Tanzania Military Intelligence vs TISS

Tanzania Military Intelligence vs TISS

Status
Not open for further replies.
TISS ni zaidi ya uijuavyo. Wengi wenu mtaishia kujua kitengo kimoja tu cha PSU.

Kwa kuwa habari nyingi zimezuiliwa ( classfied ), watu hubaki kudhania hivi na vile ama vile.

Idara ipo imara, tena sana ingawaje kuna changamoto za hapa na pale.

Naipa kongole TISS kwa kazi nzuri.

Huko 'Jey wii' nako "kuko njema" sana.

Mtoa mada! 'Ngoma droo' tu huko MI & TISS.
 
Hivi ni vyombo vinavyofanya kazi sawa (Usalama wa Taifa) lakini vinatofautiana in terms of scope (coverage).

Scope/coverage ya TISS ni ndani ya nchi na coverage ya MI ni nje ya nchi (Eg. Tuna uadui na Rwanda...je Kenya na Uganda wanachezea team ipi? Kuna msaada wowote wa kijeshi unaotoka Kenya kwenda Rwanda ? Adui zetu ni nani na wamejipanga vipi?

Pia military intelligence wanakuwa na full contigency plan ya vita na nchi zote zinazotuzunguka- Inaitwa Commander's Estimates.

Kwa mfano...Ikitokea Kenya wamepata rais kichaa kesho akaamka na kuanza kuishambulia TZ, tayari sisi tuna mchoro mzima wa vita (huo mchoro ndo huitwa Commader's estimate- tutahitaji jeshi kubwa kiasigani, vifaru vingapi, mafuta kiasigani yatatumika kuweka kwenye magari, vifaru, ndege na itatuchukua mudagani kuwamudu )...hii ni topic ndefu sana..unaweza kuijadili siku nzima..

Aisee,
 
Habari tamu sana hii tunaomba wataalam watujuze zaidi

Cc: RUCCI

Kwa ufahamu wangu tu, ukizungumzia MI au CMI au kwa jina lingie lolote lile, unagusa ujasusi au udukuzi katika mrengo wa kijeshi zaidi. Ufanisi wake ni lazima uwe wa juu kwa sababu una-specialization japokuwa yapo pia mambo mengi ndani yake yanayohusiana nayo. TISS kwa upande wake is all about the overrall security ya nchi ikijielekeza katika maeneo yote nyeti kwa usalama wa nchi. TISS kwa maana yake halisi inatakiwa iwe na wataalamu waliobobea katika fani anuai kama vile fedha, jeshi, elimu, nishati, siasa nk.

Kwa maana hiyo kufanya ulinganifu kati ya taasisi hizo mbili bado sioni kama tunaweza kupata majibu yenye uhalisia. Zote zinafanya ujasusi lakini malengo yake ni tofauti, settings za kufanyia kazi zao zinatofautiana.
 
Mkuu setting zao zinatofautiana kivipi ,nyumbua basi ili tuelewe kwa kina
 
Wadau wote mmeenda chaka
TISS ni taasisi kubwa sana inayoingilia mambo yote ya nchi ilhali CDI (Defense Intelligency) ni kwa ajili ya masuala ya kijeshi tu. inapokuja fani ya ujasusi TISS ni shughuli ingine.

Bazazi
Upo sahihi kwa 100%. Ambaye hataelewa ulichoandika basi ni Kanjanja wa div 5. Watu hawajui kuwa MI ipo ndani ya Jeshi. Lakini TISS ni idara inayojitegemea na majukumu yake yapo kila sehemu ikiwa ni pamoja na mambo ya Jeshi . TISS inagusa SIASA za nchi, uchumi, Social Affairs , Mahusiano nk ambapo jukumu lake nikufanya tathmini ya kiusalama na mwisho kushauri njia sahihi zakuchukuliwa na mamlaka stahiki.
 
Wadau nadhani kwakuwa wote tumeshapata picha kuhusu hizi idara mbili. Sasa hebu tuangalie wamefaulu vipi ktk kazi zao. Nitoe mfano tu wa Marekani ambapo CIA na intelligence organisations zingine zimefanikiwa kuifikisha Marekani hapo ilipo na kuwa Taifa lenye nguvu na sauti zaidi hapa duniani.wamefanikiwa hata kuiangusha dola kubwa iliyokuwa Hasimu wake mkuu yaani USSR. Hata hivyo kuna sehemu idara hizo za kijasusi za USA zilifanya makosa hata kugharimu maisha ya watu. Mfano tukio la Sep 11.

