Counselor yon12
Member
- Aug 27, 2022
- 16
- 14
TANZANIA NA CHANGAMOTO ZA AFYA YA AKILI
Utangulizi
Afya ya akili kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa ni ustawi wa mtu kisaikolojia na kihisia. Mara nyingi miili yetu huwa na afya njema, lakini kuna wakati miili yetu hupata magonjwa mbalimbali na hivyo kuhitaji tiba ili kurudi kwenye hali au utimamu wake.
Mtu anapokuwa na homa, mvurugiko wa tumbo au aina nyingine za magonjwa nirahisi sana kutambua na hivyo kwenda kwa watoa huduma (hospitali) kwaajili ya kupatiwa matibabu na kufanyiwa vipimo kubaini ugonjwa unaomsumbua mhusika lakini je vipi kuhusu afya ya akili?
Ubongo wa mwanadamu pamoja na kazi zingine unajihusisha zaidi na udhibiti wa mawazo na hisia za mwanadamu. Kama ilivyo kwa miili yetu kupata na kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ubongo pia unaweza kuwa na ugonjwa na hivyo kupelekea kubadili hisia zetu, jinsi tunavyofikiri, jinsi tunavyoingiliana na kushirikkiana na watu wengine katika jamii na pia kubadili mienendo na maisha yetu kwa ujumla.
Mabadiliko haya ndiyo tunaweza kusema kuwa ni changamoto za afya ya akili (ugonjwa wa akili), kama ilivyo kwa magonjwa ya mwili mtu mwenye magonjwa ya akili anahitaji msaada kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili (washauri na wanasaikolojia) ili aweze kurejea katika hali au utimamu wake wa akili kama mwanzo.
Katika nyakati tofauti tofauti kumekuwa na matukio mengi yanayohusishwa na changamoto za afya ya akili hapa nchini. Vyombo mbalimbali vya habari mitandao ya kijamii katika kipindi hiki vimekuwa vikiripoti matukio ya mauaji ya kinyama, uzalilishaji na ukatili mkubwa wa kijinsia kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Changamoto hizi za afya ya akili zinaligarimu taifa kwani waathirika wakubwa ni vijana ambao ni wazalishaji wakubwa na wadau wakubwa wa maendeleo kwa taifa (nguvu kazi ya taifa). Hivyo basi kuwa na waathirika wa magonjwa ya akili wengi katika kundi hili la vijana kunalirudisha nyuma taifa kimaendeleo.
Takwimu za magonjwa ya akili nchini
Katika kuadhimisha siku ya afya ya akili duniani Oktoba 2021 iliripotiwa kuwa Watanzania milioni saba wana matatizo yanayohusiana na afya ya akili(chanzo Mwananchi.co.tz) na miongoni mwa sababu zilizotajwa kuchochea tatizo hilo ni msongo wa mawazo, ugumu wa maisha na matamanio yakuwa na maisha bora.
Takwimu za wizara ya afya nchini Tanzania zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne ana magonjwa ya akili (chanzo news.un.org/sw/story/2016) kutokana na hili mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore alinukuliwa akisema “watoto wengi na vijana, matajiri kwa masikini wote katika kona zote za dunia wanakabiliwa na magonjwa ya afya ya akili, janga hilo halina mipaka huku matatizo ya akili yakianza kabla ya umri wa miaka 14, tunahitaji mikakati ya haraka na bunifu katika kuzuia, kuchunguza na iwapo inahitajika kutibu katika umri mdogo”(chanzo news.un.org/sw/story/2016).
Lakini pia mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alinukuliwa akisema “ni watoto wachache tu wana uwezo wa kufikia programu zinazowafundisha mbinu za kukabiliana na hisia zao” (chanzo news.un.org/sw/story/2016). Hii inaonesha ni kwajinsi gani taifa na ulimwengu kwa ujumla unavyokabiliwa na changamoto za afya ya akili kwa watu wa rika lote na hivyo basi hatua makusudi zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti hali ya ongezeko la watu wenye matatizo ya afya ya akili.
Mapendekezo
Kuwatumia wataalamu wa saikolojia waliopo nchini ili kutoa elimu juu ya afya ya kili, changamoto zake, sababu zake, dalili zake na wapi mwathirika anaweza kupata msaada wa kisaikolojia.
Kuajiri na kufungua vituo vingi nchini vinavyoweza kutoa msaada wa kisaikolojia kwa jamii. Mfano serikali imeanzisha kwenye vituo vya polisi kitengo cha dawati la jinsia wanawake, wazee na watoto, kamati za mtakuwa, wasaidizi wa sheria vijijini (paralegal) maafisa ustawi na maafisa maendeleo kila ngazi lengo likiwa kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia bila kujua kuwa wanaofanya vitendo vya ukatili ni waathirika wa magonjwa ya akili na hvyo huhitaji zaidi msaada kutoka kwa wataalamu wa masuala ya saikolojia.
Kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014 (education and training policy of Tanzania 2014) iliyokuwa inataka kila shule kuajiri mshauri (counselor) ambaye atasaidia wanafunzi juu ya changamoto za afya ya akili wanazokumbana nazo shuleni. Utekelezaji wa sera hii ungesaidia kupunguza waathirika wa matatizo ya akili kwenye jamii zetu lakini pia kuongeza uelewa kwa jamii juu ya changamoto za afya ya akili.
Kuandaa mtaala mpya wenye somo linalohusu afya ya akili toka ngazi za chini za elimu hii itasaidia kupambana na matatizo ya afya ya akili katika umri mdogo.
Hitimisho
Nichukue fursa hii kuishauri serikali yangu kupitia wizara ya afya kuona umuhimu wa kuwa na wataalamu wa saikolojia watakaokuwa na uwezo wa kushughulikia changaomo za afya ya akili wataalamu hawa waajiriwe kama wanavyoajiriwa wataalamu wa afya ya mwili kwa wingi hili litasaidia kujenga jamii imara isiyo kuwa na changamoto za ukatili wa kijinsia, mauaji ya kikatili yasiyokuwa na sababu za msingi ambayo yanaligarimu taifa. Ikumbukwe kuwa hakuna afya ya mwili bila afya na utimamu wa akili.
Ahsanteni sana naomba kuwasilisha.

- Visa mbalimbali vilivyoripotiwa kutokana na changamoto za afya ya akili nipamoja na;
- Mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi
- Watoto kuua wazazi wao kutokana na mali
- Wazazi kuua watoto wao kutokana na ugumu wa maisha, udokozi na tabia mbaya
- Ubakaji na ulawiti kwa watoto
- Watu kujinyonga na kujirusha kwenye majengo marefu (gorofa) n.k

Attachments
Upvote
10