Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Inaendelea kutoka bandiko #20 .


Tatizo ni kwamba makada wanaomtumia Mwalimu kama kina Nape Nnauye na wenzao, pia wale wanaomshauri Rais Kikwete, wanafanya hivyo huku wakiwa wavivu wa kumsoma Mwalimu.

Muungano wetu haukutokana na msaafu au biblia, na Mwalimu kadhihirisha hilo. Muungano ni wa wananchi, kama wanataka kuubadili, ni wao ndio watakaoulinda kwa gharama. Wananchi hataulinda muungano watakaoundiwa na CCM. Haitatokea. Sana sana utalindwa na vifaru na Mabomu, lakini tatizo ni kwamba mabomu na vifaru vitatokana na kodi ya wananchi hawa hawa. Kwahiyo mafanikio ya CCM katika ulinzi huo yatakuwa ni ya muda tu.

Lipo suala lingine muhimu, nalo ni la Hoja ya mwalimu dhidi ya serikali tatu enzi za sakata la G55. Kama tunavyojua na kama tutakavyojadili, hoja ya Tanganyika ilikuwa na uzito uliostahili kiasi cha kupewa baraka zote za chama na serikali hivyo kuwasilishwa bungeni mwaka 1994. Hata mwenyekiti wa sasa wa BLK, Samuel Sitta alikuwa ni sehemu ya wabunge hao 55, huku pia akiwa ni waziri wa Katiba na Sheria. Ndani ya wiki tatu, Bill Husika ilipitia versions tatu tofauti, huku ile ya mwisho ikielekeza suala hili sasa lipatiwe ufumbuzi kupitia kura ya maoni kwani wananchi ndio wenye uamuzi wa mwisho. Waziri wa sheria na katiba, Samuel Sitta akaahidi kufanyia kazi mchakato huo. Hata Hansard za bunge juu ya suala hili zipo. Isingekuwa Mwalimu kuingilia, Tanganyika ingerudi.

Kwanini Nyerere aliingilia?

Kufikia 1994, Mwalimu alishaona jinsi gani mfumo wa serikali mbili haufanyi kazi, hasa chini ya mfumo wa vyama vingi na ndio maana alimpa kazi jaji Bomani kuja na solution ili kuepuka mgogoro ambao ungekuja baadae kidogo (1995) ambapo CCM ingeshinda Bara na CUF Zanzibar. Hali hii ingevunja muungano kwani siasa za CUF zilikuwa ni za kupinga mfumo uliopo chini ya CCM. Jaji bomani akaja na solution ya kuiga mfumo wa shirikisho la marekani la kumfanya makamu wa rais kuwa mgombea mwenza, na kumtoa rais wa znz asiwe tena makamo wa rais. Vinginevyo mwalimu hakuingilia suala la G55 kwa ajili ya kulinda chama, chama ambacho kilishaamua kukana misingi yake, kuua azimio la arusha 1992 kle zanziba kwa kuanzia, kimya kimya bila ya kumshirikisha mwalimu. Mwalimu aliingilia suala la G55 ili kuokoa muungano, lakini muhimu zaidi, kuokoa taifa lisichafuke na migogoro ya kidini, lakini pia, kulinda heshima ya katiba ya JMT ambayo iliweka wazi kwamba taifa letu ni secula state (lisilofuata itikadi ya dini yoyote).

