Tanzania mpya: Chama cha Mapinduzi (CCM) kifutiwe usajili Tanzania

pulex

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
536
Reaction score
2,213
Tumefika hapa tulipo ni kwasababu ya CCM. Chama hichi kimeshapoteza misingi yake na dira, viongozi wanauana kwa sumu, utekaji na mauaji, ukandamizaji wa haki, ufisadi wa kufuru, yaani yale yaliopo kwenye kitabu cha msajili wa vyama kuhusu hichi chama yamekiukwa na inapaswa kufutiwa usajili pale nchi itakapo kombolewa mikononi mwa hawa majambazi.

Nakuhakikishia hata kama ikiletwa katiba mpya, ila hiki chama kikawepo, kuna siku wahuni watarudi na kuvunja hiyo katiba kama unavyoona kwa samia. Maana vyombo vya dola vimejaa watu wanakadi ya CCM, hiv hata nchi ikachukuliwa na Lissu na kwenye vyombo wamejaa maafisa wana makadi ya ccm kuna usalama hapo?.

Chama kimeiba sana mali za wananchi kujijenga chenyewe na kumiliki mali nyingi za chama, hivyo hata baada ya katiba mpya kitawasumbua watakaokuwepo madarakan, inabidi chama hichi kifutwe na mali zao zote zirudishwe kwa wananchi kupitia serikali, na chama kipya kianzishwe kiwe kama mpinzani, hakina mali za wizi, na kutakuwa na haki hata ya kushindana na vyama vingine. Ila ikifanyika kosa, katiba mpya ikaja na hiki chama kikaachwa na nguvu ya pesa walizonazo, na watu wao walivyo jaa kwenye mifumo (dola), yaani hyo katiba itakanyagwa kama uyu Samia anacho fanya, katiba iliyopo na mapungufu yote ila bado imekanyagwa na akijinasibu kuita ni kitabu tu, uku chama chake kipo kimya.

CCM inabidi ifutiwe usajili kwa maslahi mapana ya nchi, kukiacha hichi chama, ni kosa kubwa sana, nchi hata akichukua upinzani watasumbuliwa sana, fikiria usalama wa taifa umejaa UVCCM, alafu nchi anaenda shika mpinzani usalama wake uko wapi?, maana hawa wanaficha kadi zao mfukoni, hujui kma ni ccm, unashangaa umepigwa tukio. Ila ukifuta chama hawana ujanja, utakuwa umeangusha majini yote yaliyojificha kwenye dola wakiwa na kadi zao za CCM watakuwa wamekuwa neutralized.

Hili ni jambo la kuzingatiwa sana baadae, maana nimeona tunapoelekea, sio mbali, upinzani inachukua nchi pale uchaguzi utapokuja kuwa wa haki au kwa nguvu ya wananchi wataikamata dola, ila wasipokifuta CCM, watahujumiwa sana maana mifumo imeoza, kila afisa ana kadi ya CCM, watasabotage maendeleo ya chama kipya au kufanya chchte kibaya uku wakiwa wameahidiwa nafasi kubwa chama kikuu (CCM) kikirejea.

Nimeona niliongee hapa mapema ili watu walitafakari, maana na amini serikali mpya itakuja sio muda mrefu, na kuna watu kwenye hili jukwaa watakuwa viongozi, ushauri huu msiupuuze. CCM ni hatari ikiachwa hai iwe kwenye dola au nje ya dola.
 
Tusubiri 2030 hizi mbuzi za Tanzania bado hazijielewi mama Samia kishatupiga bao la mkono wa Nape mchana kweupe.
 
Naunga hoja mkono ila je mfutaji ndiye msajili au mwingine,mahakama,bunge au mhimili uliojichimbia? Je hili ndio litokee Tanzania hii ya ukosefu uwajibikaji,usawa,utii washeria kibaguzi kwa matabaka?
 
Sio tu Ccm iwapo mabadiliko yakitokea vyama vyote vya siasa Tz vinatakiwa kufutwa na Mali zake kutaifishwa
Kisha turuhusu usajil wa vyama vya siasa visivyozidi vinne tu
 
Back
Top Bottom