Tanzania na Abbott wasaini Makubaliano ya kuanzisha Uzalishaji wa Vipimo vya haraka vya Magonjwa

Tanzania na Abbott wasaini Makubaliano ya kuanzisha Uzalishaji wa Vipimo vya haraka vya Magonjwa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesaini makubaliano ya ushirikiano (MoU) na kampuni ya kimataifa ya huduma za afya Abbott, kwa lengo la kuchunguza uwezekano wa kuanzisha uzalishaji wa vipimo vya haraka vya magonjwa mbalimbali hapa nchini.

Makubaliano hayo yamelenga kupunguza utegemezi wa bidhaa za afya kutoka nje ya nchi kwa kuongeza uzalishaji wa ndani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa Awamu ya Sita wa kuimarisha sekta ya afya kwa kutumia teknolojia na ubunifu wa kisasa

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mjini Dodoma, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Tanzania inategemea kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza vipimo vya UKIMWI, kaswende na homa ya ini ili kurahisisha upatikanaji wake, kupunguza gharama na kuiweka nchi kwenye ramani ya huduma bora za afya Afrika

Waziri Mhagama ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, Tanzania inaweza kuwa kitovu cha uzalishaji na usambazaji wa vipimo hivyo kwa nchi jirani, hali itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na afya kwa ujumla

Makubaliano haya ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya, kuongeza upatikanaji wa vipimo muhimu na kupambana na magonjwa yanayoambukiza kwa ufanisi zaidi




Chanzo: Jambo Tv
 
Back
Top Bottom