya ziwa Tanganyika, serikali ya uingereza ikaridhia na kulipitisha jina hilo la Tanganyika litumike katika eneo lote ambalo lilikuwa chini ya mwingereza. Tanganyika sasa ikaongezewa neno "protectorate", na kuanza tambulika rasmi kama "Tanganyika Protectorate". Muda sio mrefu, protectorate ikatolewa na kuwekwa "territory", hivyo Tanganyika Territory mwaka huo huo wa 1920.

Kwa maana hii:

*Jina Tanganyika asili yake ni wenyeji walioishi Tanganyika kabla hata ya ujio wa wageni.
*Tanganyika ni jina lililotambulisha nchi/territory husika kwa miaka 41 ya ukoloni na mingine mitatu ya uhuru kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 1964.

Kwa maana hii, jina la Tanganyika liliishi kwa karibia miaka 44.

Baada ya muungano, Tanzania emerged as a new state, nchi ambayo haikujengwa kwa mujibu wa katiba iliyopendekezwa na makubaliano ya mkataba wa muungao (1964), hivyo serikali husika kuwa almost unconstitutional. Lakini kilichookoa serikali ile na kuipa uhalali ikawa ni masuala nje kabisa ya katiba:

1. Historia ya TANU kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi.
2. Azimio la arusha (1967) ambalo lilifufua matumaini ya wananchi wengi kwamba kila aina ya unyonjaji, tofauti za vipato, matabaka, udini na ukabila vitatokomezwa, huku matunda ya uhuru yakipatikana.
3. Uwepo wa Nyerere mwenye charisma na integrity unmatched katika africa na dunia ya tatu ya wakati ule.

Haya yakawa ni masuala tosha ya wananchi kuipa TANU/CCM uhalali wa kutawala bila ya kujalisha katiba ya nchi inasema nini au inawa affect vipi wananchi.

Pamoja na mafanikio haya, suala la katiba mpya inayoakisi historia ya taifa likawa ni suala la kukwepa kwa muda tu. Kama tutakavyoona baadae, sakata la Jumbe na mengine yaliyofuatia yalikuwa ni mwanzo wa questioning CCM's constitutional legitimacy, kitu ambacho hadi leo is still questionable.


Inaendelea bandiko linalofuatia...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi naomba unipe rejea (references) kuhusu hili:

Wawakilishi wa serikali ya uingereza katika eneo lililokuja kuitwa Tanganyika baadae, wakashauri majina yafuatayo ndiyo yatumike kutambulisha eneo husika:

1. New Maryland - serikali ya uingereza ikalikataa.

2. Smutsland - likakataliwa.

3. Victoria - likakataliwa.

4. Ebumea - likakataliwa.

5. Windsorland - nalo likakataliwa.

Natanguliza shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea kutoka bandiko #3


Suala lingine muhimu pia nia kwamba, licha ya Tanzania kuwepo kama taifa kwa miaka 50, taifa hili has never been consistent sio tu na matakwa ya wananchi bali pia juu ya nini taifa hili linataka kuwafanyia wananchi. Kwa mfano:

*Mwaka 1961-1966 - Tanzania was a "party state". Lengo kuu katika kipindi hiki lilikuwa to create and sustain a new order kufuatia uhuru. Viongozi wetu wakiongozwa na Nyerere hawakuwa na uzoefu na masuala ya madaraka, hivyo it became prudent to secure their own position at the helm of the state.

Mwaka 1967-1985- Tanzania ikageuka kuwa "developmental state". Lengo kuu katika kipindi hiki likawa kwamba kuleketea wananchi matunda ya uhuru kwani viongozi muda sio mrefu wakabaini kwamba walihitajika kuonyesha uwezo wa kuendeleza nchi zao kiuchumi, na matokeo yake yawe katika maendeleo ya kijamii - maji elimu afya n.k.

Mwaka 1986 - hadi leo (2014), our state has shifted from that of being developmental to "CONTRACTING STATE". Tofauti na kipindi cha nyuma, serikali ikapoteza umiliki wa dira yake ya taifa na sera kwa ujumla na kuzihamishia kwa mataifa makubwa kupitia mashirika ya kimataifa ya fedha - IMF na World Bank. Since then, serikali imekuwa ikiimbia ubeti wa uliberali na kuchezeshwa na wakubwa hawa wa nje. In the process, the state has been contracting in terms of kuwahudumia wananchi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Wananchi hawakuandaliwa kuingia kwenye soko huria na serikali ikaamua kuwaingiza kwenye mfumo huo kiholela. Serikali kupitia chama baadae ikalifuta azimio la arusha kimya kimya mwaka 1992, na tangia wakati huo, wananchi walio wengi wamekuwa wanaishi maisha ya kuokoteza okoteza. Wataganyika ambao ndio wengi katika muungano huu ambao sasa umebakia kuwa ni ushirikiano baada ya ule ulioasisiwa na Nyerere na Karume kuvunjwa na Katiba ya Zanzibar (2010), badala ya viongozi kuwaokoa watanganyika na kusema sasa basi, imetosha, na nyie mnahitaji Tanganyika yenu ambayo mtakuwa na fursa ya kujipangia mambo yepi yawe yenu na yepi yawe ya pamoja, viongozi hawa wameamua mchana kweupe kuwadhulumu wananchi wa Tanganyika haki yao, haki waliyojichagulia kupitia tume ya katiba - autonomy, self determination, hence fostering of democracy.

CCM inasahau kwamba wananchi hawajakataa muungano bali wamekataa mfumo wa muungano ambao, kwanza haujawaletea neema yoyote wananchi wa pande zote mbili zaidi ya madaraka kwa kada ya watu fulani, lakini muhimu zaidi, muungano unaotetewa na ccm leo ni wa "nchi mbili, serikali mbili". Huo sio muungano aliotuachia Nyerere, ndio maana tutaupinga kwa kila namna.

CCM inasahau kwamba wananchi hulinda yale tu wanayoshirikishwa kuyatengeneza, na katika hili, suala la mfumo wa muungano linalopiganiwa na ccm will not be the creation of the peole bali CCM. Kwahiyo watakaoulinda muungano huu tena kwa gharama za wananchi (kodi) na pengine kwa gharama zitakazoathiri maisha ya wananchi iwapo mabomu yatatumika kuulinda mfumo wa aina hii, hao watakuwa ni CCM, na watabeba lawama zote.

Mwalimu Nyerere kupitia gazeti la Observer la uingereza, toleo la tarehe 20 Aprili alinena hivi:

Iwapo umma wa wazanzibari bila ya ushawishi wowote kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa muungao una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana

Miaka 46 baada ya maneno haya ya Mwalimu, leo umma unatishiwa mabomu na vifaru. Na sio kwamba kwasababu hawautaki muungano, bali kwa sababu (1) Mfumo wa serikali mbili umeleta hasara kuliko faida kwa miaka 50 (2) Muungano wa Mwalimu na Karume haupo tena, umevunjwa na zanzibar 2010. Kwahiyo wananchi wanataka mapungufu yafanyiwe kazi ili kuboresha na kudumisha muungano kwani serikali mbili zinazidi kuudhoofisha, na serikali moja ni jambo lisilowezekana. Halikuwezekana miaka 50 iliyopita ambapo Mwalimu mwenyewe alipinga, sembuse leo wakati the union question has always remained to be the Zanzibar Question?

Kwa vile suala la Tanganyika lilikataa kukaa chii ya zulia baada ya sakata la jumbe 1984, tukio jingine muhimu la kihistoria katika harakati za kuizindua Tangayika lilikuwa 1993 kupitia sakata la G55. Katika hili pia, Mwalimu alitetea mfumo uliopo kwa hoja, lakini muhimu zaidi, akiwa anapinga kukiukwa kwa katiba ya muungano uliotambua Tanzania kama nchi moja. Leo utetezi wa muungano katika mazingira ya nchi mbili serikali mbili unajengwa kwa misingi gani ya hoja?

Tutambue kwamba kutokana na mapungufu yaliyopo pamoja na uchakachuaji wa historia yetu watanganyika, sio tu kwamba tunaweza anza upya kwa manufaa ya vizazi vyetu vikavyo, bali tuna haja ya kuanza upya na kulipatia taifa letu la Tanganyika Dira na Self Determination. Hivyo ndivyo majirani wetu wataweza tuamini katika muktadha wa shirikisho la Afrika Mashariki ambalo Mwalimu katika kikao cha OAU, Julai 1964 jijini Cairo alisema (yameukuliwa pia kwenye kitabu cha Mwalimu cha "Uhuru na Umoja", 1966, Ukurasa 300-304:

Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilohgawika, ndilo nataka liwepo. Hii haina maana huku ni kuwa na serrikali moja kwa bara lote,katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote. Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo fulani fulani. Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani na sio kutoka serikali kuu. Hii ni sawa na kusema kuwa Africa mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zitagawiwa baina ya serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo.

CCM, huu ndio wosia wa Mwalimu katika nyakati za leo. Msikilizeni kama mna ia ya kuokoa muungano wetu. CCM imeachia Zanzibar ivunje katiba ya muungano kupitia katiba ya zanzibar ya 2010. Katika hili, Mwalimu kupitia hotuba zake ambazo zimejaa "youtube" anasema kwamba:

"Iwapo watangayika watavunja muungano kwa hoja ya sisi watanganyika na wao wazanzibari, wataganyika hawatabaki salama.
Lakini iwapo wazanzibari watavunja muungano kwa hoja za sisi wazanzibari, na wao watangayika, wao hawatabaki salama bali watanganyika watabak salama"

Wazanzibari wamevuja muungano tayari kwani tofauti na katiba ya JMT (2010), Tanzania ni nchi mbili. Lakini walichofanya zanziba ni hatua muhimu kwao kuelekea mamlaka kamili na ya kweli ndani ya muungano kwani hayawezi patikana bila ya kuzinduliwa kwa Taganyika. CCM ina fursa ya kuokoa muungano na pia wazanzibari kwa kuizindua Tanganyika, vinginevyo bila ya kuizindua Tanganyika, wazanzibari hatimaye watauvunja muungano kwa hoja ya sisi wazanzibari, na wao watanganyika. Na katika hili, Mwalimu alituhakikishia kwamba watanganyika tutabaki salama. Swali linalofuatia ni je, lengo la ccm ni kuizuia Tanganyika ili zanzibar hatimaye ivunje kabisa muungano kisha sisi watanganyik tuishie kushuhudia ndugu na majirani zetu wakimalizana sababu tu sisi tutakuwa salama kama Tanganyika? Sidhani kama hii ndio njia ambayo CCM ndio inapendelea Tanganyika irudi, kama itarudi. Tukifika huko, ccm ijue tu ingeweza epusha maafa yote.

