Tanzania na Afrika Kusini kukuza wigo wa Ushirikiano

Tanzania na Afrika Kusini kukuza wigo wa Ushirikiano

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Tanzania na Afrika Kusini kukuza wigo wa Ushirikiano

Tanzania na Afrika Kusini zinatazamia kukuza wigo wa ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati kwa manufaa wananchi wa pande zote mbili.

Hayo yanesemwa katika kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende-Malepe alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha pande hizo mbili zinakuza ushirikiano wao, Mhe. Waziri Kombo alisema kuwa ameunda timu ya wajumbe ambayo itajumuika na wajumbe kutoka Afrika Kusini kuunda tume itakayojadili fursa mbalimbali ambazo Tanzania na Afrika Kusini zinaweza kuziangazia na hivyo kuongeza wigo wa ushirikiano wao.

Kwa upande wake Balozi Noluthando amesema mbali na sekta ya biashara, Tanzania na Afrika Kusini zinaweza kuongeza ushirikiano kwenye uwekezaji, uchakataji wa bidhaa za kilimo, mafuta, gesi na madini.

Aidha, kwa pamoja viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuwa na eneo la kumbukumbu ya historia ya mataifa hayo mjini Morogoro.

publer-1741768837817.jpg
publer-1741768834090.jpg
publer-1741768832712.jpg
publer-1741768836917.jpg
publer-1741768839368.jpg
 
Labda kuongeza mabaharia wale kwenda kuuza kazi ambazo wamezikimbia tanzania.Yani mtu anazamia south afrika alafu anaenda kuuza sigara barabarani wakati hiyo kazi alikuwa hawezi kufanya huku
 
Back
Top Bottom