Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #21
Inaendelea kutoka bandiko #20 .
Tatizo ni kwamba makada wanaomtumia Mwalimu kama kina Nape Nnauye na wenzao, pia wale wanaomshauri Rais Kikwete, wanafanya hivyo huku wakiwa wavivu wa kumsoma Mwalimu.
Muungano wetu haukutokana na msaafu au biblia, na Mwalimu kadhihirisha hilo. Muungano ni wa wananchi, kama wanataka kuubadili, ni wao ndio watakaoulinda kwa gharama. Wananchi hataulinda muungano watakaoundiwa na CCM. Haitatokea. Sana sana utalindwa na vifaru na Mabomu, lakini tatizo ni kwamba mabomu na vifaru vitatokana na kodi ya wananchi hawa hawa. Kwahiyo mafanikio ya CCM katika ulinzi huo yatakuwa ni ya muda tu.
Lipo suala lingine muhimu, nalo ni la Hoja ya mwalimu dhidi ya serikali tatu enzi za sakata la G55. Kama tunavyojua na kama tutakavyojadili, hoja ya Tanganyika ilikuwa na uzito uliostahili kiasi cha kupewa baraka zote za chama na serikali hivyo kuwasilishwa bungeni mwaka 1994. Hata mwenyekiti wa sasa wa BLK, Samuel Sitta alikuwa ni sehemu ya wabunge hao 55, huku pia akiwa ni waziri wa Katiba na Sheria. Ndani ya wiki tatu, Bill Husika ilipitia versions tatu tofauti, huku ile ya mwisho ikielekeza suala hili sasa lipatiwe ufumbuzi kupitia kura ya maoni kwani wananchi ndio wenye uamuzi wa mwisho. Waziri wa sheria na katiba, Samuel Sitta akaahidi kufanyia kazi mchakato huo. Hata Hansard za bunge juu ya suala hili zipo. Isingekuwa Mwalimu kuingilia, Tanganyika ingerudi.
Kwanini Nyerere aliingilia?
Kufikia 1994, Mwalimu alishaona jinsi gani mfumo wa serikali mbili haufanyi kazi, hasa chini ya mfumo wa vyama vingi na ndio maana alimpa kazi jaji Bomani kuja na solution ili kuepuka mgogoro ambao ungekuja baadae kidogo (1995) ambapo CCM ingeshinda Bara na CUF Zanzibar. Hali hii ingevunja muungano kwani siasa za CUF zilikuwa ni za kupinga mfumo uliopo chini ya CCM. Jaji bomani akaja na solution ya kuiga mfumo wa shirikisho la marekani la kumfanya makamu wa rais kuwa mgombea mwenza, na kumtoa rais wa znz asiwe tena makamo wa rais. Vinginevyo mwalimu hakuingilia suala la G55 kwa ajili ya kulinda chama, chama ambacho kilishaamua kukana misingi yake, kuua azimio la arusha 1992 kle zanziba kwa kuanzia, kimya kimya bila ya kumshirikisha mwalimu. Mwalimu aliingilia suala la G55 ili kuokoa muungano, lakini muhimu zaidi, kuokoa taifa lisichafuke na migogoro ya kidini, lakini pia, kulinda heshima ya katiba ya JMT ambayo iliweka wazi kwamba taifa letu ni secula state (lisilofuata itikadi ya dini yoyote).
Kitendo cha zanzibar kujiunga na OIC ilikuwa ni kinyume cha katiba, lakini muhimu pia, hoja ya Tanganyika ilitawaliwa sana na malumbano ya kidini. Hapo ndipo Mwalimu akaingilia, na ninanukuu baadhi ya maneno yake katika consultative meeting wakati ule:
Ni pale hoja ya Tanganyika ilipozidi kushika kasi ndani ya CCM (wabunge) ndio mwalimu akajenga hoja kwamba hata hiyo hoja wanayoimamia, hoja hiyo haikuwa ni sera ya ccm, kwahiyo njia bora kwa wahusika ni kwenda kuipigania nje ya CCM. Lakini hii haina maana kwamba Mwalimu alikuwa anatetea serikali mbili kwasababu tu hii ni sera ya CCM, na wala hakuwa na nia ya kuzuia CCM isipasuke kwa kiasi kikubwa kuliko kuzuia muungano usivunjike kwa hoja za kidini ambazo zingeangamiza taifa.
Mwisho, mwalimu alisema hivi, na maneno haya yanarudiwa sana kwenye ITV na pia yapo youtube:
Swali linalofuatia ni je, kwa kiasi gani hoja za Mwalimu wakati ule zipo relevant katika sakata la leo ambapo hoja ya Tanganyika imetokana na maoni ya wananchi wengi wa pande zote mbili za muungano kwa mujibu rasimu ya katiba?
Itaendelea kwa jinsi bandiko #1 lilivyoainisha.
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.

Na katika hali ya mazungumzo tuliyonayo, hapa tunayoyazungumza haya, wakubwa wanatuita tuje tuanze maelewano ya kupunguza chuki. Wanajua wakubwa kwaba hali tuliyonayo ni ya chuki. Tumechoka na wazanzibari, tumechoka na wazanzibari. Hayo ndio mazungumzo. Mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na msukumo huu unaowasukumeni wa chuki wa zanzibari na uislamu, nasema mbele yenu na nasema mbele ya mungu, kuna msukumo 'tumechoka na wazanzibari' lakini ndani yake humo humo umo udini. Tumechoka na wazanzibari na ndani ya humo humo umo udini. Nimewatest watu mimi, umo udini mkubwa ndani. Kwasababu wewe ndugu rais, wewe muislam, wewe mzanzibari, umefanya madhambi. Basi rais, mzanzibari, muislam amefanya makosa,, mzanzibari, muislamu amefanya makosa. Kwahiyo kuna msukumo, msukumo huu wa uzanzibari na uislamu unaosukuma jambo hili. Kwahiyo nasema nini mimi? Nasema mkijenga, mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na misingi hiyo ya kuchoka na wazanzibari - na chini chini mmechoka na uislamu. Sababu hizo mbili, hizo hizo zitakazoua muungano. Mkiunda serikali ya Tanganyika kwa msukumo huu, muungano utakufa, na muungano ukifa kwa ukabila (maana uzanzibari ni ukabila tu) na udini, sababu hizi mbili za ukabila na udini zitakazoua muungano, zitaua Tanganyika.
Ni pale hoja ya Tanganyika ilipozidi kushika kasi ndani ya CCM (wabunge) ndio mwalimu akajenga hoja kwamba hata hiyo hoja wanayoimamia, hoja hiyo haikuwa ni sera ya ccm, kwahiyo njia bora kwa wahusika ni kwenda kuipigania nje ya CCM. Lakini hii haina maana kwamba Mwalimu alikuwa anatetea serikali mbili kwasababu tu hii ni sera ya CCM, na wala hakuwa na nia ya kuzuia CCM isipasuke kwa kiasi kikubwa kuliko kuzuia muungano usivunjike kwa hoja za kidini ambazo zingeangamiza taifa.
Mwisho, mwalimu alisema hivi, na maneno haya yanarudiwa sana kwenye ITV na pia yapo youtube:
Iwapo watanganyika watauvunja muungano kwa hoja kwamba sisi watanganyika, na wao wazanzibari, watanganyika hawatabaki salama. Na iwapo wazanzibari watauvunja muungano kwa hoja za 'wao ni watanganyika, na sisi ni wazanzibari, Watanganyika watabaki Salama
Swali linalofuatia ni je, kwa kiasi gani hoja za Mwalimu wakati ule zipo relevant katika sakata la leo ambapo hoja ya Tanganyika imetokana na maoni ya wananchi wengi wa pande zote mbili za muungano kwa mujibu rasimu ya katiba?
Itaendelea kwa jinsi bandiko #1 lilivyoainisha.
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
Last edited by a moderator: