Tanzania miongoni mwa nchi zenye uhuru mdogo zaidi wa mtandao

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Cloudwards 2026 ikihusisha nchi 171 ikitathmini viwango vyao vya udhibiti wa mtandao kwa kutumia vigezo vya; matumizi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, upatikanaji wa maudhui mbalimbali ya kisiasa na kidini, kanuni zinazohusu matumizi ya VPN pampja na maudhui ya kiutuuzima.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi hizo kwa kiwango cha asilimia 28%, ambapo nchi zingine za Afrika ni Ethiopia, Uganda, Misri na Sudan.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba sababu za udhibiti wa mtandao na mauddhui zinatofautiana, kuanzia kulinda watu wanaolengwa na matamshi ya chuki hadi kudhibiti upinzani wa kisiasa. Katika maeneo yenye vikwazo vikali zaidi, udhibiti na ufuatiliaji wa mtandao hutumiwa mara nyingi kama nyenzo za kudhibiti wa simulizi/nadharia

Utafiti huo unaeleza kwamba athari za kuvunja sheria za serikali kuhusu udhibiti wa maudhui hutofautiana kulingana na nchi, zinaweza kujumuisha faini, au hata kukamatwa na kufungwa jela, hasa katika maeneo yenye vizuizi vikali.

Katika kiwango cha aslimia 0-100% iliyotumika kupima kiwango cha uhuru wa mtandao, zipo baadhi ya nchi kama Ubelgiji, Costa Rica, Timor-Leste na New Zealand zilifikia asilimia 92% kiwango cha juu ya uhuru wa mtandao, hali inayomaanisha kuwa wananchi wake wanakabiliwa na vizuizi vichache zaidi mtandaoni

1775736800276.png
 
Na hata hiki kidogo Wana ccm hawakitaki
Unabinya uhuru wa habar
Mahakama
NGO/CSo
.vyama vya siasa
Kisha unasema unapambana na rushwa na ubadhilifu
 
Mnataka uhuru wa Aina ipi zaidi ya huu mkubwa uliopitiliza?
Uhuru upi mkubwa chawa ?

Hapo ulipo umewasha VPN kuingia hili jukwaa lililofungiwa baada ya ile post yenye taarifa ya wizi na ufisadi wa mgodi wa makaa ya mawe aliouibua Polepole ambaye alitekwa na kuuwawa.
 
Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Cloudwards 2026 ikihusisha nchi 171 ikitathmini viwango vyao vya udhibiti wa mtandao kwa kutumia vigezo vya; matumizi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, upatikanaji wa maudhui mbalimbali ya kisiasa na kidini, kanuni zinazohusu matumizi ya VPN pampja na maudhui ya kiutuuzima.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi hizo kwa kiwango cha asilimia 28%, ambapo nchi zingine za Afrika ni Ethiopia, Uganda, Misri na Sudan.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba sababu za udhibiti wa mtandao na mauddhui zinatofautiana, kuanzia kulinda watu wanaolengwa na matamshi ya chuki hadi kudhibiti upinzani wa kisiasa. Katika maeneo yenye vikwazo vikali zaidi, udhibiti na ufuatiliaji wa mtandao hutumiwa mara nyingi kama nyenzo za kudhibiti wa simulizi/nadharia

Utafiti huo unaeleza kwamba athari za kuvunja sheria za serikali kuhusu udhibiti wa maudhui hutofautiana kulingana na nchi, zinaweza kujumuisha faini, au hata kukamatwa na kufungwa jela, hasa katika maeneo yenye vizuizi vikali.

Katika kiwango cha aslimia 0-100% iliyotumika kupima kiwango cha uhuru wa mtandao, zipo baadhi ya nchi kama Ubelgiji, Costa Rica, Timor-Leste na New Zealand zilifikia asilimia 92% kiwango cha juu ya uhuru wa mtandao, hali inayomaanisha kuwa wananchi wake wanakabiliwa na vizuizi vichache zaidi mtandaoni

Tanzania hakuna uhuru wa maoni, mawazo na habari. Kila mtu analazimishwa kuisifia serikali, hata kama inaua watu kila kukicha.
 
Back
Top Bottom