Kitendo cha zanzibar kujiunga na OIC ilikuwa ni kinyume cha katiba, lakini muhimu pia, hoja ya Tanganyika ilitawaliwa sana na malumbano ya kidini. Hapo ndipo Mwalimu akaingilia, na ninanukuu baadhi ya maneno yake katika consultative meeting wakati ule:

Na katika hali ya mazungumzo tuliyonayo, hapa tunayoyazungumza haya, wakubwa wanatuita tuje tuanze maelewano ya kupunguza chuki. Wanajua wakubwa kwaba hali tuliyonayo ni ya chuki. Tumechoka na wazanzibari, tumechoka na wazanzibari. Hayo ndio mazungumzo. Mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na msukumo huu unaowasukumeni wa chuki wa zanzibari na uislamu, nasema mbele yenu na nasema mbele ya mungu, kuna msukumo 'tumechoka na wazanzibari' lakini ndani yake humo humo umo udini. Tumechoka na wazanzibari na ndani ya humo humo umo udini. Nimewatest watu mimi, umo udini mkubwa ndani. Kwasababu wewe ndugu rais, wewe muislam, wewe mzanzibari, umefanya madhambi. Basi rais, mzanzibari, muislam amefanya makosa,, mzanzibari, muislamu amefanya makosa. Kwahiyo kuna msukumo, msukumo huu wa uzanzibari na uislamu unaosukuma jambo hili. Kwahiyo nasema nini mimi? Nasema mkijenga, mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na misingi hiyo ya kuchoka na wazanzibari - na chini chini mmechoka na uislamu. Sababu hizo mbili, hizo hizo zitakazoua muungano. Mkiunda serikali ya Tanganyika kwa msukumo huu, muungano utakufa, na muungano ukifa kwa ukabila (maana uzanzibari ni ukabila tu) na udini, sababu hizi mbili za ukabila na udini zitakazoua muungano, zitaua Tanganyika.

Ni pale hoja ya Tanganyika ilipozidi kushika kasi ndani ya CCM (wabunge) ndio mwalimu akajenga hoja kwamba hata hiyo hoja wanayoimamia, hoja hiyo haikuwa ni sera ya ccm, kwahiyo njia bora kwa wahusika ni kwenda kuipigania nje ya CCM. Lakini hii haina maana kwamba Mwalimu alikuwa anatetea serikali mbili kwasababu tu hii ni sera ya CCM, na wala hakuwa na nia ya kuzuia CCM isipasuke kwa kiasi kikubwa kuliko kuzuia muungano usivunjike kwa hoja za kidini ambazo zingeangamiza taifa.

Mwisho, mwalimu alisema hivi, na maneno haya yanarudiwa sana kwenye ITV na pia yapo youtube:

Iwapo watanganyika watauvunja muungano kwa hoja kwamba sisi watanganyika, na wao wazanzibari, watanganyika hawatabaki salama. Na iwapo wazanzibari watauvunja muungano kwa hoja za 'wao ni watanganyika, na sisi ni wazanzibari, Watanganyika watabaki Salama

Swali linalofuatia ni je, kwa kiasi gani hoja za Mwalimu wakati ule zipo relevant katika sakata la leo ambapo hoja ya Tanganyika imetokana na maoni ya wananchi wengi wa pande zote mbili za muungano kwa mujibu rasimu ya katiba?

Itaendelea kwa jinsi bandiko #1 lilivyoainisha.


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimejikita kwenye gharama zaidi, na hapa naona mnaweka ngonjela tuu. Huu muungano ulishakosewa tangu mwanzo, hauna faida strategic au economical kwa watu wa bara. Hili ni katika myth za Mwalimu Nyerere na another political miscalculation kwa upande wake.

Mnaotaka serikali ya tatu naona mnataka kutupeleka vichakani tuu. Mimi nasema tuvunjeni. Wengi wetu bara hatuna faida nao zaidi ya kusikiliza manung'uniko kutoka Zanzibar. 3% ya nchi sio tatizo kuiacha iende. Watakuja na passport na tutakwenda na passport kwao. Sema kutuletea serikali nyingine hapa ili tuu kikidhi haja za wachache nadhani ni kutulaghai kama mlivyo tulaghai 1964
 
Mimi nimejikita kwenye gharama zaidi, na hapa naona mnaweka ngonjela tuu. Huu muungano ulishakosewa tangu mwanzo, hauna faida strategic au economical kwa watu wa bara. Hili ni katika myth za Mwalimu Nyerere na another political miscalculation kwa upande wake.

