SoC02 Tanzania na changamoto za ukuaji wa viwanda vidogo vidogo

SoC02 Tanzania na changamoto za ukuaji wa viwanda vidogo vidogo

Stories of Change - 2022 Competition

Uledi peter mahanga

New Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Viwanda vidogo vidogo ni miongoni mwa sekta muhimu ambazo zinasaidia saaana kutatua changamoto za uhaba wa ajira na kukuza uchumi wa mtanzania mtu mmoja mmoja. Mfano wa viwanda hivyo ni kama uselemala, ufundi kushona na vingine vingi.

Viwanda hivi vidogo kama endapo vikawekewa mikakati ya kuvikuza ndio vinaweza kuwa kiwanda kikubwa ambacho kitasaidia kupata faida kama za serikali kukusanya mapato, kutatua tatizo la uhaba wa ajira nchini, kuondokana na watu wanaotegemea kuajiliwa zaidi na kupenda kujiajili

Viwanda hivi vidogo vimekuwa vikikumbwa na changamoto nyingi saaana. Moja ya changamoto ni uhaba wa mitaji, kukosa sifa za kukopesheka na taasisi za fedha Kwani dhamani zao ni kama hazitambuliki na taasisi hizo. Pia changamoto nyingine ni uduni wa teknolojia na uhaba wa masoko.

Ili kutatua changamoto hizo serikali inatakiwa kutengeneza mikakati endelevu Kwa ajili ya kuinua sekta ya viwanda vidogo ili baadae kuwa na matajili. Changamoto hizo zinaweza kutatuliwa Kwa njia zifuatazo

Kwanza kuimarisha Kwa kuiwezesha sekta ambayo inadhamana ya kusimamia viwanda vidogo yaani (SIDO). Ili kuiwezesha shirika hilo kufanya na kuwafikia viwanda vidogo linahitaji wataalamu ambao watasaidia kukuza viwanda hivyo vidogo. Vilevile serikali iwekeze hela au mtaji Kwa ajili ya kukopesha watu wa viwanda vidogo kama wanavofanya katika sekta ya kilimo.

Pia kutengeneza mazingira rafiki Kwa ajili ya kukuza sekta ya viwanda. Vilevile kutengeneza mazingira wezeshi Kwa ajili ya watu kupenda saaana sekta hiyo.

Pia kuboresha elimu ya ufundi kwani viwanda hivi vidogo Kwa sehemu ni mazao ya vyuo vya ufundi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom