Tanzania: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auawa katika maandamano ya upinzani Tanzania

Tanzania: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auawa katika maandamano ya upinzani Tanzania

KichwaNgumu254

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
1,284
Reaction score
1,152
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) nchini Tanzania, Akwiilina B Akwilina ameuawa wakati jeshi la polisi lilipotumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema.

Tukio hili limetokea jana wakati wafuasi wa Chadema na viongozi wao walipoandamana kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kudai fomu za mawakala wao. Wafuasi kadhaa wa Chadema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Profesa Prof. Zacharia Mganilwa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ameeleza kuwa mwanafunzi wao wa shahada ya Manunuzi na Ugavi Akwilina Akwilini alifariki dunia siku ya Ijumaa.Amesema mwili wa msichana huyo umekutwa na jeraha la risasi kichwani.

Kwa mujibu wa uongozi huo wa chuo hicho, mwanafunzi huyo alikuwa akielekea Bagamoyo kupeleka fomu za kuomba nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kuwa mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa wakati polisi walipokuwa wakitawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana.

Uchaguzi katika majombo ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam na Siha Mkoani Kilimanjaro unafanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majombo hayo, Maulid Mtulia na Dr Godwin Mollel kujiuzulu nyadhifa zao.

Link: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auawa katika maandamano ya upinzani Tanzania

Link: Tanzania's opposition accuse police of killing student
 
Naona hii ni Kenyan news.
NB:Zikiletwa habari nzuri kutoka Tanzania sitaki kuona nyumbu yoyote akilalamika
 
Bora umeamua kuleta taarifa yenyewe hapa. Wale walozoea kuimba Kenya mna roho mbaya, kutoka chee hadi machweo, hapa watapita kimya kimyaaa.
hakuna mtu anaepita kimia hapa. Serikali ya Magufuli yaku rahumiwa katika hili swala pamoja na polisi. Hakuna haja yakutumia live bullets kwenye mahandamano. East Africa countries we are all just shitholes. Hakuna mwenye unafuu kwenye swala la demokrasia. Uhuru is better in democrasy than Magu. Hili naongea kwa uwazi
 
Sasa hayo mauaji ndiyo mje kujilinganisha wakenya na wa Tz?
Kajilinganisheni kwenye miji na mapenzi na siyo uhai wa mtu.
Eti mapenzi? Hahaha! 😀 Sijui hapo ndo itakuwaje? Umesema ya kweli lakini. Ila jeshi la polisi kwenye nchi zote za Afrika Mashariki lina upungufu fulani, ikifika kwenye maswala ya kakabiliana na wananchi.
 
Bahati mbaya tu
Mnataka kushikilia bango
83e559cdb722437ab7761f9c86271c93.jpg
 
hakuna mtu anaepita kimia hapa. Serikali ya Magufuli yaku rahumiwa katika hili swala pamoja na polisi. Hakuna haja yakutumia live bullets kwenye mahandamano. East Africa countries we are all just shitholes. Hakuna mwenye unafuu kwenye swala la demokrasia. Uhuru is better in democrasy than Magu. Hili naongea kwa uwazi
Kumbe wakati mwingine huwa unachapia pointi za maana? Kula like yangu mkuu!
 
Mimi ni mtanzania hiyo sio bahati mbaya Bali walikusudia kuua mtu,sema lengo limefeli baada ya kuua MTU asiyekusudiwa!
Yote sawa ispokuwa watu wengine wana tafsiri vibaya kulinga na hali ilivyo.
Sio kila kitu kuhishtumu tu uowongozi mzima ukizingatia natukio lenyewe.
Mi ntafurahi watanzania nahasa police wote tukajifunza kuhusu hili swala.
Maana huu msiba si wa Chadema wala ccm bali ni wa nchi nzima.
Hakuna asie guswa na tukio hili la mzazi kupoteza mtoto kirahisi na alie msomesha kwa kipindi kirefu na usawa wenyewe kama huu.
 
Kumbe wakati mwingine huwa unachapia pointi za maana? Kula like yangu mkuu!
Kwenye hili wala msilinganishe Kenya na Tanzania, ni kama ardhi na mbingu. Tanzania mtu mmoja ameuliwa, polisi sita wameshakamatwa, serikali imekiri na kuomba msamaha kupitia rais, waziri na vyombo husika, rais ametoa kauli ya kulaani kitendo hicho na kuomba hatua kali zichukuliwe kwa waliohusika.

Kenya zaidi ya watu 60 waliuliwa wakati wa uchaguzi, serikali haijasema lolote zaidi ya kusema waliouliwa walijitakia, hakuna polisi yeyote aliyekamatwa na hakuna uchunguzi wala hatua yoyote iliyochukuliwa, kama vile waliokufa ni nguruwe hawana haki wala thamani yoyote ile.
 
Hii ni bahati mbaya mbona madaktari wanakosea sana kwenye kazi zao na kusababisha vifo vya uzembe kwa wagonjwa?

Kumlaumu au kumuhusisha JPM moja kwa moja au kwa namna yoyote na hili tukio ni utaahira mxiiiiu
 
Yote sawa ispokuwa watu wengine wana tafsiri vibaya kulinga na hali ilivyo.
Sio kila kitu kuhishtumu tu uowongozi mzima ukizingatia natukio lenyewe.
Mi ntafurahi watanzania nahasa police wote tukajifunza kuhusu hili swala.
Maana huu msiba si wa Chadema wala ccm bali ni wa nchi nzima.
Hakuna asie guswa na tukio hili la mzazi kupoteza mtoto kirahisi na alie msomesha kwa kipindi kirefu na usawa wenyewe kama huu.
Maandamano ya amani polisi wataendaje na silaha za moto na kuzifyetua usawa wa watu hapo unatetea uozo gani ndugu?
 
Maandamano ya amani polisi wataendaje na silaha za moto na kuzifyetua usawa wa watu hapo unatetea uozo gani ndugu?
Kwahiyo maandamo ya amani yasio na kibali wala kueleza umma nia na madhumuni ya hayo maandamo, unataka polisi wasubiri mpaka upepo ubadilike wauni wayateke hayo maadamano ndio polisi wakimbilie kutafuta silaha za moto. Hiyo polisi itachekwa dunia nzima.
 
Back
Top Bottom