Mnaotaka serikali ya tatu naona mnataka kutupeleka vichakani tuu. Mimi nasema tuvunjeni. Wengi wetu bara hatuna faida nao zaidi ya kusikiliza manung'uniko kutoka Zanzibar. 3% ya nchi sio tatizo kuiacha iende. Watakuja na passport na tutakwenda na passport kwao. Sema kutuletea serikali nyingine hapa ili tuu kikidhi haja za wachache nadhani ni kutulaghai kama mlivyo tulaghai 1964

Mjadala wetu juu ya gharama tunaendelea nao kule kwenye uzi juu ya mtazamo wa hotuba ya JK katika BLK ulioanzishwa na Nguruvi3. Kuna hoja kule ambazo tunasubiri majibu kutoka kwako. Katika uzi huu, bado hatujafikia kwenye suala la gharama, tumeanza kwanza na asili ya Tanganyika kwa kuwekana sawa kihistoria.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimejikita kwenye gharama zaidi, na hapa naona mnaweka ngonjela tuu. Huu muungano ulishakosewa tangu mwanzo, hauna faida strategic au economical kwa watu wa bara. Hili ni katika myth za Mwalimu Nyerere na another political miscalculation kwa upande wake.

Mnaotaka serikali ya tatu naona mnataka kutupeleka vichakani tuu. Mimi nasema tuvunjeni. Wengi wetu bara hatuna faida nao zaidi ya kusikiliza manung'uniko kutoka Zanzibar. 3% ya nchi sio tatizo kuiacha iende. Watakuja na passport na tutakwenda na passport kwao. Sema kutuletea serikali nyingine hapa ili tuu kikidhi haja za wachache nadhani ni kutulaghai kama mlivyo tulaghai 1964
Twende kwenye uzi ule tuangalie gharama kinadharia na kiuhalisia kama alivyosema Mchambuzi.

Kama serikali 3 zenye mambo 7 ni mzigo, vipi serikali 2 zenye mambo 22 yasiyojulikana nani anayaebeba?
 
Last edited by a moderator:
Twende kwenye uzi ule tuangalie gharama kinadharia na kiuhalisia kama alivyosema Mchambuzi.

Kama serikali 3 zenye mambo 7 ni mzigo, vipi serikali 2 zenye mambo 22 yasiyojulikana nani anayaebeba?

Serikali mbili zenye:

1. Mambo ya muungano.
2. Mambo ya Tanzania bara.
3. Na mambo mchanganyiko wa muungano na Tanzania bara.

Na bado anasema eti mfumo wa sasa ni practical, serikali tatu shirikisho impractical. Hawa ndio pia wanaunga mkono maboresho ya mfumo yatakayowasilishwa na watu wao BLK kwamba tuongeze bunge la Tanzania bara kwa jina la baraza la wawakilishi la Tanzania bara, na kuleta mabunge matatu ndani ya nchi. Mtanganyika na wenzake sijui elimu yao walipata wapi ambapo wenzao tulifundishwa kwamba kuna mihimili mitatu ya dola:
1.Serikali.
2.Bunge.
3.Mahakama

Nia ikiwa ni check and order. Hili bunge la Tanzania bara, sera na sherria zake zitasimamiwa na serikali ipi? Serikali mbili mabunge matatu? Hawa watu ni vichaa au? Eti ili kulinda maslahi ya watanzania bara, siku ya mjadala wa masuala ya bara, wabunge wa zanzibar hawataruhusiwa kuingia. Kwanini Nguruvi3 asione hawa kama ni watalii kwa gharama za watanganyika, huku hayo ambayo watayapisha tujadili na wao wakienda kutalii, bado yasubiri baraka zao kupitia baraza la wawakilishi la znz?