Wananchi wenzangu, TANGANYIKA ndio ASILI YAKO, Usidanganyike na muungano wa Kisiasa fraught with Legal Manipulation and Political Expediency. Tukiendelea kuendekeza haya, ni hatua ya kutojali well being ya vizazi vyetu vijavyo.
Nguruvi3, tunaomba somo lako kuhusu hoja ya Waziri Mku Pinda na Tanganyika.

Itaendelea kwa utaratibu ulioanishwa bandiko #1 .

TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi
Pinda alipokuwa anahutubia jumuiya ya wazazi wa CCM Dodoma alikuwa na hoja hizi:
1. Kwamba, wanaotaka Tanganyika, wanaitaka ipi, kabla ya ukoloni au miaka 3 baada ya uhuru (1961-1964)
2.Tatizo la muungano wa serikali 2 ni Zanibar kukosa utambulisho wake
3.Tatizo la Watanganyika kunyimwa ardhi znz halina mashiko kwasababu znz ina ardhi ndogo
4. Watu wengi wanaoishi sasa hivi hawajui Tanganyika, bali Tanzania.

Pinda alizaliwa mwaka 1948 wakati huo Tanganyika ikiwa chini ya Waingereza kama UN trust territory ' na gavana wake akiwa Sir William Dennis Battershil.
Hivyo kwa uzawa, Mh Pinda ni Mtanganyika zaidi ya wengi waliopo hai hadi sasa.
Cheti chake cha kuzaliwa ni cha Tanganyika, eti leo kaitambui kwasababu ya Tanzania! jamani Mizengo!

Wakati anazaliwa mkutano wa Tanganyika African Association( ulifanyika mwaka mmoja kabla) pengine wazazi wake wakiwa katika ndoa au akiwa njiani kuja Tanganyika.

Tanganyika African Association (TANU )ilipoasisiwa mwaka 1954 Pinda alikuwa na miaka 6.
Tukipata Uhuru kutoka kwa Richard Turnbull Pinda alikuwa na miaka13 ikimaanisha alishaanza shule, na alishuhudia uhuru wa Tanganyika kwa macho yake mwenyewe akiwa kijana mkubwa tu.

Hadi hapo tunaona Pinda ameishi chini ya magavana wa Tanganyika wawili, amesoma katika Tanganyika iliyokuwa chini ya udhamini wa UN na maandishi yake shuleni yalihusiana na historia ya Tanganyika.

Tanganyika ilikuwepo miaka mingi sana kabla ya Pinda kuzaliwa. Kilichotokea ilikuwa ni wakoloni kubadilisha nyakati za utawala, lakini Tanganyika ilikuwa ile ile na watu wale wale.

Hata Pinda baada ya uhuru hakubadili uraia kutoka Tanganyika ya mkoloni kwenda Tanganyika ya miaka 6 baadaye. Wala hakuulizwa cheti za kuzaliwa kingine hadi leo hii pale Dodoma.
Tanganyika ya ukoloni anaitoa wapi Mzee Kayanza.

Mwaka 1964 Pinda alikuwa na miaka 16. Kwa nyakati hizi alikuwa kidato cha kwanza huenda.
Muungano wa 1964 ulikuwa wa Tanganyika na Zanzibar.

Mwaka 1965 katiba ya muda ikiandikwa Pinda alikuwa na miaka 15 tukiwa na Tanganyika na znz
Mwaka 1967 sheria namba 24 iliyoifuta Tanganyika ikitekelezwa Pinda alikuwa na miaka 19

Mpaka hapa alipokuwa na miaka 19 tulikuwa na Tanganyika na Zanzibar.
Hivyo kwanza amepotosha kusema Tanganyika ya Wakoloni, na pili amepotosha kusema Tanganyika ya miaka 3. Tanganyika ya awali ilifutika mwaka 1967, miaka karne nyingi tangu iwepo

Mwaka 1974 Pinda alikuwa kazini kama wakili wa serikali. Hiyo ni miaka 2 tangu Karume afariki na Aboud Jumbe awe Rais. Pinda anafahamu ZNZ kuliko waijuavyo wengi.

Mwaka 1978 alikuwa ofisi ya Rais ikiwa ni mwaka mmoja baada ya katiba ya JMT ya 1977 iliyounda Tanzania bara na Tanzania zanzibar. Pinda alikuwa na ufahamu mzuri tu jinsi Tanganyika ilivyotoweka mwaka 1967 na kukomelewa msumari mwaka 1977

1982 hadi 1992 alikuwa katibu myeka masadizi ofisi ya Rais hivyo alishuhudia kuandikwa kwa katiba ya kwanza ya Zanzibar. Alichosahau ni kuwa Zanzibar ni ile iliyoungana na Tanganyika, na sasa anatuaminisha znz iliungana na Tanzania. Huu ni usahalifu mbaya sana kwa mtu aliyeshuhudia matukio yote.

2010 Zanzibar ikifanya marekebisho ya katiba yake na kuifanya iwe nchi kamili ikiwa na kila kitu pamoja na vikosi vya majeshi na Amir jeshi wake, Pinda ni Waziri mkuu wa JMT.

Alichoshindwa kutambua ni kuwa Znz ilikuwa nchi kutoka wapi? na kwanini iwe nchi na Tanzania iwe znz? Hapa ndipo aliponukuliwa akisema hana ufahamu wa Tanganyika.

Kwa historia tu, Pinda ni Mtanganyika mzoefu kuliko wengi. Ameishi, amekulia na kusoma Tanganyika, Kitendo cha kusema haijui Tanganyika ni ulaghai usio na chembe ya haya.
Ni rahisi kwa Pinda kutamka Tanganyika kama 'mother tongue'' kuliko Tanzania.

Tuendelee...
 
UTAMBULISHO WA ZNZ
Pinda anataka znz ipate utambulisho. Akiwa mwanasheria kitaaluma ameshindwa kutambua mkataba wa muungano ulikuwa baina ya nchi ngapi na nini kilitokea akiwa ofisi ya rais kwa matukio tuliyoyaorodhesha hapo juu.

Katiba ya 2010 ambayo iliiyoondoa znz katika JMT kimantiki imeipa znz uwezo wa kutambulika kama nchi kwa jina, bendera, wimbo wa taifa, Rais, BLW, vikosi vya ulinzi na usalama.
Hayo yametokea machoni mwa Pinda akiwa waziri mkuu, mshauri mkuu wa pili wa Rais wa JMT.

Pinda hakumbuki yeye kama waziri mkuu hana uwezo wa kuzungumza na masheha katika shehia yoyote kule znz kwa capacity ya waziri mkuu.

Uwaziri mkuu wake unaishia bara kwasababu ZNZ ina uongozi kamili na yeye hana lake hata kwa bahati mbaya. Ni kutokana na hilo hana utambulisho znz na ni kitu cha ajabu anapodai znz ipewe utambulisho.

Znz inao utambulisho,kilichokosekana ni mshirika wa znz katika JMT ambaye ni Tanganyika.
Katika mazingira ya kwaida Pinda alipaswa kulia kuliko kuitafutia znz utambulisho.

Angeangua kilio kwasababu ile nchi aliyozaliwa Tanganyika imetoweka katika mazingira tatanishi.
Pinda hana kumbu kumbu za uwepo wa Tanganyika kama alivyosema.

Katika hali isiyo ya kawaida, mapendekezo ya Pinda kule Dodoma kama waziri mkuu lazima yaende baraza la wawakilishi znz kupewa baraka zote.

Endapo Pinda anapendekeza ujenzi wa vyoo vya shule basi kama waziri mkuu lazima apate ridhaa ya BLW znz kama ilivyo katika katiba ya znz iliyofanyiwa marekebisho 2010.

Ni kwa muktadha huo, Pinda anaitambua znz zaidi kuliko sisi wa mitaani kwasababu hawezi kutekeleza majukumu yake hadi pale Pandu Kificho na wenzake 50 wanaoitwa BLW watakapokubali.

Kinachomsumbua mzee Kayanza ni usahaulifu wa historia pengine kutokana na majukumu mengi ya kazi au tatizo la kibinadamu la kumbu kumbu hafifu.

WATANGAYIKA KUNYIMWA ARDHI
Hili Pinda analiona dogo sana lakini kwa wananchi wa nchi moja ni kubwa.
Nguvu ya soko huamuliwa na soko lenyewe.

Itakuwa ni kituko mtu kwenda kununua ardhi ya sh milioni 50 kwa ekari moja kuliko kununua mashamba Tanganyika.Hata hivyo katika misingi ya utaifa znz haipaswi kuweka vikwazo hivyo.

Hii maana yake ipo siku Kilimanjaro nao watasema hivyo na Pinda takubaliana nao.
Sheria ya ardhi iimemlenga Mtanganyika kwasababu Mkenya na mtaliano au Mwarabu hawaguswi na sheria hiyo.Ni ubaguzi huu ndio unapelekea Watanganyika kujiuliza kama sisi ni taifa.

Ubaguzi wa ardhi ni sehemu tu ya ubaguzi unaoendelea visiwani ukiwalenga Watanganyika na si raia wa eneo lingine.

Katika nchi moja znz haitambui leseni ya Tanzania bara,na kazi ni kwa kibali achilia mbali ukazi.
Kama waziri mkuu Pinda alipaswa kuliangalia hili tatizo kwa upana wake zaidi hasa katika ubaguzi na wala si kwa mtazamo hafifu finyu na potofu alioutoa.
 
WATU WENGI WANAOISHI HAWAIJUI TANGANYIKA

Pinda anshindwa kuelewa kuwa historia haindikwi bali inajiandika.
Kama tulikuwa taifa moja lilittokana na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar na kuzaa Tanzania, na sasa ZNZ imejitoa kwanini kusiwepo na serikali ya Tanganyika.

Uwepo wa serikali ya Tnganyika ni njia ya kuondoa malalamiko na kudumisha muungano na wala si kuvunja

Kizazi kikubwa cha sasa hakijui Tanganyika lakini kinahoji hii Tanzania ni nchi iliyopata uhuru lini na kutoka wapi?

Kinahoji hivyo kwasababu kama mtu haruhusiwi kuishi znz ambayo ni sehemu ya Tanzania, hiyo Tanzania ni nchi gani.

Kutokana na maswali hayo kizazi kimebaini kuwa jina Tanzania linatumika kwa ajili ya miradi na wala si kama taifa.

Leo Watanganyika wakawaida wanajua zile gharama za umeme wanazotozwa kumbe zinakwenda nchi jirani.

Wanajua kuwa kodi zao za kusomesha watoto zinaishia kuendesha serikali ya nchi jirani.
Wanajua gharama za ulinzi na usalama ni zao na kwamba nchi jirani haina mchango.
Wanajua kuwa kumbe ajira zinazotolewa kwa wznz ni kwasababu wao ni ma TX wa nchi jirani.

Huko vyuoni, wanafunzi wanasoma kwa mikopo ambayo hutakiwa kurudisha wakati wakitembea na bahasha za khaki.

Kwa vile nafasi zao za kazi kama Watanganyika wamepewa vijana wa nchi jirani, wao wanaendelea kusaga lami.

Kibaya zaidi, wanalipa mikopo wakiwa hawana kazi.
Wenzao wa nchi jirani ya znz wanasoma bure na kpata ajira kwasababu ni wznz.

Kizazi hiki kinachosononeka kitalipa mikopo ambayo miaka 3 ijayo itatolewa kama 'grant' kwa wanafunzi kutoka nchi ya kigeni ya zanzibar.

Lakini pia wanajiuliza kama wenzetu wanaserikali yao sisi ya kwetu iko wapi?
Hii inayoitwa ya muungano mbona ni mzigo kwetu?
Muungano gani ambao mmoja anachangia na mwingine anadokoa?

Kizazi hiki kimeamka na kinataka turejee maiaka 16 baada Pinda kuzaliwa.
Kwa bahati nzuri wazee walioishi Tanganyika kama akina Salima Ahmed , Butiku na Warioba na Augustino Ramadhani wakiongozwa na jopo la wasomi wameona hatari iliyo mbele.
Hatari hiyo ni kuparaganyika kwa taifa, kuendelea kwa chuki na kuvunjika kwa umoja.

Ndio maana tume ya Warioba ikasema mambo yawe 7, hayo mengine kila mtu ashughulike kivyake.

La sivyo, basi tukubaliane kuwa jahazi limeingia maji, tugawane mbao na misumari.

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3,

Shukrani kwa darasa lako muhimu ambalo limelenga kuingia kwa undani zaidi kufafanua nini ni asili ya Tanganyika katika muktadha wa kauli yetu mbiu ya "TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA." Umeijadili vyema hoja ya Waziri Mkuu Pinda na kuonyesha bayana jinsi gani hoja yake ilijaa upotoshaji. Kwa kuongezea tu katika hilo, ni muhimu tuweke msisitizo ufuatao:

1. Mwaka 1885 ndio mwaka rasmi ambao nchi iliyokuja kuitwa Tanganyika iliwekewa mipaka yake, na kwa kuanzia ikapewa jina la "German East Africa".

2. Mwaka 1920 - eneo hili la German East Africa likagawanywa kwa mataifa makubwa ya wakati ule kufuatia defeat ya ujerumani kwenye vita vya dunia 1918/19. Kwa mfano eneo moja wapo la german east africa - rwanda, likaenda kwa mfaransa, huku eneo tunaloishi sasa likipatiwa jina la "Tanganyika Territory na Taganyika Protectorate baadae kama nilivyokwisha jadili;

3. Mwaka 1961, Tanganyika ikapata uhuru ambapo neno "protectorate" likaondolewa na kubakishwa "Tanganyika" huru.

4. Mwaka 1962, tukapata katiba yetu na kuwa Jamhuri, hivyo kuitwa "Jamhuri ya Tanganyika".

5. Mwaka 1964, tukaungana na zanzibar na katika hili ni muhimu turekebishe upotoshaji wa Waziri Mkuu Pinda pale anaposema "Tanganyika" iliishia mwaka 1964. Katika hili, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, Pinda hajasema ukweli kwani:

Mkataba wa Muungano wa Aprili 26, 1964 unasema hivi:

Mkataba wa Muungano Baina Ya Jamhuri Ya Tanganyika na Jamhuri Ya Watu Wa Zanzibar.

Hivyo ndivyo muungano wetu ulivyotambulishwa na kutangazwa. Na hata vyombo vya habari vya mataifa ya nje yalitamka hivyo.

Kwahiyo tofauti na hoja ya Pinda kwamba Jina la Tanganyika liliisha mwaka 1964,

6. Mwaka 1964-1965 - taifa letu lilitambulika kama:

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanganyika Na Zanzibar

Kwa maana hii, mkataba wa muungao (1964) ambao ulitambua utambulisho huu, ulikuwa bado unaheshimika angalau kwa utambulisho wa taifa letu.

Kama anavyojadili Nguruvi3 hapo juu, Pinda ni mwanasheria by profession, hivyo alitakiwa awe na uelewa juu ya masuala muhimu ya kisheria yanayohusisha muungano wetu. Kwa mfano, aidha kwa kujua au kutokujua, Pinda anasahau kwamba hata sheria za kwanza kabisa za muungano, bado zitaitaja Tanganyika:

Sherria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 1964, Na. 22 ya 1964.

7. Mwaka 1965-1977

Hiki kilikuwa ni kipindi cha katiba ya muda iliyotungwa mwaka 1965. Ni katika kipindi hiki kama anavyojadili Nguruvi3, sheria ya mabadiliko namba 24 ya 1967 ikapitishwa kuiua Tanganyika na kuileta Tanzania bara.

Watanganyika hawakujali sana kwani kama nilivyoeleza huko nyuma, uhalali wa serikali ya nyerere kutoka kwa wananchi haukuwa ni kwa mujibu wa katiba bali uadilifu wa nyerere na uwezo wake mkubwa, baadae azimio la arusha lakini pia historia na mafanikio ya tanu kutetea wanyonge, so umma haukujali sana legitimacy ya tanu na serikali yake itokane na katiba; lakini pia, kwa vile tanu ilishika hatamu kwa kujipenyeza kwenye katiba ya muda (1965) huku katiba hiyo ikitamka kwamba TANU kitakuwa ni chama pekee Tanzania, umma haukujali sana kupoteza serikali ya Tanganyika kwani serikali hiyo iliitwa ya Tanzania/Tanzania bara huku nani akiwa juu ya masuala yote ya muungano na yasiyo na muungao? Tanganyika National African Union (TANU), kwahiyo kimsingi, Tanganyika kwa wengi haikupotea, ilihamishiwa tu kwenye chama.

8. Mwaka 1977-2010

Mwaka 1977 Tanu ikaja na solution ya kuigeuza nchi kuwa moja na yenye serikali mbili kikatiba kwa kuunganisha vyama vya Tanu na asp; Katiba ya JMT (1977) ikaambatana na sheria iliyoifuta Zanzibar kama vile Tanganyika ilivyofutwa na sheria namba 24, 1967. Zanzibar ikabadilishwa kuwa "Tanzania Visiwani"; Wazanzibari wakashtuka kwamba hii ni kinyume cha mkataba wa muungano lakini worse, bila ya uangalifu, watajikuta ni sawa na visiwa vingine kama ukerewe, mafia, bongoyo n.k; hivyo wakafanya mabadiliko ya haraka katika katiba yao na kufutilia mbali jina "Tangayika visiwani" kwani haikuwa sahihi kwa katiba ya JMT (1977) kutamka kwamba ni muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Baadae tutajadili haya kwa undani zaidi.

Muhimu ni kwamba pamoja na mapungufu ya muungano, nyerere alisimamia hoja kwamba katiba ya JMT inakiukwa, kwa mfano wakati wa sakata la G55 1993, kwani katiba ilitambua Tanzania kama nchi moja.

9. 2010-2014

Kufuatia mabadiliko ya katiba ya znz, kimsingi sasa tuna nchi mbili na serikali mbili. Nyerere alishinda kwa hoja juu ya nchi moja, serikali mbili, je ccm inataka kushinda kwa hoja ya kutetea nchi mbili serikali mbili?wapo wapi wenye hoja hii tupambane kwa hoja?

Tunasikia mitaani kwamba ccm inashinikiza BLW wabadili kipengele kinachoitambulisha znz kama nchi. CCM ikae ikijua kwamba hili halitatokea kwani znz's grievances against mfumo wa muungano yani the union question has always been the zanzibar's question of autonomy and self determination. Hata tume ya warioba ilifanya utafiti iwapo znz wataweza badilisha kifungu husika cha katiba yao ya 2010. Baada ya utafiti wa kina kwa wananchi, wanasiasa na opinion leaders wenye influence ndani ya jamii ya znz, tume ikabaini kwamba znz hawawezi rudi tena nyuma. Katiba yao inasema ili kurudi nyuma, lazima iitishwe kura ya maoni na kupitisha maamuzi kwa two thirds. Tume imebaini hili haliwezekani, wazanzibari hawawezi kurudi nyuma, labda kama CCM ina mpango wa kuwarudisha nyuma kwa mabomu na vifaru. Sidhani, lakini kama wapo makada wachache wenye mawazo hayo, wakumbuke maneno ya Nyerere katika mahojiano na Gazeti la Observer la Uingereza, April 20th 1968 kwamba hatowapiga mabomu wale wote watakaopinga muungano na kuongeza kwamba iwapo umma utaona muungano haua faida kwao, basi kutakuwa haina haja ya kuuendeleza.

Kufikia hapa, umma wa znz na tanganyika hawapingi muungano, bali wanataka kuuendeleza kwa mfumo wanaoona unawafaa zaidi, na wengi wanapendelea serikali tatu. Lakini kuna kila dalili kwamba ccm imejipanga kukataa matakwa ya wengi kwa gharama zote.
Dingswayo, itakurudia na swali lako la reference.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kila siku kuna swali halijibiwi. Ni nini legal foundation ya muungano huu unaopigiwa debe wa serikali 2?

Legal foundation ya serikali 3 ni article of union ya mwaka 1964.
 
Kila siku kuna swali halijibiwi. Ni nini legal foundation ya muungano huu unaopigiwa debe wa serikali 2?

Legal foundation ya serikali 3 ni article of union ya mwaka 1964.

Baada ya utangulizi hapo juu kuhusu asili ya Tanganyika, katika bandiko linalofuata, nimedhamiria kujadili suala lililogusiwa na Nguruvi3 hapo juu - the legal foundation of the union/msingi wa kisheria wa muungano; Bandiko langu litakalofuata muda mfupi baadae litakuwa kama ifuatavyo:

SEHEMU YA KWANZA: JE NI MFUMO GANI WA SERIKALI ULIOKUSUDIWA NA MKATABA WA MUUNGANO (1964)?



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA KWANZA: JE NI MFUMO GANI WA SERIKALI ULIOKUSUDIWA NA MKATABA WA MUUNGANO?

Baada ya mkataba wa muungano kuwa siri kwa kipindi kirefu, hatimaye nyaraka hii sasa ipo hadharani na wananchi tumepata fursa ya kuichambua mstari kwa mstari. Nyaraka hii inapatikana katika vitabu vingi vilivyoandikwa ndani na nje ya nchi kama vile kitabu cha issa shvji (2007): Panafricanism or pragmatism? The lessons from the union of Tanganyika and Zanzibar. Nitakuwa narejea vifungu mbalimbali vya mkataba kuu kila inapobidi.

Kwa kuutazama mkataba wa muungano (1964), mfumo uliokusudiwa unaonyesha wazi kwamba ulikuwa ni ule unaoonyesha mgawanyiko wa wazi wa madaraka baina ya pande mbili kuu: Upande wa serikali kuu na upande wa sehemu zinazounda serikali kuu. Kwanza ni serikali za Tanganyika nna zanzibar ambazo zilikubali kuunda Jamhuri ya Muungano ambao uliitwa "Muungano baina ya Jamhuri Ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"; Ni kufuatia mkataba wenye utambulisho huu, jamhuri hizi mbili huru kwa hiari yao wakakubali kwamba watapunguza baadhi ya madaraka ya serikali zao kwa serikali hiyo mpya. Jamhuri mbili hizi zikasalimisha madaraka hayo (baadhi) kwa serikali mpya ya muungano ambayo ikapewa mamlaka pekee kwa jamhuri nzima kama ibara ya (iv) ya mkataba wa muungano ulivyoelekeza:

Mambo yafuatayo ndiyo yatakayokuwa chini ya Bunge na serikali ya jamhuri ya muungano:

1. Katiba na serikali ya jamhuri ya muungano.
2.Mambo ya nchi za nje.
3.Ulinzi
4.Polisi
5.Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari
6.Uraia
7.Uhamiaji
8.Mikopo na biashara ya nchi za je
9.Utumishi katika jamhuri ya muungano.
10. Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi, ushuru wa forodha a ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, posta na simu.

Mfumo huu ni dhahiri ulikuwa unalenga shirikisho na hii haikuwa ajabu kwani katika kikao cha OAU, Julai 1964 jijini Cairo alionyesha nia yake ya afrika yenye muungano wa mfumo wa shirikisho. Maneno haya yaechapishwa pia hapa [Julius K. Nyerere "The Nature and requirements of african unity, katika "African Forum, Vol 1. Na. 1 (1965), uk 46:

Bara lenyeukubwa wake kamili, moja na lisilohgawika, ndilo nataka liwepo. Hii haina maana huku ni kuwa na serrikali moja kwa bara lote,katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote. Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo fulani fulani. Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani na sio kutoka serikali kuu. Hii ni sawa na kusema kuwa Africa mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zitagawiwa baina ya serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo.

Kwa kuzingatia kifungu kile pale juu, kifungu (iv) cha mkataba wa muungano, pamoja na maneno ya baba wa taifa hapo juu, tukiachilia mbali mabadiliko yaliyojitokeza baadae, kilichosukuma dhamira kwa pande mbili kuungana kilikuwa kuanzisha kwa mfumo wa shirikisho.

Isitoshe, nia ya Mwalimu ilikuwa ni kuleta shirikisho la afrika mashariki ambapo zanzibar ingekuwa sehemu ya shirikisho hilo; chelewa chelewa ya Majirani zetu katika maamuzi ndio zikapelekea Mwalimu na Karume kuamua kufungua dimba kuonyesha mfano mwaka 1964. Ili kuthibitisha hoja hii, katika kikao cha Pan African Freedom Movement For East and Central Africa (PAFMECA) kilichofanyika Nairobi miezi kumi kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (5 Juni, 1963), Nyerere ambae alikuwa na ushawishi mkubwa sana katika suala zima la panafricanism alisema yafuatayo (Gazeti la Tanganyika Standard, 16/11/1964):

Sisi viongozi wa nchi za afrika mashariki tunajifunga kisiasa kuwa na shirikisho la afrika mashariki. Mkutano wetu wa leo unaongozwa na hamu ya kuunganisha bara la afrika na sio ubinafsi wa maslahi ya maeneo yetu. Leo ni siku ya vitendo katika kuelekea katika maadili tunayoyaamini na umoja na uhuru ambao sote tumeupatia mateso na kujitolea mhaga kwa ajili hiyo.

Zanzibar haikuwa katika kikao hiki kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa katika maandalizi ya uhuru lakini bado ilitajwa katika mpango ujao wa shirikisho la afrika mashariki. Viongozi hawa akiwepo nyerere wakaja na tamko kwamba (source: A Declaration of Federation by the Governments of East Africa on June 5th 1963, lenye kumbukumbu Na. 13/931/63 POT/1/1 kama ilivyochapishwa katika "meetings and discussions on the proposed East Africa Federation (Dar-es-salaam: Tanganyika Government, Ministry of Information):

Ingawaje Zanzibar haikuwasilishwa katika mkutano huu inatulazimu tuseme wazi kuwa nayo inakaribishwa kujiunga na mkutano huu wenye kulenga shirikisho. Mara tu baada ya zanzibar kumaliza taratibu zake za uchaguzi serikali yake itashirikishwa katika kamati ya kufuatilia jambo hilo au kamati nyingine ile itakayoanzishwa katika kufikia hilo shirikisho.

Kwahiyo tunaona jinsi gani Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya shirikisho la afrika mashariki envisioned na Nyerere, Kenyatta na Obote kabla ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Na ndio maana muungano wetu kupitia mkataba wa 1964 ukawa na lengo na structure ya kishirikisho kama nilivyokwisha jadili.

Kwa mantiki hii,ni wazi kwamba sio mamlaka ya zanzibar, wala ya Tanganyika yalitakiwa kuwa chini ya serikali ya muungano, wala serikali ya "Tanzania Bara".

Panapotokea ushirikiano baina ya mataifa mawili au zaidi, ushirikiano huu huwa unachukua sura moja kati ya hizi:

1.Serikali Moja:
Hali hii hutokea pale ambapo ushirikiano huo haujawa wa hiyari bali ni wa kulazimisha ambapo taifa moja lenye nguvu dhidi ya taifa jingine hulazimisha muungano wa serikali moja; mfano mzuri ni muungano baina ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini, muungano ambao ulizaa migogoro isiyo na utofauti sana na ile ya muungano wetu. Hapa tukumbuke kwamba Mwalimu baadae alikuja kusema kwamba tumeiga mfumo wa muungano wa uingereza (unitary system), lakini baada ya ujio wa vyama vingi, mfumo huu ukaleta kizaa zaa juu ya suala la makamu wa rais wa znz. Hii ni kwasababu kwa vile mkataba wa muungano (1964) ulikuja chakachuliwa baadae na TANU (tutaona kwa undani baadae) kwa kuingiza vyama vya siasa kwenye suuala la muungano kinyume na mkataba, lazima suala hili lingeleta matatizo baadae; kufuatia mfumo wa vyama vingi, bila ya mabadiliko ya haraka ccm ingejikuta ina rais wa Muungano kutoka ccm na wa zanzibar kutoka CUF 1995, hivyo nchi kuwa na rais wa jamhuri ya muungano kutoka chama kimoja cha siasa na makamu kutoka chama kingine. Mwalimu akabaini kwamba bila ya kurudi kwenye elements ya shirikisho, hali itakuwa ngumu. Hivyo Jaji Bomani akapewa jukumu la kutafuta ufumbuzi. Mapendekezo yake yakawa kuiga mfumo wa shirikisho wa marekani "mgombea mwenza kuwa ni makamu wa rais"; hadi leo tunatumia mfumo huo ambao ulitupatia marehemu Dr. Omari Ali Juma, Dr. Shein na sasa Dr. Bilal, kama makamu wa rais. CCM inapinga shirikisho wakati ni mfumo wa shirikisho ndio ulikiokoa chama nna aibu ya mwaka 1995.

Kwahiyo basi, mfumo wa serikali moja ni aina ya kwanza ya ushirikiano wa mataifa mawili au zaidi na huwa siyo wa hiari bali kulazimisha. Chini ya mfumo wa aina hii nguvu zote za mamlaka zinakuwa chini ya serikali ya "bwana mkubwa" anayesalimisha amri. Kwa kuitazama tu dhana hii ya serikali moja, tunaona kwamba haiendani na mkataba wa muuungano (1964) uliotiwa sahihi na Nyerere na Karume wakiwakilisha wananchi wao kama marais wa jamhuri mbili huru (kwa hiari).

Wale wote wanaotetea serikali moja ni lazima wafahamu kwamba the legal foundation of our union ni mkataba wa muungano, na hakuna misingi ya kihistoria wala kisheria inayoonyesha kilichodhamiriwa kilikuwa ni serikali moja.

Historia ni kitu ambacho hakiwezi chakachulika. Mwaka 1982, Machi 6, aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Joseph Warioba, alinukuliwa na Gazeti la Daily News aliyekuwa akijibu hoja ya professor srivastava aliyekuwa anajadili mapungufu ya katiba ya JMT (1977) na kusema kwamba:

Nina wasiwasi kuwa Profesa alikuwa akiitizama Katiba ya 1977 katika mtazamo wa kishirikisho ambapo ungeweza kuwa na serikali tatu tofauti. Nina uhakika waliotunga katiba ya jamhuri ya muungano(1977) hawakuwa na mawazo hayo vichwani mwao.

Tamko hili la Jaji Warioba akiwa Mwanasheria Mkuu wa serikali tena rais akiwa ni Mwalimu Nyerere ni ushahidi usio na mashaka kwamba wale wote wanaojenga hoja kwambalengo la Mwalimu lilikuwa kupelekea serikali moja baadae ni hoja isiyokuwa sahihi. Kwa maana nyingine, hata leo CCM wanapohoji kwanini wazo la serikali moja halikulewa sambamba na serikali tatu katika rasimu ni hoja isiyokuwa na maana kwani Katiba ya 1977 pamoja na mapungufu yake haikuweka provision zozote za kuelekea serikali moja. Lakini suala la serikali tatu ndilo lililojengewa misingi yake katika mkataba wa muungano (1964).

Itaendelea...


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi na Nguruvi3, wakati mnaendelea kutoa shule, na mimi niongezee tu my two cents...naona wengi hawajui hata hilo jina Tanzania lilitokea wapi! Kwa tuliokuwepo, tunakumbuka harakati zilizofanyika kutafuta jina muafaka la Taifa jipya baada ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Zanzibar. Mapendekezo yalikuwa mengi yakitokana na kukokotoa majina Tanganyika na Zanzibar lakini ninayoweza kuyakumbuka sana yalikuwa manne; Zanzibat Tanganyika (Zantan), Tanganyika Zanzibar (Tangibar), Tanganyika/Zanzibar (Tanzan) na Tanganyika/Zanzibar (Tanbar). Jina ambalo lilionekana kukubalika haraka lilikuwa Tanzan na kwa kweli lilianza kutumika hata kabla ya kupitishwa rasmi. Hata hivyo wajuzi wengine walijitokeza na kupendekea kuwa neno tanzan haliendani na msamiati wa Kiswahili, hivyo liishie na vowel moja au mbili. Kulikua na (a) Tanzana, (b) Tanzani, (c) Tanzania na TANZANIA ikaibuka mshindi.

Ninachotaka kusisitiza ni kuwa Tanzania ilitokana na majina mawili; Tanganyika na Zanzibar, na hivyo Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikaja kujulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hoja yangu hapa ni kuwakumbusha wote kwamba unapoitaja Tanzania tayari unazitaja Tanganyika na Zanzibar, hakuna jina lililopotea! Swali ni kwa nini ilitulazimu kufanya hivi? Kwa nini baada ya kuungana tukatafuta jina jipya badala ya kujiita tu Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Binafsi naamini hii ilikuwa ni kama transition tu kwa lengo la kuunda nchi moja yenye mamlaka moja. Kwa jinsi mambo yalivyo sasa, hii ndoto ni wazi imefutika na hasa baada ya kuanzishwa kwa nchi ya Zanzibar ndani ya Tanzania, na tukiacha siasa hata somo la hesabu hapa linagoma. Sababu na uwezo labda bado zipo lakini nia halipo kabisa na kuamini hivyo ni kudanganyana, Muungano kwishnei!
 
Inaendelea kutoka bandiko [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=1]#1 2[/URL] .

Mwishoni mwa bandiko [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=1]#1 2[/URL] tulianza mjadala juu ya sura kuu tatu ambazo ushirikiano wa kimataifa baina ya mataifa mawili au zaidi huweza chukua. Tulianza kwa kujadili serikali moja ambapo tukahitimisha kwa ushahidi kwamba serikali moja haikuwa tu sio lengo lilidhamiriwa na mkataba wa muungano (1964), bali pia Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977) haukudhamiria serikali moja wakati ule na hata kwa baadae; Mwanasheia mkuu wa serikali wa wakati ule (1982) Jaji Warioba alithibitisha hilo; sasa tuangalie aina ya pili na ya tatu ya sura za ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi mbili au zaidi kisha tupime iwapo sura hizo ndizo zilizodhamiriwa ndani ya mkataba wa muungano:

2. Matangamano ya serikali za majimbo.

Inapotokea kwamba nchi zaidi zaidi ya mbili, ridhaa yao, zimejileta pamoja, iwapo zinazidi mbili na zina lengo la kuungana, nchi hizo zinaweza kufikia makubaliano kwamba mamlaka halisi yabakie katika nchi moja moja husika. Chini ya mfumo huu, serikali kuu huwa haina nguvu na badala yake huwa inapewa tu madaraka. Mfano mzuri ni mfumo wa jumuiya ya ulaya (EU) ambapo tunaona kwamba nchi shiriki kama vile Ujerumani, ufaransa, uingereza, ugiriki n.k, zinaendelea kubakia na nguvu za juu kabisa za kujifanyia maamuzi yao, na sio bunge la jumuiya ya ulaya au viongozi wa jumuiya hii. Mfumo huu pia sio ule ulioelekezwa ndani ya mkataba wa muungano. Lakini hapa niseme tu kwamba kutokana na weak legal foundation ya muungano wetu, leo tupo pahala ambapo bunge la upande mmoja wa muungano (Zanzibar), limejinyakulia mamlaka ya kupitisha sheria zinazoathiri upande mwinginr wa muungano (Tanzania bara/Tanganyika), hata kama maamuzi hayo ni ya kusaidia kina mama wakulima wadogo wadogo Tukuyu; hapo ndipo ccm leo imetufikisha na mfumo wake wa serikali mbili.

3. Mwisho ni mfumo wa shirikisho.

Chini ya mfumo huu wa muungano, serikali kuu na serikali za mataifa yaliyopo ndani ya muungano hushirikiana katika maeneo kadhaa ya madaraka. Utekelezaji wake ni pamoja na ifuatavyo:

A) Kuanzishwa kwa muungano wa kisiasa baina ya nchi mbalimbali ili kila moja ibakie na utawala na uendeshaji wa mambo yake ya ndani/yasiyo ya muungano).

B) mfumo wa kisiasa ambapo nchi shiriki zinabakia na mamlaka karibia yote ya ndani (yasiyo ya muungano) na kubakisha masuala kama mambo ya nje, uhamiaji, ulinzi, uraia etc kuwa ni ya serikali kuu au shirikisho.

C) Katika kundi la nchi zilizoungana, kunakuwa na serikali moja inayosimamia mambo ya nje, ulinzi, uhamiaji, uraia, etc, lakini kila nchi shiriki ikibakia na mamlaka ya kuamua mambo yake yenyewe.

Kwa kuangalia mkataba wa muungano na kufananisha na maelezo ya mfumo namba tatu hapo juu, tunaona wazi kwamba hivyo ndivyo mkataba wa muungano ulidhamiria, sio serikali moja wala matangamano ya serikali za majimbo.

Kwa kusoma mkataba wa muungano, tunaona kwamba kilichodhamiriwa katika ibara zake ni mfumo ambao serikali kuu na zile shiriki katika muungano zitakuwa na nguvu zinazolingana - mfumo wa shirikisho ambao kunakuwa na mgawanyiko wa mahakama, bunge na urais baina ya serikali kuu na zile shiriki huku kila serikali ikiwa na nguvu zake kamili juu ya masuala yasiokuwa ya muungano;

Hoja hii inathibitishwa na kesi moja maarufu sana nchini marekani - Kesi ya Tarbles ya mwaka 1872 iliyoaumuliwa na mahakama kuu ya marekani kama ifuatavyo (tafsiri):

Kuna ndani ya mipaka ya eneo la kila jimbo, serikali mbili ambazo zinafungwa katika utendaji wao, lakini kila moja ikiwa huru kutoka nyingine na zenye sauti ya mwisho katika mamlaka ilizo hodhi. Kila moja ina idara zake, sheria zake pekee, na kila moja ikiwa na mahakama zake yenyewe za kukazia sheria hizo. Hakuna serikali inayoweza kuingia katika eneo la mamlaka ya nyingine wala kuamuru uingiliaji wa watendaji wake wa sheria katika matendo ya mwingine.

Itaendelea kwa mujibu wa yale yaliyoainishwa katika bandiko #1 .

TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Inaendelea kutoka bandiko #3


Suala lingine muhimu pia nia kwamba, licha ya Tanzania kuwepo kama taifa kwa miaka 50, taifa hili has never been consistent sio tu na matakwa ya wananchi bali pia juu ya nini taifa hili linataka kuwafanyia wananchi. Kwa mfano:

*Mwaka 1961-1966 - Tanzania was a "party state". Lengo kuu katika kipindi hiki lilikuwa to create and sustain a new order kufuatia uhuru. Viongozi wetu wakiongozwa na Nyerere hawakuwa na uzoefu na masuala ya madaraka, hivyo it became prudent to secure their own position at the helm of the state.

Mwaka 1967-1985- Tanzania ikageuka kuwa "developmental state". Lengo kuu katika kipindi hiki likawa kwamba kuleketea wananchi matunda ya uhuru kwani viongozi muda sio mrefu wakabaini kwamba walihitajika kuonyesha uwezo wa kuendeleza nchi zao kiuchumi, na matokeo yake yawe katika maendeleo ya kijamii - maji elimu afya n.k.

Mwaka 1986 - hadi leo (2014), our state has shifted from that of being developmental to "CONTRACTING STATE". Tofauti na kipindi cha nyuma, serikali ikapoteza umiliki wa dira yake ya taifa na sera kwa ujumla na kuzihamishia kwa mataifa makubwa kupitia mashirika ya kimataifa ya fedha - IMF na World Bank. Since then, serikali imekuwa ikiimbia ubeti wa uliberali na kuchezeshwa na wakubwa hawa wa nje. In the process, the state has been contracting in terms of kuwahudumia wananchi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Wananchi hawakuandaliwa kuingia kwenye soko huria na serikali ikaamua kuwaingiza kwenye mfumo huo kiholela. Serikali kupitia chama baadae ikalifuta azimio la arusha kimya kimya mwaka 1992, na tangia wakati huo, wananchi walio wengi wamekuwa wanaishi maisha ya kuokoteza okoteza. Wataganyika ambao ndio wengi katika muungano huu ambao sasa umebakia kuwa ni ushirikiano baada ya ule ulioasisiwa na Nyerere na Karume kuvunjwa na Katiba ya Zanzibar (2010), badala ya viongozi kuwaokoa watanganyika na kusema sasa basi, imetosha, na nyie mnahitaji Tanganyika yenu ambayo mtakuwa na fursa ya kujipangia mambo yepi yawe yenu na yepi yawe ya pamoja, viongozi hawa wameamua mchana kweupe kuwadhulumu wananchi wa Tanganyika haki yao, haki waliyojichagulia kupitia tume ya katiba - autonomy, self determination, hence fostering of democracy.

CCM inasahau kwamba wananchi hawajakataa muungano bali wamekataa mfumo wa muungano ambao, kwanza haujawaletea neema yoyote wananchi wa pande zote mbili zaidi ya madaraka kwa kada ya watu fulani, lakini muhimu zaidi, muungano unaotetewa na ccm leo ni wa "nchi mbili, serikali mbili". Huo sio muungano aliotuachia Nyerere, ndio maana tutaupinga kwa kila namna.

CCM inasahau kwamba wananchi hulinda yale tu wanayoshirikishwa kuyatengeneza, na katika hili, suala la mfumo wa muungano linalopiganiwa na ccm will not be the creation of the peole bali CCM. Kwahiyo watakaoulinda muungano huu tena kwa gharama za wananchi (kodi) na pengine kwa gharama zitakazoathiri maisha ya wananchi iwapo mabomu yatatumika kuulinda mfumo wa aina hii, hao watakuwa ni CCM, na watabeba lawama zote.

