SoC04 Tanzania mpya yenye matumizi bora ya nishati ya gesi asilia

Tanzania Tuitakayo competition threads

Gentlemen_

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
4,431
Reaction score
13,876

KURASA 1: UTANGULIZI

Maono ya Serikali hivi karibuni yameonyesha ni jinsi gani imepania kufanya mapinduzi ya sekta ya nishati hapa nchini, rejea maagizo ya viongozi wetu wa juu hasa Mheshimiwa Rais
Mwananchi.JPG

Chanzo: Mwananchi

Pia, Rais Samia hakuishia hapo alitoa agizo kwa mheshimiwa Waziri Dkt. Seleman Jafo

Mwananchi - katazo.JPG

Chanzo: Mwananchi
Maoni ya Mdau baada ya agizo hilo:

Mwananchi - Mdau.JPG

Chanzo: Mwananchi

NINI KIFANYIKE?

Nigusie kidogo aina mbili ambazo ningependekeza zitumike kulingana na aina ya mazingira tuliyonayo, ubora wa teknolojia pia utaalamu tulionao kama nchi.

Compressed Natural Gas (CNG)
: Ni gesi ambayo haina harufu kali, haina ladha na haina sumu, gesi hii imeundwa na takribani asilimia 90% ya methane, naitrojeni, karbondayoksaidi, propeni na viambata vidogo mno vya etheni. Inatambulika kwa ubora wake wa kutunza mazingira kutokana na hilo basi inatambulika kuwa best alternative fuel type.

LNG fuel au Liquefied Natural Gas (LNG): Ni gesi asilia ambayo imebadilishwa kwenda kwenye hali ya kimiminika (Liquefied) baada ya kupitia mchakato maalumu wa Liquefaction. Katika mchakato huo gesi asilia inapoozwa kwenda katika viwango vidogo vya hali joto mpaka pale gesi hiyo kubadirika na kuwa kimiminika na uwingi wa gesi unashushwa kwa karibu mara mia sita!

Ikumbukwe LNG haina viambata vya sumu vya kuharibu (non-toxic & corrosive) pia LNG ikiwa imebanwa (compressed) ina uwiano wa 1/600 ukilinganisha na gesi asilia kabla haijafanyiwa mchakato, hali hii inafanya iwe gharama nafuu pia utunzaji wake kuwa rahisi na usafirishaji wake kuwa rafiki.

CNG na LNG ni sawa kwa kila kitu kasoro usafirishaji na utunzaji wake, pia uandaaji wa LNG ni gharama zaidi kulinganisha na CNG.

Kuielezea kwa ukubwa hatutamaliza leo, ingawa kitu cha msingi ni kukumbusha kuwa CNG ni rahisi kuiongeza (refuel) kuliko LNG ambayo inahitaji utaalamu na vifaa bora. Pia LNG inaweza kubadirishwa na kuwa CNG.

Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
MAPENDEKEZO

1. Kuundwa/Kuboreshwa kwa tume/chombo cha kusimamia gesi asilia

Tume hii itatumika kuratibu, kuendesha na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa nishati hii kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa ubora na usalama wa hali ya juu.

2. Kupanga gesi asilia katika matumizi ya makundi makuu matatu

Kundi A: Majumbani na maeneo ya biashara ya kipato cha chini;

Kundi B: Viwandani, Mashuleni, Mahospitalini Mahotelini n.k;

Kundi C: Stesheni za nishati na Karakana za Magari.

Alternative Fuels Data Center.jpg

Chanzo: Alternative Fuels Data Center

3. Kuandaa magari maalumu ya kusambaza gesi

Gari hizi zitatengenezwa au kuagizwa kwa matakwa maalumu ya nchi (Special Order)

slideserve.jpg

Chanzo: Slideserve

Screenshot_23-5-2024_142253_www.google.co.tz.jpeg

Chanzo: OpenPR
Gari hizi zitasambaza kwa njia mbili kama ifuatavyo:-
A - Kuacha Tenki katika eneo maalumu

Screenshot_23-5-2024_142555_www.google.co.tz.jpeg

Chanzo: Auyan company

B - Kujaza (Re-filling) gesi kama vile gari za maji inavyojaza katika matenki ya watumiaji mitaani.

Tianjin Sinogas.jpg

Chanzo: Tianjin Sino Gas

4. Rasilimali watu makini

Hapa nashauri Serikali kuwekeza katika wataalamu wapya na kuwatumia vizuri wataalamu waliopo. Huu mradi unapaswa kusimamiwa na watu walio na uzoefu, “exposure” na uzalendo wa hali ya juu.

Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika.

KURASA 2: JINSI MFUMO UTAKAVYOFANYA KAZI

1. Usalama:

Jambo la kwanza ni kuhakikisha mfumo huu ni salama kwa watumiaji wake, nimependekeza uchimbiwaji wa matenki ya gesi chini ya ardhi kwa urefu utakaonekana unafaa ft 6+ kulingana na ukubwa wa tenki. Kwanini?
  • Jua halitaathiri kwa kuongeza joto katika tenki hili
  • Mvua na hali zote za hewa hazitaathiri tenki hili
  • Halitafikiwa na vitu vya kuweza kulidhuru kirahisi mfano MOTO
  • Ni salama kwa watoto na watu mbalimbali wenye changamoto za akili n.k
  • Ni salama endapo kutatokea changamoto ya kuripuka.
Angalizo: Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kubaini na kuzuia hali mbalimbali za hatari mfano ‘ gas leakage ‘ , itakuwa na mfumo wa kuhisi joto kupitiliza hivyo koki kuu itajizima na kutuma taarifa kwa msimamizi (operator) mkuu wa hilo tenki. Mambo ni mengi nimeandaa MANUAL kuhusu mfumo huu.. naomba tuendelee mbele.

Shandong luen auto 2.jpg

Chanzo: Shandong Luen Auto

2. Mfumo wa malipo na kuanzisha huduma (Activation Scheme):

a. Tokeni maalumu:
Itaandaliwa system itakayoweza kupokea tokeni ili kuanzisha huduma ya gesi hiyo kwa kiwango fulani kulingana na tokeni husika kutoka katika tenki hilo lililopandikizwa ardhini, hili tenki linakuwa limewekwa na tume bila maombi ya moja kwa moja kutoka kwa mwananchi;

b. Bando kwa Kilogramu:
Gesi hii pia itajazwa kulingana na manunuzi ya mteja husika, ambapo itategemea na kilogramu ngapi kanunua zikiisha basi itahitajika gari lije kujaza upya, hili tenki linakuwa ni la mwananchi ambae ataamua alitumie kwa muda gani bila kuathiri usalama wake na watu wengine;

c. Jamii husika kuchangia gharama na kutumia kwa pamoja:
Hii inafaa hasa katika miji mipya ambapo tume itaweka ujenzi wa stesheni ya gesi asilia ambapo mifumo ya usambazaji itafanyika kutoka katika stesheni hiyo kwenda katika nyumba za jamii hiyo itakayoamua kujiunga kwa njia hiyo. Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.

Hii stesheni inakuwa ni mali ya tume, na bili za matumizi zitakuwa zinatumwa kwa jamii hiyo ambayo italipa kwa pamoja, ingawa kutawekwa pia mita ndogo ndogo kubaini na kugundua ni Kaya, Familia ipi iliyotumia gesi nyingi zaidi hivyo kulipa maradufu kulingana na matumizi yake.

Natural Gas.jpg

Chanzo: Natural Gas

KURASA 3: MATOKEO CHANYA

1- Utunzaji bora wa Mazingira
2- Kukuza uchumi

3- Kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia
4- Kuchochea uvumbuzi na ubunifu zaidi

5- Chachu ya ajira kwa Watanzania
6- Gharama za maisha kupungua

NAWASILISHA
 
Upvote 11
Na compression inafanyika ili kuweza kusafirisha / kutunza more in less space
My main point ipo hapa..

Katika eneo zima la space, kutunza na kusafirisha.

Utahitaji malori 50 kusafirisha CNG but kwa upande wa LNG utajitaji lori moja tu.. perhaps.

Kwa nature ya Nchi zetu je unafkiri kipi ni reliable?

Ni bora ulete LNG uje utumie kavu na uifanyie decompression au ulete CNG tupu katika distribution channels?
 
Unahitaji nishati nyingi zaidi na gharama kubwa zaidi kuicompress methane kuwa lng na utunzaji wake kubakia liquid ni gharama pia it only makes sense kama unaisafirisha mbali na hakuna alternative nyingine mfano kutoka bongo kwenye meli kwenda Japan n.k.

Kwa nchi within ni rahisi kuisafirisha gesi asilia kama yenyewe kwa mabomba mpaka kwenye vituo vya kujazia kama gesi asilia na ukifika pale ndio ufanye compression iwe gesi compressed (pressure hii sio kubwa kama ya kubadilisha gesi kuwa kimiminika) ukifanya hivyo utajikuta nishati hii inakuwa gharama na kama issue ni usafi wa nishati na hautaki kutumia CNG, LPG au Umeme ni bora kuwaza hata Hydrogen Gas..., lakini kwa bongo CNG is way to go kweye magari
 
Lakini kwa bongo CNG is way to go kweye magari
katika magari inatumika, ingawa msisitizo upo katika matumizi majumbani, kuepuka kuni, mkaa etc.

Ulisema Distribution ya CNG ni throughout Pipelines kwa nature ya miji yetu/Nchi yetu kutandaza Pipelines za Gas ni reliable?
 
Kwenye magari ni best alternative sababu tunayo na investment itakuwa ni pipes kutoka kwenye source mpaka baadhi ya vituo ili kujazia watu hii gesi asilia under pressure na kuwa CNG (Compressed Natural gas)

Hapana nimesema gesi asilia ya Mtwara the best alternative ingekuwa kuisambaza kwenye mabomba kama mabomba ya maji katika kila Kaya jambo ambalo kwetu sisi sio practical na ni gharama na ndio maana watu / madalali wanavutia kutumia kutumia LPG ambayo tunaagiza kutoka nje au mimi nimeshauri tutumie umeme katika mapishi....

Sasa nachokikwepa ni long distribution ya Pipelines.. ni gharama sio safe and reliable..

That's why nikaopt kusafirisha LNG ije ihifadhiwe ktk vituo vikuu vya mkoa then ifanyiwe decompression ije ktk CNG na kusambazwa through different ways including Pipelines na magari maalumu..

Just imagine usambaze Pipelines katika nchi nzima itawezekana vipi?... si rahisi.

Tupige hesabu ndogo tu... umeme UNIT 1 ni kiasi gani... umeme kwa matumizi tu ya kawaida haujatosha je tukiongeza na kupikia itakuwaje...?

Calculate cost comparison ya umeme na gas tuone which is reliable.. (Mchanganuo)

Nice contents so far..
 
Ahsante sana... kwa mchango wako na swali zuri.

Ukisoma vizuri kuna kipengele cha RASILIMALI WATU ambapo niliandika hivi:

"Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika"

Nilifikiria hiyo changamoto mwanzo pia nilitoa pendekezo la kuwa na TUME ambayo itakuwa serious na hili swala.
Sawa sawa, kwakweli kwa suala la gesi tuwe makini sana
 
Sasa nachokikwepa ni long distribution ya Pipelines.. ni gharama sio safe and reliable..

That's why nikaopt kusafirisha LNG ije ihifadhiwe ktk vituo vikuu vya mkoa then ifanyiwe decompression ije ktk CNG na kusambazwa through different ways including Pipelines na magari maalumu..

Just imagine usambaze Pipelines katika nchi nzima itawezekana vipi?... si rahisi.
Unajua option nzuri zaidi ? Kama issue ni kupikia wala isisambazwe sehemu zote ipelekwe tu kwenye vyanzo vya kufua umeme ili ibadilishwe kuwa umeme na kusambazwa kwenye kila kaya hapa hakuna haja ya compression ni pipe to kutoka kwenye source mpaka kwenye ufuaji na kama vipi ufuaji ufanyike huko huko kwenye source hakuna sababu ya kusafirisha
Tupige hesabu ndogo tu... umeme UNIT 1 ni kiasi gani...
Hii ipo kwenye uzi huu
post number 30

Kwa mahesabu ya haraka haraka kilo moja ya LPG ni kama 13.6 Kwh (yaani units 13.6) ule mtungi wa kwenye elfu 60 average tuseme una kilo 15 (ingawa sio 15 kuna uzito wa cylinder) kwahio mtungi huu una kama 13.6 x 15 = 204 Units

Kwahio tuseme kwa bei ya sasa ya mtungi inabidi unit moja iwe kwenye 294/= (60,000/= gawia 204)

Tukija kwenye ufanisi kama mtu atatumia induction cooker ambayo ni most efficient kulikio hata gesi.... (Kuna vyanzo vinasema zaidi ya mara tatu) utaona kwamba umeme unaweza ukawa Nishati Safi Kabisa ya kupikia na gharama ndogo kabisa...
umeme kwa matumizi tu ya kawaida haujatosha je tukiongeza na kupikia itakuwaje...?

Calculate cost comparison ya umeme na gas tuone which is reliable.. (Mchanganuo)

Nice contents so far..
Mkuu unajua bwawa likiisha at full capacity tutakuwa tumedouble uzalishaji wa umeme ? Na kama hautoshi kwanini tusiongeze ?
 
Unajua option nzuri zaidi ? Kama issue ni kupikia wala isisambazwe sehemu zote ipelekwe tu kwenye vyanzo vya kufua umeme ili ibadilishwe kuwa umeme na kusambazwa kwenye kila kaya hapa hakuna haja ya compression ni pipe to kutoka kwenye source mpaka kwenye ufuaji na kama vipi ufuaji ufanyike huko huko kwenye source hakuna sababu ya kusafirisha

Hii ipo kwenye uzi huu
post number 30

Kwa mahesabu ya haraka haraka kilo moja ya LPG ni kama 13.6 Kwh (yaani units 13.6) ule mtungi wa kwenye elfu 60 average tuseme una kilo 15 (ingawa sio 15 kuna uzito wa cylinder) kwahio mtungi huu una kama 13.6 x 15 = 204 Units

Kwahio tuseme kwa bei ya sasa ya mtungi inabidi unit moja iwe kwenye 294/= (60,000/= gawia 204)

Tukija kwenye ufanisi kama mtu atatumia induction cooker ambayo ni most efficient kulikio hata gesi.... (Kuna vyanzo vinasema zaidi ya mara tatu) utaona kwamba umeme unaweza ukawa Nishati Safi Kabisa ya kupikia na gharama ndogo kabisa...

Mkuu unajua bwawa likiisha at full capacity tutakuwa tumedouble uzalishaji wa umeme ? Na kama hautoshi kwanini tusiongeze ?
Je cost comparison ya kuibadiri gesi kuwa nishati ya umeme ipoje?...

So far ni mchakato kutoka hatua moja kwenda nyingine..

Hata Nchi zilizoendelea bado zipo ktk transformation..

Mfano: Magari ya petrol na Dizel sahivi yanapigwa chini.. wakahamia ktk hybrid (Petrol/Diesel & LPG, CNG/Electrical)

Kutoka ktk hybrid wanahamia ktk full electrical vehicles..

Sisi bado tupo ktk Matumizi ghafi ya PETROL na DIESEL bado hatak hybrid haijachanganya..

Ina maana kama tutaweza kumaintain umeme ukawa stable na kupatikana kwa bei nzuri UMEME ni best option but bado hatujafikia huko tupo on transformation.. ndio maana best option kwa sasa ni Gesi Asilia..
 
Je cost comparison ya kuibadiri gesi kuwa nishati ya umeme ipoje?...
Cost comparison ya kubadilisha gesi kuwa umeme hapo ni kwamba ile gesi inawasha boilers ni kama wewe unavyochemsha maji kwahio hapo ni direct use ya hio gesi inasafirishwa mpaka kwenye mtambo wa umeme na inatumika kama vile ambavyo ungetumia mafuta kuwasha generator maji kuzungusha water wheel n.k....

It's a practical cost effective means
 
KURASA 1: UTANGULIZI

Maono ya Serikali hivi karibuni yameonyesha ni jinsi gani imepania kufanya mapinduzi ya sekta ya nishati hapa nchini, rejea maagizo ya viongozi wetu wa juu hasa Mheshimiwa Rais
View attachment 2998022
Chanzo: Mwananchi

Pia, Rais Samia hakuishia hapo alitoa agizo kwa mheshimiwa Waziri Dkt. Seleman Jafo

View attachment 2998024
Chanzo: Mwananchi
Maoni ya Mdau baada ya agizo hilo:

View attachment 2998025
Chanzo: Mwananchi

NINI KIFANYIKE?

Nigusie kidogo aina mbili ambazo ningependekeza zitumike kulingana na aina ya mazingira tuliyonayo, ubora wa teknolojia pia utaalamu tulionao kama nchi.

Compressed Natural Gas (CNG)
: Ni gesi ambayo haina harufu kali, haina ladha na haina sumu, gesi hii imeundwa ka takribani asilimia 90% ya methane, naitrojeni, karbondayoksaidi, propeni na viambata vidogo mno vya etheni. Inatambulika kwa ubora wake wa kutunza mazingira kutokana na hilo basi inatambulika kuwa best alternative fuel type.

LNG fuel au Liquefied Natural Gas (LNG): Ni gesi asilia ambayo imebadirishwa kwenda kwenye hali ya kimiminika (Liquefied) baada ya kupitia mchakato maalumu wa Liquefaction. Katika mchakato huo gesi asilia inapoozwa kwenda katika viwango vidogo vya hali joto mpaka pale gesi hiyo kubadirika na kuwa kimiminika na uwingi wa gesi unashushwa kwa karibu mara mia sita!

Ikumbukwe LNG haina viambata vya sumu vya kuharibu (non-toxic & corrosive) pia LNG ikiwa imebanwa (compressed) ina uwiano wa 1/600 ukilinganisha na gesi asilia kabla haijafanyiwa mchakato, hali hii inafanya iwe gharama nafuu pia utunzaji wake kuwa rahisi na usafirishaji wake kuwa rafiki.

CNG na LNG ni sawa kwa kila kitu kasoro usafirishaji na utunzaji wake, pia uandaaji wa LNG ni gharama zaidi kulinganisha na CNG.

Kuielezea kwa ukubwa hatutamaliza leo, ingawa kitu cha msingi ni kukumbusha kuwa CNG ni rahisi kuiongeza (refuel) kuliko LNG ambayo inahitaji utaalamu na vifaa bora. Pia LNG inaweza kubadirishwa na kuwa CNG.

Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
MAPENDEKEZO

1. Kuundwa/Kuboreshwa kwa tume/chombo cha kusimamia gesi asilia

Tume hii itatumika kuratibu, kuendesha na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa nishati hii kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa ubora na usalama wa hali ya juu.

2. Kupanga gesi asilia katika matumizi ya makundi makuu matatu

Kundi A: Majumbani na maeneo ya biashara ya kipato cha chini;

Kundi B: Viwandani, Mashuleni, Mahospitalini Mahotelini n.k;

Kundi C: Stesheni za nishati na Karakana za Magari.

View attachment 2998030
Chanzo: Alternative Fuels Data Center

3. Kuandaa magari maalumu ya kusambaza gesi

Gari hizi zitatengenezwa au kuagizwa kwa matakwa maalumu ya nchi (Special Order)

View attachment 2998034
Chanzo: Slideserve

View attachment 2998037

Chanzo: OpenPR
Gari hizi zitasambaza kwa njia mbili kama ifuatavyo:-
A - Kuacha Tenki katika eneo maalumu

View attachment 2998038
Chanzo: Auyan company

B - Kujaza (Re-filling) gesi kama vile gari za maji inavyojaza katika matenki ya watumiaji mitaani.

View attachment 2998041
Chanzo: Tianjin Sino Gas

4. Rasilimali watu makini

Hapa nashauri Serikali kuwekeza katika wataalamu wapya na kuwatumia vizuri wataalamu waliopo. Huu mradi unapaswa kusimamiwa na watu walio na uzoefu, “exposure” na uzalendo wa hali ya juu.

Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika.

KURASA 2: JINSI MFUMO UTAKAVYOFANYA KAZI

1. Usalama:

Jambo la kwanza ni kuhakikisha mfumo huu ni salama kwa watumiaji wake, nimependekeza uchimbiwaji wa matenki ya gesi chini ya ardhi kwa urefu utakaonekana unafaa ft 6+ kulingana na ukubwa wa tenki. Kwanini?
  • Jua halitaathiri kwa kuongeza joto katika tenki hili
  • Mvua na hali zote za hewa hazitaathiri tenki hili
  • Halitafikiwa na vitu vya kuweza kulidhuru kirahisi mfano MOTO
  • Ni salama kwa watoto na watu mbalimbali wenye changamoto za akili n.k
  • Ni salama endapo kutatokea changamoto ya kuripuka.
Angalizo: Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kubaini na kuzuia hali mbalimbali za hatari mfano ‘ gas leakage ‘ , itakuwa na mfumo wa kuhisi joto kupitiliza hivyo koki kuu itajizima na kutuma taarifa kwa msimamizi (operator) mkuu wa hilo tenki. Mambo ni mengi nimeandaa MANUAL kuhusu mfumo huu.. naomba tuendelee mbele.

View attachment 2998047
Chanzo: Shandong Luen Auto

2. Mfumo wa malipo na kuanzisha huduma (Activation Scheme):

a. Tokeni maalumu:
Itaandaliwa system itakayoweza kupokea tokeni ili kuanzisha huduma ya gesi hiyo kwa kiwango fulani kulingana na tokeni husika kutoka katika tenki hilo lililopandikizwa ardhini, hili tenki linakuwa limewekwa na tume bila maombi ya moja kwa moja kutoka kwa mwananchi;

b. Bando kwa Kilogramu:
Gesi hii pia itajazwa kulingana na manunuzi ya mteja husika, ambapo itategemea na kilogramu ngapi kanunua zikiisha basi itahitajika gari lije kujaza upya, hili tenki linakuwa ni la mwananchi ambae ataamua alitumie kwa muda gani bila kuathiri usalama wake na watu wengine;

c. Jamii husika kuchangia gharama na kutumia kwa pamoja:
Hii inafaa hasa katika miji mipya ambapo tume itaweka ujenzi wa stesheni ya gesi asilia ambapo mifumo ya usambazaji itafanyika kutoka katika stesheni hiyo kwenda katika nyumba za jamii hiyo itakayoamua kujiunga kwa njia hiyo. Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.

Hii stesheni inakuwa ni mali ya tume, na bili za matumizi zitakuwa zinatumwa kwa jamii hiyo ambayo italipa kwa pamoja, ingawa kutawekwa pia mita ndogo ndogo kubaini na kugundua ni Kaya, Familia ipi iliyotumia gesi nyingi zaidi hivyo kulipa maradufu kulingana na matumizi yake.

View attachment 2998049
Chanzo: Natural Gas

KURASA 3: MATOKEO CHANYA

1- Utunzaji bora wa Mazingira
2- Kukuza uchumi

3- Kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia
4- Kuchochea uvumbuzi na ubunifu zaidi

5- Chachu ya ajira kwa Watanzania
6- Gharama za maisha kupungua

NAWASILISHA
🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom