SoC04 Tanzania mpya: Kuanzisha chuo maalumu kitakachotoa taaluma kwa dada wa kazi za nyumbani

SoC04 Tanzania mpya: Kuanzisha chuo maalumu kitakachotoa taaluma kwa dada wa kazi za nyumbani

Tanzania Tuitakayo competition threads

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
TANZANIA MPYA: KUANZISHA CHUO MAALUMU KITAKACHOTOA TAALUMA KWA DADA WA KAZI ZA NYUMBANI.

Ni wazi kuwa Viongozi wakubwa wa serikali walioko madarakani na waliomaliza muda wao wengi wao walilelewa na wazazi wao wote wawili hasa mama ambaye muda mwingi alikua nyumbani.

Na katika malezi haya asilimia kubwa kulikuwa na vijana wengi wenye maadili mema ambao wengi wao ni viongozi wa sasa.

Lakini cha ajabu ni kuwa wawakilishi wa wananchi Bungeni ambao ndio watunga Sheria wamekuwa wakilalamikia mmomonyoko wa maadili kuwa umeongezeka ndani ya Jamii, bila kutafuta kiini cha tatizo hilo kubwa.

Sasa nani wa kulisaidia Taifa kama watunga Sheria wenyewe wanalalamika?

IMG_1483.jpeg

Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya Mwaka ya Mwaka 2004 katika moja ya vifungu vyake inaeleza wazi muda wa mama anaenyonyesha kurudi kazini mara baada ya miezi mitatu ya kukaa nyumbani na ile miezi mingine ya kuingia kazini nusu siku.

IMG_1485.jpeg

Mara baada ya miezi sita mzazi anapaswa kurudi kazini na kumuachia dada wa kazi mtoto.

IMG_1491.jpeg


Malezi ya dada wa kazi na mzazi ni sawa? Na tunatarajia kupata taifa lenye watu wa aina gani hapo mbeleni? Nani anajua wapi alipotoka dada huyu? Familia yake ikoje? Amekulia katika malezi ya namna gani?

IMG_1486.jpeg


Atawafundisha nini hawa watoto ili waje kuwa Viongozi bora wa baadae?

Kwanza tunapaswa kujiuliza huyu dada wa kazi ana uelewa wowote kuhusu malezi ya watoto? Amepitia mafunzo yapi?

Na hapa tunakumbushwa umuhimu wa kuwa na chuo maalumu kwa ajili ya watu watakaokuwa walezi wa watoto nyumbani.

Wakati Taifa likipitia kipindi kigumu cha kuwa na vijana waliokosa ajira basi lifikirie kuanzisha masomo kwa ajili ya watu hao muhimu ambao kila mtu anawahitaji na kuwatumia.

IMG_1487.jpeg


Lakini pia malezi ya maeneo ya vijijini ambayo mama wengi wako nyumbani wakiwalea watoto wao na watoto kuona namna wazazi wazazi wanavyochakarika utaona watoto nao wanarithi kutoka kwa wazazi wao.

IMG_1490.jpeg


IMG_1482.jpeg


IMG_1489.jpeg


Maeneo ya vijijini ndiko kunakopatikana vijana wachapakazi kutokana na malezi mazuri kutoka kwa wazazi wao na mmomonyoko wa maadili upo kwa kiasi kidogo sana.

IMG_1488.jpeg

Sasa nini kifanyike?
Bunge liangalie namna gani ya kumsaidia mwanamke ambae anafanya kazi masaa nane hadi kumi na mawili na kumuachia mfanyakazi watoto.

IMG_1483.jpeg


Kama ni hizi asilimia hamsini kwa hamsini basi wabunge wanawake wapambane Bungeni kutoa maoni eidha ya kuanzishwa kwa chuo maalumu cha kufundisha wadada wa kazi za ndani na watakaolipwa mshahara mzuri kwa sababu kazi ya kulea pia ni ngumu.

IMG_1486.jpeg


Chuo hicho cha kufundisha dada wa kazi kitasaidia kujua wapi walikotoka wadada hawa na ukatili majumbani kwa wadada na watoto kutapungua na tutapata kizazi bora kabisa.

Lakini pia Sheria mpya ikitungwa iangalie ni majukumu yapi apewe mama anaelea hadi hapo mtoto atakapofikia umri wa kwenda Shule.

Suala jingine linalosikitisha ni mishahara wanayolipwq baba wa familia.

Unakuta baba anategemewa na familia yake yenye watoto wanne na mshahara anaopewa unakuta haukidhi mahitaji ya Kodi,ada,matumizi nyumbani na mambo mengine sasa kwa nini mtu huyu asiibe.

IMG_1493.jpeg


Hali hii husababisha mama nae kuingia mtaani kutafuta kipato kwa kuwa pesa ya mume haitoshi hata kidogo hali inayosababisha watoto kuachwa wenyewe nyumbani na kujifunza vitu visivyofaa.

IMG_1495.jpeg

  • Tanzania mpya inahitaji mabadiliko katika sekta ya Sheria ili kulinusuru Taifa la Tanzania.
 
Upvote 7
Vizuri". pia Dada wa kazi walipwe mishahara mizuri
 
Ulikuwa na hoja nzuri mpaka pale uliposema kianzishwe chuo kwa ajili ya wadada wa ndani , kwamba mtu asipewe elimu nyingine afundishwe tu kuwa mlezi wa watoto , yaani iwe profession yake kwa maisha yake , mbona haiingii akilini
 
Back
Top Bottom