Mwalimu Nyerere kupitia gazeti la Observer la uingereza, toleo la tarehe 20 Aprili alinena hivi:



Miaka 46 baada ya maneno haya ya Mwalimu, leo umma unatishiwa mabomu na vifaru. Na sio kwamba kwasababu hawautaki muungano, bali kwa sababu (1) Mfumo wa serikali mbili umeleta hasara kuliko faida kwa miaka 50 (2) Muungano wa Mwalimu na Karume haupo tena, umevunjwa na zanzibar 2010. Kwahiyo wananchi wanataka mapungufu yafanyiwe kazi ili kuboresha na kudumisha muungano kwani serikali mbili zinazidi kuudhoofisha, na serikali moja ni jambo lisilowezekana. Halikuwezekana miaka 50 iliyopita ambapo Mwalimu mwenyewe alipinga, sembuse leo wakati the union question has always remained to be the Zanzibar Question?

Kwa vile suala la Tanganyika lilikataa kukaa chii ya zulia baada ya sakata la jumbe 1984, tukio jingine muhimu la kihistoria katika harakati za kuizindua Tangayika lilikuwa 1993 kupitia sakata la G55. Katika hili pia, Mwalimu alitetea mfumo uliopo kwa hoja, lakini muhimu zaidi, akiwa anapinga kukiukwa kwa katiba ya muungano uliotambua Tanzania kama nchi moja. Leo utetezi wa muungano katika mazingira ya nchi mbili serikali mbili unajengwa kwa misingi gani ya hoja?

Tutambue kwamba kutokana na mapungufu yaliyopo pamoja na uchakachuaji wa historia yetu watanganyika, sio tu kwamba tunaweza anza upya kwa manufaa ya vizazi vyetu vikavyo, bali tuna haja ya kuanza upya na kulipatia taifa letu la Tanganyika Dira na Self Determination. Hivyo ndivyo majirani wetu wataweza tuamini katika muktadha wa shirikisho la Afrika Mashariki ambalo Mwalimu katika kikao cha OAU, Julai 1964 jijini Cairo alisema (yameukuliwa pia kwenye kitabu cha Mwalimu cha "Uhuru na Umoja", 1966, Ukurasa 300-304:



CCM, huu ndio wosia wa Mwalimu katika nyakati za leo. Msikilizeni kama mna ia ya kuokoa muungano wetu. CCM imeachia Zanzibar ivunje katiba ya muungano kupitia katiba ya zanzibar ya 2010. Katika hili, Mwalimu kupitia hotuba zake ambazo zimejaa "youtube" anasema kwamba:

"Iwapo watangayika watavunja muungano kwa hoja ya sisi watanganyika na wao wazanzibari, wataganyika hawatabaki salama.
Lakini iwapo wazanzibari watavunja muungano kwa hoja za sisi wazanzibari, na wao watangayika, wao hawatabaki salama bali watanganyika watabak salama"

Wazanzibari wamevuja muungano tayari kwani tofauti na katiba ya JMT (2010), Tanzania ni nchi mbili. Lakini walichofanya zanziba ni hatua muhimu kwao kuelekea mamlaka kamili na ya kweli ndani ya muungano kwani hayawezi patikana bila ya kuzinduliwa kwa Taganyika. CCM ina fursa ya kuokoa muungano na pia wazanzibari kwa kuizindua Tanganyika, vinginevyo bila ya kuizindua Tanganyika, wazanzibari hatimaye watauvunja muungano kwa hoja ya sisi wazanzibari, na wao watanganyika. Na katika hili, Mwalimu alituhakikishia kwamba watanganyika tutabaki salama. Swali linalofuatia ni je, lengo la ccm ni kuizuia Tanganyika ili zanzibar hatimaye ivunje kabisa muungano kisha sisi watanganyik tuishie kushuhudia ndugu na majirani zetu wakimalizana sababu tu sisi tutakuwa salama kama Tanganyika? Sidhani kama hii ndio njia ambayo CCM ndio inapendelea Tanganyika irudi, kama itarudi. Tukifika huko, ccm ijue tu ingeweza epusha maafa yote.

Wananchi wenzangu, TANGANYIKA ndio ASILI YAKO, Usidanganyike na muungano wa Kisiasa fraught with Legal Manipulation and Political Expediency. Tukiendelea kuendekeza haya, ni hatua ya kutojali well being ya vizazi vyetu vijavyo.
Nguruvi3, tunaomba somo lako kuhusu hoja ya Waziri Mku Pinda na Tanganyika.

Itaendelea kwa utaratibu ulioanishwa bandiko #1 .

TANZANIA KWANZA, TANGANYIKA KABLA.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,
Kwa kweli unaandika mambo muhimu sana kwa wa TGk wajue wapi walipotoka , walipo na nini mwelekeo wao.

Nakumbuka hata Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema katika moja ya hotba zake akanena Wazanaki wanasema “ UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA” akiwa na maana ya MFICHAFICHA MARADHI KILIO KITAMFICHUA.

Hongera sana.

Lakin nina wasi wasi na somo la Nguruvi3, kwani ahali yangu huyu anafahamu mengi sana lakin TATIZO LAKE ANA JAZBA NA USHABIKI. na hivi mara nyingi vinampelekea kuandika kama analalamika na kunung'unika na sio kuwasilisha na mara nyingi kuondoa busara na hikma katika maandiko yake.

Labda nimnasihi apunguze Jazba kama mkurya aliyekula KICHURI na kuondoa ushabiki. Weka bayana na sote tupo pamoja nawe.

Akhsantum
 
UTAMBULISHO WA ZNZ
Pinda anataka znz ipate utambulisho. Akiwa mwanasheria kitaaluma ameshindwa kutambua mkataba wa muungano ulikuwa baina ya nchi ngapi na nini kilitokea akiwa ofisi ya rais kwa matukio tuliyoyaorodhesha hapo juu.

Katiba ya 2010 ambayo iliiyoondoa znz katika JMT kimantiki imeipa znz uwezo wa kutambulika kama nchi kwa jina, bendera, wimbo wa taifa, Rais, BLW, vikosi vya ulinzi na usalama.
Hayo yametokea machoni mwa Pinda akiwa waziri mkuu, mshauri mkuu wa pili wa Rais wa JMT.

Pinda hakumbuki yeye kama waziri mkuu hana uwezo wa kuzungumza na masheha katika shehia yoyote kule znz kwa capacity ya waziri mkuu.

Uwaziri mkuu wake unaishia bara kwasababu ZNZ ina uongozi kamili na yeye hana lake hata kwa bahati mbaya. Ni kutokana na hilo hana utambulisho znz na ni kitu cha ajabu anapodai znz ipewe utambulisho.

Znz inao utambulisho,kilichokosekana ni mshirika wa znz katika JMT ambaye ni Tanganyika.
Katika mazingira ya kwaida Pinda alipaswa kulia kuliko kuitafutia znz utambulisho.

Angeangua kilio kwasababu ile nchi aliyozaliwa Tanganyika imetoweka katika mazingira tatanishi.
Pinda hana kumbu kumbu za uwepo wa Tanganyika kama alivyosema.

Katika hali isiyo ya kawaida, mapendekezo ya Pinda kule Dodoma kama waziri mkuu lazima yaende baraza la wawakilishi znz kupewa baraka zote.

Endapo Pinda anapendekeza ujenzi wa vyoo vya shule basi kama waziri mkuu lazima apate ridhaa ya BLW znz kama ilivyo katika katiba ya znz iliyofanyiwa marekebisho 2010.

Ni kwa muktadha huo, Pinda anaitambua znz zaidi kuliko sisi wa mitaani kwasababu hawezi kutekeleza majukumu yake hadi pale Pandu Kificho na wenzake 50 wanaoitwa BLW watakapokubali.

Kinachomsumbua mzee Kayanza ni usahaulifu wa historia pengine kutokana na majukumu mengi ya kazi au tatizo la kibinadamu la kumbu kumbu hafifu.

WATANGAYIKA KUNYIMWA ARDHI
Hili Pinda analiona dogo sana lakini kwa wananchi wa nchi moja ni kubwa.
Nguvu ya soko huamuliwa na soko lenyewe.

Itakuwa ni kituko mtu kwenda kununua ardhi ya sh milioni 50 kwa ekari moja kuliko kununua mashamba Tanganyika.Hata hivyo katika misingi ya utaifa znz haipaswi kuweka vikwazo hivyo.

Hii maana yake ipo siku Kilimanjaro nao watasema hivyo na Pinda takubaliana nao.
Sheria ya ardhi iimemlenga Mtanganyika kwasababu Mkenya na mtaliano au Mwarabu hawaguswi na sheria hiyo.Ni ubaguzi huu ndio unapelekea Watanganyika kujiuliza kama sisi ni taifa.

Ubaguzi wa ardhi ni sehemu tu ya ubaguzi unaoendelea visiwani ukiwalenga Watanganyika na si raia wa eneo lingine.

Katika nchi moja znz haitambui leseni ya Tanzania bara,na kazi ni kwa kibali achilia mbali ukazi.
Kama waziri mkuu Pinda alipaswa kuliangalia hili tatizo kwa upana wake zaidi hasa katika ubaguzi na wala si kwa mtazamo hafifu finyu na potofu alioutoa.

Nguruvi3,

Punguza jazba ahali yangu na nitakupa darsa hapa.

Ilipounganishwa Znz na TGK na kuunda Tz uongozi wa juu ulikuwa kama ifuatavyo. Kulikuwa na Rais wa JMTz ambaye alikuwa Nyerere, Vile vile kulikuwa na Rais wa Znz na makamo wa kwanza wa Rais wa JMTz na,naye alikuwa Mz Karume . Na Upande wa TGK kulikuwa na Waziri Mkuu na makamo wa Pili wa Rais wa Jmtz, cheo hicho hata Mz Kawawa na hata Mz Malecela aliwahi kuwa Waziri mkuu na makamo wa kwanza wa rais wakti Mwinyi alipokuwa Rais wa JMTz.

Kifupi uongozi ulikuwa unasema hivi. Kama Rais akitoka Upande mmoja wa Muungano, Basi makamo wa kwanza atatoka upande wa pili wa muungano, na makamo wa pili atatoka upande aliotoka Rais.

Hivyo toka enzi Hizo mamlaka ya waziri mkuu wa TGK yalikuwa mwisho Chumbe kama ilivyo sasa. Hivyo hayo sio kuwa yamebadilishwa katika KATIBA YA ZNZ YA 2010 Bali yalikuwepo toka zamani.


Kilichofanywa na Katiba ya Znz ya 2010 ni kuonyesha kuwa Znz ni nchi kamili na kubainisha mipaka yake na utaratibu wake wa uongozi na mipaka ya viongozi hao.

Pole sana.
 