Sasa kwa hapa kwetu, mtizamo wangu ni kwamba Hizi idara zetu zimefanya mengi makubwa sana hasa hali ya usalama na Amani iliyopo kwa miaka mingi sasa, umoja wa kitaifa na Jeshi lenye Nidhamu kubwa sana ambapo hata baadhi ya nchi zilishasikika zikitamani kuwa na Jeshi lenye nidhamu kama Tz. Kwasababu inaaminika kuwa ni mara chache sana kukuta nchi masikini ikawa na jeshi lenye nidhamu. Mifano ipo mingi sana. Sasa yote hii ni kazi ya idara zetu hizi.

Success ingine ya idara zetu hizi ni ushindi ktk vita ya kagera. Kuna msemo kuwa ukiwa na MI imara basi ni rahisi kushinda vita hata kama adui ana silaha kuliko zako. Hata hivyo pamoja na success ya zaidi ya 90% lakini pia kuna sehemu kulifanyika mistakes. Mfano:-

1. Kushindwa kuzuia mashambulizi kwenye ubalozi wa Marekani. Jukumu la Tiss

2. Mabomu ya gongo la mboto na mbagala. Jukumu la MI. Walipaswa ku fore see.

3. Kutoroka kwa kanali Seromba. Kinachodaiwa kuwa sio raia wa Tz na ni Mrwanda. Kama ni kweli basi Vetting ya kujiunga na Jeshi is questionable kwani hadi kufikia cheo hicho ni kwanini hakubainika. Yamkini kuna wengine wengi wamebaki bado. Na kama ni kweli alikuwa ni raia wa nchi jirani basi ujasusi wao ni wa hali ya juu kuzidi wa kwetu kwani wameweza kumuingiza mtu akiwa na umri mdogo hadi anapata vyeo vi kubwa karibia na retirement age.

INGAWA MENGI YALIYOFANYWA NA IDARA ZETU NI MAZURI NA YALIYOTUKUKA LAKINI WANATAKIWA KUWA MACHO ZAIDI
 
ni muhimu kuelewa kuwa vyombo vyote vina lengo la kulinda nchi yetu , TISS wapo juu aisee ,wapo wale wa foreign kwenye balozi zetu wapo ndio walipotokea kina Membe lakini kwa kweli Military intelligence wanapiga kazi na kuna vichwa kweli humu , politics hazijaingia humu ila TISS wanapata kura yangu ni kweli wanapokea lawama sana ila watu wengi hawajui amani tuliyonayo bongo hawa jamaa wamechangia sana kama ilivyo
 
Inaitwa MI.... Hicho ulichotaja ni cheo ...CMI - chief of millitary intelligence .....Msaidizi wake anaitwa DMI - director of Millitary Intelligence.
kazi ngumu Sana Hiyo ..hawa Ndio hufanya infiltration kwenye Nchi yeyote yenye mwelekeo wa kuwa Adui ...ukisikia watu wanatangaza vita ujuwe hawa miaka hadi mitatu kabla walishaingia kwa Adui .. ( kujipenyeza)

Duuuuh kuna wanajamii ni intelligent sana humu ndani mmhhh. Kuna vichwa vilipaswa kuteuliwa kwenye wizara za ulinzi sema tu this system is too corrupt to spot your talents wakuu..give us some more wakuu.
 
Kwa ufahamu wangu tu, ukizungumzia MI au CMI au kwa jina lingie lolote lile, unagusa ujasusi au udukuzi katika mrengo wa kijeshi zaidi. Ufanisi wake ni lazima uwe wa juu kwa sababu una-specialization japokuwa yapo pia mambo mengi ndani yake yanayohusiana nayo. TISS kwa upande wake is all about the overrall security ya nchi ikijielekeza katika maeneo yote nyeti kwa usalama wa nchi. TISS kwa maana yake halisi inatakiwa iwe na wataalamu waliobobea katika fani anuai kama vile fedha, jeshi, elimu, nishati, siasa nk.

Kwa maana hiyo kufanya ulinganifu kati ya taasisi hizo mbili bado sioni kama tunaweza kupata majibu yenye uhalisia. Zote zinafanya ujasusi lakini malengo yake ni tofauti, settings za kufanyia kazi zao zinatofautiana.

Naamini wanafanyakaz kwa pamoja. Ijapokuwa ni taasis mbili tofauti, ila uwezekano wa top officials wa kila upande kushare habari ni jambo la kawaida. Kama jibu la yule wa CIA, basi hata Tanzania jibu ni hilo hilo.
 
Kama tulivyoona kikatiba jukumu la ulinzi na usalama wa nchi liko chini ya Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Mwuungano wa Tanzania. Kwa nyakati tofauti baadhi ya majukumu hukasimiwa ( delegated ) kwa ofisi aidha ndani ya Ofisi ya Rais au Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jinsi hali ya hewa na majuku atakayoainisha Amiri Jeshi Mkuu.
Ili kufanya kazi kwa ufanisi vyombo hivi na vingine vyote vinavyoshughulikia ulinzi na usalama wa nchi yetu na mipaka yake vina utaratibu wa kuingia mikataba ya ushirikiano na vyombo husika kama hivyo kwenye nchi mbalimbali duniani aidha kwa dhima au kwa haja ili kutengeneza mtandao unaosaidia kuleta ufanisi katika majukumu yake nchini au kusaidia usalama nchi zingine. Kwa kifupi hizi ni idara mbili kati ya nyingi zilizopewa dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
 
Hivi ni vyombo vinavyofanya kazi sawa (Usalama wa Taifa) lakini vinatofautiana in terms of scope (coverage).

Scope/coverage ya TISS ni ndani ya nchi na coverage ya MI ni nje ya nchi (Eg. Tuna uadui na Rwanda...je Kenya na Uganda wanachezea team ipi? Kuna msaada wowote wa kijeshi unaotoka Kenya kwenda Rwanda ? Adui zetu ni nani na wamejipanga vipi?

Pia military intelligence wanakuwa na full contigency plan ya vita na nchi zote zinazotuzunguka- Inaitwa Commander's Estimates.

Kwa mfano...Ikitokea Kenya wamepata rais kichaa kesho akaamka na kuanza kuishambulia TZ, tayari sisi tuna mchoro mzima wa vita (huo mchoro ndo huitwa Commader's estimate- tutahitaji jeshi kubwa kiasigani, vifaru vingapi, mafuta kiasigani yatatumika kuweka kwenye magari, vifaru, ndege na itatuchukua mudagani kuwamudu )...hii ni topic ndefu sana..unaweza kuijadili siku nzima..

Umeivaa
 
Duuuuh kuna wanajamii ni intelligent sana humu ndani mmhhh. Kuna vichwa vilipaswa kuteuliwa kwenye wizara za ulinzi sema tu this system is too corrupt to spot your talents wakuu..give us some more wakuu.

Mkuu tambua jf kuna wa aina mbalimbali so inawezkna wanaotupa haya maujuzi ndio wahusika haswa coz kwa mtu wa kawaida huwez ng'amua haya mambo

Kiukweli nafurahia sana hii elimu
 
Kama tulivyoona kikatiba jukumu la ulinzi na usalama wa nchi liko chini ya Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Mwuungano wa Tanzania. Kwa nyakati tofauti baadhi ya majukumu hukasimiwa ( delegated ) kwa ofisi aidha ndani ya Ofisi ya Rais au Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jinsi hali ya hewa na majuku atakayoainisha Amiri Jeshi Mkuu.
Ili kufanya kazi kwa ufanisi vyombo hivi na vingine vyote vinavyoshughulikia ulinzi na usalama wa nchi yetu na mipaka yake vina utaratibu wa kuingia mikataba ya ushirikiano na vyombo husika kama hivyo kwenye nchi mbalimbali duniani aidha kwa dhima au kwa haja ili kutengeneza mtandao unaosaidia kuleta ufanisi katika majukumu yake nchini au kusaidia usalama nchi zingine. Kwa kifupi hizi ni idara mbili kati ya nyingi zilizopewa dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Jamaa wanatafuta nani yuko juu zaidi ya mwingine!!

Sasa kinachotokea hapa kila mtu anavutia kwake. Kwani kwenye gari kipi ni muhimu au ni noumer???matairi,engen,ngao,taa,au usukani??.

Kila mtu ana jukumu litakalo mfanya awe muhimu kwa wakati tofauti,ila ushirikiano haukwepeki.

Mfano kuna idara ambazo ukifika rank fulan automatic unakuwa expert wa tiss maana kuna ulazima wa kuwa hivyo hata kama hutaki.kama mtu ana uwezo achunguze.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom