Tanzania na Burundi kuendeleza miradi ya pamoja ya maendeleo

Wadau,

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu.Hassani leo Mei 21, 2021 amepokea ujumbe kutoka kwa Rais Evarist Ndayishimiye wa Burundi.

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa Rais Samia Ikulu na mjumbe maalumu wa Serikali ya Burundi ambaye pia ni Waziri wa masuala ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni Mhesh Ezechiel Nibigila.

Katika ujumbe huo Mheshimiwa Rais wa Burundi alitoa pole kwa Mama Samia kufuatia msiba wa Rais Dkt John Magufuli, ammpongeza kwa kupokea kijiti cha Urais pamoja na kuwapongeza Watanzania kudumisha amani na utulivu kipindi cha mabadiliko ya Uongozi

Aidha Rais huyo wa Burundi ameahidi kudumisha mahusiano baina ya nchi zote mbili.

Kazi iendelee.
 
Ila Burundi wanatuthamini sana, tuna kila sababu ya kuwafavor
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…