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi na Nguruvi3, wakati mnaendelea kutoa shule, na mimi niongezee tu my two cents...naona wengi hawajui hata hilo jina Tanzania lilitokea wapi! Kwa tuliokuwepo, tunakumbuka harakati zilizofanyika kutafuta jina muafaka la Taifa jipya baada ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Zanzibar. Mapendekezo yalikuwa mengi yakitokana na kukokotoa majina Tanganyika na Zanzibar lakini ninayoweza kuyakumbuka sana yalikuwa manne; Zanzibat Tanganyika (Zantan), Tanganyika Zanzibar (Tangibar), Tanganyika/Zanzibar (Tanzan) na Tanganyika/Zanzibar (Tanbar). Jina ambalo lilionekana kukubalika haraka lilikuwa Tanzan na kwa kweli lilianza kutumika hata kabla ya kupitishwa rasmi. Hata hivyo wajuzi wengine walijitokeza na kupendekea kuwa neno tanzan haliendani na msamiati wa Kiswahili, hivyo liishie na vowel moja au mbili. Kulikua na (a) Tanzana, (b) Tanzani, (c) Tanzania na TANZANIA ikaibuka mshindi.

Ninachotaka kusisitiza ni kuwa Tanzania ilitokana na majina mawili; Tanganyika na Zanzibar, na hivyo Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikaja kujulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hoja yangu hapa ni kuwakumbusha wote kwamba unapoitaja Tanzania tayari unazitaja Tanganyika na Zanzibar, hakuna jina lililopotea!

Swali ni kwa nini ilitulazimu kufanya hivi? Kwa nini baada ya kuungana tukatafuta jina jipya badala ya kujiita tu Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Binafsi naamini hii ilikuwa ni kama transition tu kwa lengo la kuunda nchi moja yenye mamlaka moja. Kwa jinsi mambo yalivyo sasa, hii ndoto ni wazi imefutika na hasa baada ya kuanzishwa kwa nchi ya Zanzibar ndani ya Tanzania, na tukiacha siasa hata somo la hesabu hapa linagoma.

Sababu na uwezo labda bado zipo lakini nia halipo kabisa na kuamini hivyo ni kudanganyana, Muungano kwishnei!
Pinda anasema hajui Tanganyika.
Akina Mag3 wamekuja na namna majina yalivyo 'kokotolewa' au sijui kutoholewa.
Pinda na wapinga Tanganyika watasema hawajui nani alipedekeza majina hayo na watahitaji majina.

Mag3 anasema Tanganyika ipo ndani ya Tanzania. Kwahesabu set kubwa inaundwa na subset mbili Tanganyika na Zanzibar. Mwaka 2010 Zanzbar wakasema wanaondoka katika seti kubwa kwa katiba.
Leo wapo wanaotuaminisha kuwa ile set kubwa bado ina nchi mbili.

Mkuu Mkandara anasema Tanganyika ilikufa na kuwa Tanzania ambayo imeungana na Zanzibar.
Tanganyika haijafa, kule kwetu Bonde tunasema imechukuliwa msukule na mwanza wanasema ni matunge.

Msukule umeonyeshwa mara nyingi sana na Mchambuzi kuanzia mwaka 1964 hadi leo ambapo tuna Tanganyika tu inayojiita Tanzania. Zanzibar haipo kabisa ina wimbo wa taifa, mipaka, Rais, vikosi vya jeshi taasisi, makamu wa Rais wengi tu n.k.

Pinda, Nape Nnauye , Mwigulu, Gamba la Nyoka, Mkandara, Mtanganyika njooni hapa tuhangaike pamoja. Landa mtatueleza tusichokujua. Tanzania ilivypatikana kwa majina ndiyo hiyo kasema Mag3, Mchambuzi kaonyesha msukule uliyoipoteza Tanganyika, haijafa mind you!
Nanyi njooni mtuambie Muungano wa Tanzania na Zanzibar ulikuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom