Tanzania na Burundi kujenga reli ya thamani ya $900m

Kama vipi kila nchi ijenge reli yake mpaka mpakani. Na kusiwepo na ubia wa aina yoyote ile ili kuepukana na mkanganyiko usio wa lazima siku za baadaye kama huu tunao ushuhudia hivi sasa kwenye reli ya TAZARA.
Kabisa bora wafanye hivyo kuepuka mkanganyiko
 
Burundi ni waaminifu kwetu kuliko PAKA, napendekeza uhusiano wetu tuujenge Zaidi na Burundi kuliko Rwanda. kagame alipandisha tozo za maroli yanayopita kwake kwenda congo kwa karibia laki tano, ili kutukomoa, kwasababu anajua kwa pande ile hatuna njia nyingine kupeleka mizigo congo, na ametaka madereva wetu wakifika mpakani wakabidhi magari kwa madereva wa Rwanda ili wanyarwanda wapate ajira....ana kiburi chote, lazima tuwe na mbadala.
 
Hata TAZARA kila nchi iligharimia upande wake, ila mkataba unataka uendeshaji uwe wa pamoja na kwa mujibu wa mkataba Zambia ndiyo itakuwa inatoa Mkurugenzi Mkuu na Tanzania kutoa Naibu Mkurugenzi Mkuu.
Sasa huoni huo mkataba utakuwa ni wa Kimangungo! Reli ya TAZARA inajitosheleza kabisa kwa mahitaji ya Tanzania peke yake kutokana na kupitia maeneo mengi ya vijijini na mjini, na yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara. Achilia mbali wingi wa abiria wanao itumia hii reli katika vipindi vyote vya msimu wa mwaka!

Sasa leo hii TAZARA iko wapo! Iko ICU! Huduma ni mbovu kupitiliza! Na chanzo kikuu ni huu mkataba wao mbovu na Zambia. Ni kwa nini kila nchi isijitegemee kwa kila kitu kwenye uendeshaji wa reli yake?
 

Ungejua Kagame ndo Big boss labda usingeongea hivyo!
 
kweli japo kwa upande wake alikuwa akitengeneza ajira kwa watu wake.
Hivyo bora uaminifu uvunjike kuliko kutuumiza sisi.
 
Lengo la kujenga TAZARA ilikuwa kusafirisha shaba kutoka Zambia na ndiyo kisa cha mkataba huo wa hovyo. Sasa sifahamu kwa nini serikali inashindwa kuanzisha mchakato wa kubadilisha mkataba huu kwa sababu hivi sasa Zambia inapitisha kiasi kikubwa cha shaba yake bandari ya Afrika ya Kusini.

Wakati umefika kila nchi iwe na treni zake na kuziendesha. Hii italeta ufanisi na kila nchi itatunza hesabu zake.
 
Asante kwa taarifa, mipango waliyopanga itimie...
sio habar njema sana kwetu...!! sababu ukinukuu maneno ya wazir wa fedha anakwambia nchi hizo zikukubaliana kuangalia wapi watatafuta pakupata fedha ya kufadhili mradi huo" tafsir yake ni kwamba kwa kipindi hk wanaangalia wapi wanaweza wakakopa sasa maana yake deni la taifa litazid ku shoot tu yaan nchi inazid kuongeza madeni, mfumko wa bei kwa maana ya gharama za maisha zinazidi kupanda na hakuna unafuu wowote wa maisha! sasa sijui tunaelekea wapi
 

Kukopa na kufanya biashara sioni kama ni shida...
 
Burunfi wako chini sana kiuchumi, kielimu na karibu kwenye kila kitu EA, ajabu Tanzania imemkumbatia sana kama ally wake mkubwa.
Huenda kuna kitu/vitu wameona ambavyo vinaweza kuwa na faida Zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…