Barubaru,

Nadhani hoja ya msingi ya Nguruvi3 ni kwamba - Waziri Mkuu anajulikana kikatiba kama waziri mkuu wa jamhuri ya muungano, lakini in practice hana mamlaka yoyote kwenye upande wa pili wa muungano, hivyo hana moral authority ya kutetea jambo ambalo hana mamlaka nayo.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
TUACHE UPOTOSHAJI KUHUSU ZANZIBAR KUTOKUWA NA UWEZO WA KUJIENDESHA NA KUGHARAMIA MUUNGANO

Wakati tukiendelea na mjadala wetu, nimeonelewa niweke sawa suala tajwa hapo juu kwani
Hoja juu ya uwezo wa zanzibar kujitegemea ni hoja iliyojaa mantiki za kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Hoja hii imejaa upotoshaji kuliko ukweli, upotoshaji unaoongozwa na kina Gamba la Nyoka na wenzao kwa nia ya kuwatisha wazanzibari wasiendeleze harakati zao za kurudi katika mkataba wa muungano wa 1964 ambao uliweka wazi mazingira ya serikali tatu - machache ya kuchangia kwa pamoja kishirikisho, na yaliyobakia kila nchi shiriki kuyasimamia kivyake. Huko nyuma tulijadili suala hili, lakini kama anavyosema Nguruvi3, kina Gamba la Nyoka na wenzake wana utamaduni wa kukimbia hoja, kisha baada ya majumaa au miezi kadhaa, wanarudi humu kurudia hoja zile zile dhaifu.

Kabla ya Mwaka 1964 (mwaka wa muungano), zanzibar ilikuwa ni taifa huru kiuchumi na kisiasa. Lilijiendeshea mambo yake yenyewe, and in actual sense, zanzibar huko nyuma ilikuwa ni moja ya economic power houses barani Africa, ikiwa katika ligi moja na nchi kama Ghana na Misri in terms of economic performance and activities. Hata Tanganyika haikuwa inafua dafu kiuchumi mbele ya Zanzibar, sasa kwanini leo tuseme zanzibar haitakuwa na uwezo wa kujiendesha? Huku ni kuitusi zanzibar kwani wananchi walipomwaga damu kupigania mapinduzi yao, hawakufanya hivyo ili waje baadae kuwa tegemezi kwa Tanganyika.

Ni baada ya muungano tunaona zanzibar ikianza kubadilika kiuchumi. Hii ilitokana na muungano kuwa na sura ya kisiasa zaidi ambapo uchumi ukafanywa mtumishi wa siasa za muungano. katika hali hiyo, masuala ya uchumi yakawa treated kama masuala ya muungano ambayo yakapangwa to be shared equally na pande zote mbili za muungano. Hadi hapo zanzibar ikawa na uchumi imara tu ambao ungeweza kujiendesha na pia kuchangia gharama za mambo (11) ya muungano.

Kilichofuatia baadae katika historia ni kuona znz ikichangia mara tatu tu katika gharama za kuendesha muungano - 1964/5, 1965/6, 1966/7, na kila mwaka kiasi kikizidi kupungua. Sasa wapo wana ccm hapa wanaokebehi zanzibar juu ya suala hili lakini wanasahau kwamba muda mfupi baada ya muungano, zanzibar ikapewa kilema cha uchumi na Tanganyika (iliyovaa koti la muungano) kupitia sheria namba (9) ya tarehe 1/5/1964. Sheria hii ilitoka kama amri na haikushirikisha viongozi wa zanzibar bali wa Tanganyika kwa kutumia mamlaka iliyopewa Tanganyika ya kipindi cha mpito. Sheria hiyo ni kama ifuatavyo:

TANGAZO LA SERIKALI Na. 246 lililochapwa 1/5/1966.

SHERIA ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, 1964.

AMRI

Kwa mujibu wa vifungu 3(b) na 8 Vya Sheria Zilizotajwa

AMRI YA UTARATIBU WA KIPINDI CHA MPITO, 1964.

1. Amri hii itajulikana kama amri ya utaratibu wa kipindi cha mpito 1964, na itaanza kutumika siku ya muungano.

2. Amri hii itasomwa kama sehemu ya katiba ya muda.
....
....
....

9. Mali na Mikataba:
Mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya Tanganyika na mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya watu wa zanziba zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au zilizomilikiwa au kutumiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano chini ya jamhuri ya muungano.

Kimsingi, kupitia sheria hii, assets zote za zanzibar pamoja na savings zake kubwa sana kwenye benki moja huko uingereza, zikahamishiwa kwenye himaya ya muungano. Zanzibar ikabaki kapa in a blink of an eye. Na sheria hii inasema kwamba itaanza kutumika siku ya muungano wakati mkataba ukiwa umeshasainiwa. Huu ulikuwa ni uchakachuaji mkubwa ulioipa zanziba kilema cha uchumi hadi leo. Lakini wanaoponda uchumi duni wa Zanzibar huko CCM hawajui haya pengine.

Zanzibar ndio ilikuwa kwanza imetoka katika mapinduzi, na haikuwa hata haija thaminisha mali zake na akiba yake kubwa kwenye benki huko London (Narodny Bank). Akiba ya Zanzibar by the time Karume anafariki 1972 ilikuwa about 25 Million Pounds Za mwingereza. Fedha hizi zilichangiwa na bei nzuri ya karafuu soko la dunia ambapo ilirurka kutoka $550 kwa tani miaka ya mwanzo ya mapinduzi na kufikia $1,500 kwa tani 1967-8; Karume alitumia fedha nyingi kujengea wananchi makazi, miundo mbinu kwa mafanikio makubwa;

Fedha na mali zote hizi zikachukuliwa na Tanganyika iliyovaa koti la muungano. Lipo suala lingine la kifedha ambapo Zanzibar Bank ambayo ilitakiwa iwe ni benki kuu ya zanzibar, nayo ikavurugwa na sheria za muungano.

Licha ya yote haya, leo zanzibar bado wana uwezo wa kusimama kiuchumi kwa mafanikio tu kwani uchumi unategemea natural resources, human capital, leadership na political will among others. Zanzibar wana rasilimali nyingi tu - wana mafuta, gesi, utalii, uvuvi, a free port, kutaja vichache tu. Lakini yote haya yamevurugwa na muungano wa kisiasa. Kwa mfano, Katiba ya muungano (1977) haisemi hadi leo zanzibar watanufaika vipi na rasilimali zake, na wala haizungumzi economic justice za wazanzibari. Uchumi na rasilimali zinatajwa kijuu juu tu na kisiasa.

Iwapo zanzibar watapewa fiscal and economic autonomy, hakuna shaka kwamba wataweza kuamka kiuchumi pengine kuliko hata Tanganyika. Sisi Tanganyika hatuna nia ya kujenga uchumi wa wananchi, je Zanzibar wakiamua to build a strong domestic economy kwa manufaa ya wananchi, kwanini wasifanikiwe? Haitachukua zaidi ya miaka 15, tutabaki midomo wazi. Lakini ni iwapo wataamua leo na wataendelea na juhudi zao zilizoanza na katiba yao ya 2010.

Kuna many wealthy small islands in the world ambazo zilikuwa na changamoto kama tu zanzibar kwa maana ya idadi ndogo ya watu na eneo dogo la ardhi, lakini kwa vile they had political will, leo sio tu wapo huru kiuchumi, bali pia wapo mbele sana ya nchi kubwa na zenye rasilimali zaidi yao.

Zanzibar ina urefu wa kilometa 1,500 na upana wa kilometa 30, huku idadi yake ya watu ikiwa ni karibia 1.4 million. Tufananishe na nchi jirani yake ya Mauritius:

Mauritius ukubwa wake haufikii zanzibar, ni kama robo mbili tu ya zanzibar - ina urefu wa Kilometa 45 na upana wa kilometa 65. Lakini bado it performs better sio tu zaidi ya Zanzibar bali Tanzania kwa ujumla. Most major economic and commercial indicators zinadhihirisha ukweli huu. Kwa mfao, kwa mujibu wa World Economic Forum's Travel and Tourism Competitiveness Index ya hivi karibuni juu ya Middle East and Africa, Mauritius wapo ranked top FIVE, wakati Tanzania ipo ranked 19th. Tanzania hii hii yenye wanasiasa wanaobeza potentials za nchi ndogo wakati chini ya utawala wao, "ukubwa wa pua haujawahi kuwa wingi wa makamasi". Vile vile, kwenye Global Index, Mauritius is 40th, Bwana mkubwa Tanzania is 98th.

Tukumbuke kwamba tofauti na Tanzania yenye kila aina ya vivutio vya kitalii - mbuga za wanyama, mlima wenye barafu south of equator, olduvai gorge alipopatikana binadamu wa kwanza,Mauritius hawana vivutio vya maana kama hivi lakini bado wanapokea watalii wengi kuliko Tanzania kwa zaidi ya asilimia ishirini. Kwa mfano, Takwimu za World Tourism Organization zinaonyesha Tanzania hupokea watalii 700,000, na Mauritius watalii 900,000.

Pia katika "Doing Business Report", inayoangalia ease of doing business/ubora wa mazingira ya kufanya biashara, Mauritius is 17th in the world, sisi Tanzania na ukubwa wetu wa pua, we are 131st.

Mauritious ina GDP ambayo ni nusu tu ya Tanzania (kama USD 12 Billion, compared na ya Tanzania inayovuka USD 25 Billion sasa), lakini bado wananchi wa mauritious wana maisha bora kwa mbali sana ikilinganishwa na Watanzania. Wananchi wa mauritious ni miongoni mwa wananchi wenye hali bora za maisha sio afrika tu bali katika nchi zinazoendelea. Isitoshe, na udogo wao, hawapo tena katika low income countries bali middle income. Tanzania na ukubwa wetu wa pua, hii bado ni ndoto licha ya matumaini mengi wanayotoa wanasiasa kwa wananchi.

Tusiwatishe wazanzibari, bali tuwape moyoo kuelekea autonomy and self determination kwani hivyo ndivyo na Tanganyika itapatikana na kupelekea uwepo wa muungano unaoendeshwa kwa ushindani and with less waste of resources tofauti na mfumo mbovu wa ccm na serikali zake mbili zisizo na tija.

Wazanzibari should be inspired by the likes of Mauritious, tusiwakatishe tamaa, tusiwatishe. Isitoshe, wakiamua kufungua kesi ya madai ya uchakachuaji wa mali na akiba zake nilizojadili, ndani ya serikali ya ccm hapatatosha.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Barubaru,

Nadhani hoja ya msingi ya Nguruvi3 ni kwamba - Waziri Mkuu anajulikana kikatiba kama waziri mkuu wa jamhuri ya muungano, lakini in practice hana mamlaka yoyote kwenye upande wa pili wa muungano, hivyo hana moral authority ya kutetea jambo ambalo hana mamlaka nayo.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,

Unajuwa lengo kuu la JF ni KUILIMISHANA na KUPEANA Habari na hata Kuburudishana. Hivyo kumbuka unapoandika humu unatakiwa kujua kuna watu wanafyonza ilmu hususan katika darsa hizi za Muungano kwani Serikali zote mbili JMTz na SMZ wanajitahidi kwa gharama kubwa kuficha ukweli na uhalisi wa historia ya muungano wenu.

Upotoshaji wowote katika darsa hizi unatakiwa ujue kuwa utawaathiri wengi sana ndio maana tunapoona kuna upungufu au kuteleza basi tunasawazisha.

Nilikuwa IN'DHALI hapo awali kuwa ahali yangu ana MUNKAR, CHUKI NA USHABIKI na hivyo mara zote anaandika kwa lugha ya kulalamika na kunung'unika na mara zote zinamtoa katika uhalisia wa kile anachoandika.

Unapogusa Muungano lazima uwe mkweli na ubainishe mfumo wake. Unapomgusa PM wa JMTz lazima ujue kuwa ana mwenzake upande wa pili wa muungano ambaye ni Rais wa Znz na SMZ ambazo zinafanya kazi huko Znz.

Lazima ubainishe kuwa katika Muungano wenu kuna mambo mmekubaliana Kushirikiana na mengine yao nje ya Muungano ambapo kila nchi inajitegemea kwayo. LAKIN PIA ULITAKIWA KUELEZA KUWA TGK IMEJIVIKA JOHO LA MUUNGANO NA kuiingiza Serikali yake kama JMTz.

Sasa LAZIMA IJULIKANE SIO KILE MWENYE MAMLAKA KATIKA JMTz BASI MAMLAKA YAKE YANAWEZA KUTUMIKA MPAKA ZNZ. Sio tu waziri mkuu lakin hata waziri wa Maji, Nishati, Ardhwi, afya, Ilmu na wengineo mamlaka yao mwisho Chumbe, Znz hawatambuliki kama ilivyo kwa wenye mamlaka kama hayo upande wa Znz hawatambuliki huko TGK.

Nilitaka tu kuweka sawa kwa wale wasiojuwa hayo kwani mwongozo huu ni mzuri sana katika mjadala huu wa muungano na mastakabali wa wananchi washirika wa muungano wenu.

Nashukuru sana na samahani kama nitakuwa nimepindisha mjadala LAKIN NIA YANGU ILIKUWA KUWEKA SAWA MAMBO KWA FAIDI YA WENGI WASIOJUA HAYO.

Ahsantum na ijumaa njema.

 
TUJADILI UKWELI KUHUSU MWALIMU NYERERE NA MFUMO WA SERIKALI MBILI

Kuna upotoshaji ambao umekuwa unafanywa na baadhi ya wana ccm ambapo wamekuwa wanamtumia Baba wa Taifa vibaya kuhusiana na suala zima la kutetea mfumo wa serikali mbili, huku wakiwashutumu wale wote wanaojenga hoja juu ya umuhimu wa serikali tatu, kwamba hawa ni wasaliti ndani ya chama. Kwa maana hii, watu kama Kina Jaji Warioba, Salim, Butiku, wanaonekana kama vile ni wasaliti wa mwalimu. Mkakati huu umezidi kuwachanganya wananchi hasa ikizingatiwa kwamba kundi hili (Wariona, Salim, Butiku) ni kundi ambalo lilikuwa na ukaribu na mwalimu kuliko kundi lingine lolote ndani na nje ya chama. Hata wakati ule (awamu ya pili) makada wengi wa ccm walipokuwa wanampinga Mwalimu katika masuala mbalimbali kama vile uadilifu wa viongozi, azimio la arusha, umuhimu wa kuheshimu katiba, makada wengi wa ccm ambao leo ndio wanaonekana ni wazalendo wa taifa hili (sitataja majina), wakati ule hawakuwa upande wa Mwalimu kihoja. Katika hali hiyo, kina Salim, Warioba, Butiku, hawa hawakuwahi kuyumba wala yumbishwa na makada wa wakati ule ambao wengi waliwageuza wazee wetu hawa kuwa maadui wa kisiasa. Cha kustaajabisha, leo makada hawa wanatumia jina la Mwalimu kupingana na maoni ya wananchi kupitia rasimu ya katiba, huku wakimweka mwalimu upande wao.

Kina Warioba sio majuha kuunga mkono hoja ya serikali tatu. Mbali ya sababu ambazo tayari zipo wazi kama vile kuvunjika kwa muungano ambao Mwalimu na Karume waliuacha, nimeona kuna haja ya kuja kuweka rekodi sawa juu ya mtazamo wa Mwalimu. Vinginevyo muungano alioacha Mwalimu na Karume ulishavunjika hata kabla tume ya katiba chini ya Jaji Warioba ilikuwa haijateuliwa. Warioba na makamishna wenzake waliteuliwa katika tume wakati Tanzania tayari ni nchi mbili zenye serikali mbili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar (2010). Badala ya makada wa ccm kuelezea umma hili limetokeaje na nini ni athari zake kwa muungano, makada hawa wanahamishia hisia zao na hoja zao za ovyo ovyo kwa tume ya warioba badala ya kuhojiana wenyewe ndani ya chama. Sisi tunao amini katika Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla, tutaelimisha umma kwa kuweka historia sawa.

Kwanini Mwalimu aliamua baadae mfumo sahihi ni serikali mbili?

Mwalimu alifanya hivyo kwa sababu kuu mbili.

1. Kwanza ni kwamba mara baada tu ya muungano, Rais Karume hakuwa na mwelekeo wa kuheshimu mkataba wa muungano kwani alichokuwa anakihitaji - uhakika wa ulinzi kutoka Tanganyika, alishakipata. Kwa mfano, Issa Shvji katika kitabu chake cha "Let the People Speak: Tanzania Down the Road to Neoliberalism (2006, pp 90) anasema hivi:

Karume, however had no time for legal arrangements. He continued to exercise power in complete disregard on union matters. Karume declared that they would not be elections in Zanzibar for the next 50 Years. Nyerere was exasperated but he could do little without pushing Karume out of the union. Meanwhile, his legal craftsmen amended the constitution to postpone the constitutional commission and the constituent assembly indefinitely. The union was governed by the interim constitution of 1965 for the next 12 years.

Character ya Karume ilichangia sana kwa Nyerere kubadili mawazo juu ya lengo lake la shirikisho, hivyo nchi kuwa na katiba ya muda kama anavyojadili shivji. Karume hakuwa na muda kuheshimu makubaliano ya Mkataba wa muungano from the get go, hivyo shirikisho lingekumbwa na matatizo ingawa it was the most proper arrangement kisheria na kidemokrasia. Na kwa vile mfumo wa chama kimoja ulikuwepo, mfumo wa serikali mbili haukuwa na matatizo makubwa. Lakini tatizo likaanza kujitokeza pale siasa za vyama (TANU) zilipoanza kuingilia hata masuala yasiyo ya muungano. Tutajadili hili baadae ikiwa ni pamoja na sakata la Jumbe ambapo kimsingi he was challenging the supremacy of the party katika muungano.

Lakini sababu nyingine equally important ya Nyerere kupingana na serikali moja ni kwamba pamoja na udogo wake kama taifa, bado zanzibar ilikuwa na hadhi sawa kama Tanganyika kwa maana ya "a sovereign state", hivyo kuimeza kwa muungano wa serikali moja ni suala ambalo baadae lingekuja leta matatizo. Ingawa Karume alimwambia Mwalimu kwamba hata serikali moja kwake ingekuwa sawa, Mwalimu hakuona busara kufanya hivyo. Na baadae busara hizi zikawa dhahiri kwa kutazama hoja ya shivji hapo juu.

Nini kilimfanya Mwalimu aamue kikatiba mwaka 1977 kwamba muundo wa muungano uwe ni wa serikali mbili?

Kama tulivyokwisha jadili hapa na pia awali, Mwalimu alikuwa na ndoto ya "federation system", sio "unitary system, tofauti na wengi wanavyojadili. Ni katika hili la unitary system Nyerere alipingana na Kwame Nkrumah katika vision yao ya Panafricanism. Mwanzoni Kwame alionekana na busara zaidi ya Mwalimu lakini haikuchukua muda mrefu, Mwalimu akaonekana kwamba alikuwa sahihi zaidi ya Nkrumah. Lakini swali la msingi linabakia, kwanini serikali mbili kikatiba (1977)?

Jibu ni kwamba kazi aliyoanzisha na wenzake kina Nkrumah ilikuwa kwanza ni kupigania uhuru wa Afrika, na baadae umoja wa Afrika. Katika hali hii, muungano wowote ulilazimika kuheshimu "uhuru" wa washirika kabla ya kuanza kuhubiri "umoja"

Katika kitabu chake Mwalimu anasema hivi:

Hatukutaka tudhaniwe hata kwa makosa kwamba tulianzisha ubeberu mpya, kwahiyo mimi nilipanga mfumo wa serikali mbili.

Ni vizui kuelezea shabaha ilikuwa kuziunganisha nchi za Afrika mashariki ziwe nchi moja; wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katika mazungumzo ya kutafuta uwezekano wa kuungana.

Kama jambo hilo lingetokea, mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa shirikisho, ama shiikisho la nchi tatu zenye serikali nne, au shirikisho la nchi nne zenye serikali tano.

Hapa tunaona kwamba mwalimu hakuwa na tatizo la serikali kuwa zaidi ya moja, mbili, tatu kwani hivyo ndivyo shirikisho linatakiwa liwe. Hata leo, sisi wapiganaji wa Tanganyika hatupingi "nchi moja" bali tunapinga "nchi mbili, serikali mbili", lakini muhimu zaidi, tunapinga nchi moja, serikali mbili kwani hilo haliwezekani pia kwa hoja tulizojadili hapa and elsewhere.

Nikiendelea kumnukuu Mwalimu, anasema:

Nani anaweza kusema katika mazingira ya sasa kunaweza kuundwa afrika moja? Kama hakuna, hofu ya kuundwa serikali ya Tanganyika ipo wapi?

Kama jambo hilo lingetokea, mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa shirikisho, ama shirikisho la nchi tatu zenye serikali nne, au shirikisho la nchi nne zenye serikali tano.

Inaendelea bandiko linalofuata

Cc Nguruvi3, Gamba la Nyoka, Barubaru, Mag3, Mtanganyika, Nape Nnauye, JokaKuu, Ritz, MwanaDiwani, zomba, Pasco, EMT, ZeMarcopolo, Mzee Mwanakijiji.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom