Tanzania: Mtendaji wa Kijiji auawa na kuchomwa moto porini. Makamu wa Rais atoa salamu ya shilingi ml 5 Kwa familia

Tanzania: Mtendaji wa Kijiji auawa na kuchomwa moto porini. Makamu wa Rais atoa salamu ya shilingi ml 5 Kwa familia

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Serikali imesema baadhi ya watuhumiwa wanaodaiwa kumuua Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyahua wilayani Sikonge, Said Maduka kisha mwili wake kuuchoma moto na kuutelekeza porini, watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi wa kisayansi kukamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha rambirambi ya shilingi milioni tano kwa familia ya marehemu Maduka iliyopo kijiji cha Mibono Mpya wilayani Sikonge, iliyotolewa na Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango.

Chacha amesema Dkt. Mpango alitoa ahadi ya kuipatia rambirambi familia hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja wilayani Sikonge.

Inadaiwa kuwa Maduka aliauwa wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi ya kupeleka hati ya kuitwa mahakamani ‘Summons’ kwa familia mbili zilizokuwa zina mgogoro wa ardhi.

Mwili wa marehemu ulipatikana porini Septemba 21 mwaka huu.

Marehemu Maduka ameacha wake wawili, watoto sita pamoja na mama yake mzazi ambao wamegawanywa fedha hiyo ya rambirambi.

#AzamTVUpda
IMG-20241116-WA0010.jpg
 
Back
Top Bottom