What a positive comment...bravo!Nimeyatumia mara mbili, nilikua na shauku ya kutaka kuhisi yalivyo. Ama kwa kweli huu ni mradi unaofaa kufaulu, utani pembeni, huu mradi Wabongo walifaa kuupokea vizuri na kuufanya ufaulu lakini kwa sasa sijui wanavyokwenda. Aidha mimi itakua nilikua na bahati mbaya ya kusafiri siku isiyofaa. Kwa kuzitumia mara mbili nilikumbana na mambo yasiyofaa. Yafuatavyo
Dereva kugombana na abiria, kuna mama wawili waliokalia kiti kimojaa kinachofaa kutumiwa na abiria mmoja. Ssasa dereva alitoka usukani akaja kugombana nao hadi mmoja akasimama. Jamaa alionekana mwenye hasira za kuchoka, hamna tofauti na wale wa madaladala ya kawaida.
Wabongo wengine kutofuata foleni, yaani tupo tumepanga foleni ya kulipia kwenye kituo, wanakuja pembeni na kujichomeka chomeka pale mbele karibu na mhudumu wa kupokea hela.
Uendeshaji wa breki za ghafla, duh hili bana, yaani mumejazana halafu breki hiyooo.
Kujazana sana huku wengi wakisimama, labda yanafaa kuwa na kiwango.
Kuchelewa, kuna mengine yanasubiriwa sana, umelipia lakini haliji.
Risiti kugoma goma, inaonyesha duplicate wakati msafiri amelipia papo hapo. Niliona baba fulani akiteseka sana kwa hili.
Wakati wa kutoka risiti ilinigomea ikabidi mhudumu anifungulie mlango mwenyewe, halafu hata wahudumu wenyewe hawapo muda wote. Unakuta risiti zinagoma kufungua kiingilio cha kituo na hamna mhudumu wa kuelekeza karibu.
Mara ya kwanza nilitupa risiti kwenye pipa la taka mara tu baada ya kushuka, sikujua unafaa udumishe risiti hadi utoke nje ya kituo, ilibidi niombe kufunguliwa kiingilio. Aidha ningelazimika kulipia tena, panafaa kuwa na maelekezo.
Pia niliabiri pale Posta ya zamani nikiwa na nia ye kwenda Ubungo, nikajikuta Kivukoni halafu likaegezwa pembeni na kuombwa tushuke tusubiri la kwenda Ubungo. Japo hapa siwezi kuwalaumu maana sikuwa makini kwa kuangalia linakoelekea, mimi nilina limeandikwa Ubungo nikajua basi huko ndiko litakwenda.
Lingine nilipanda nikiwa na kusudi la kwenda mjini kumbe la Gerezani, pia siwezi kuwalaumu hapa maana pia sikua makini.
Halafu hayafai kwa watu wanaosafiri kwa umbali mfupi, maana nauli ni ile ile ilhali madaladala yameondolewa barabarani.
However we acknowledge there are some challenges, received but we are zero tolerance in any insults or abuse to Tz by Kenyans...if we cannot collaborate or working together, then go ur way...in fact whatever we are doing here does not have any coin from your country and therefore we are not accountable to you..