Tanzania na Cyprus zasaini hati za makubaliano ya ushirikiano

Tanzania na Cyprus zasaini hati za makubaliano ya ushirikiano

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Dar es Salaam, 9 Julai 2025 – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Cyprus leo zimesaini hati za makubaliano (MoU) za kushirikiana katika mashauriano ya kisiasa na usafiri wa majini, hatua inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Hati hizo zimesainiwa wakati wa ziara ya kihistoria ya siku tatu nchini Tanzania ya Mhe Dkt. Constantinos Kombos, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus. Akifungua mkutano huo, mwenyeji wa mgeni huyo Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema ziara hii ni muhimu kwa sasa kwani uhusiano wetu umeamshwa na fursa mbalimbali za kiuchumi baina ya nchi zetu.

Akizungumzia kuhusu makubaliano yaliyosainiwa, Mhe. Kombo alisema ni matumaini ya Serikali kuwa makubaliano hayo yataleta chachu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali – ikiwemo utalii, kilimo, uchimbaji na utafiti wa madini, uchumi wa buluu, vyombo vya usafiri ikiwemo meli za biashara, soko la ajira, nishati mbadala na kuwezesha uwekezaji unaoongeza thamani.

Hatua hii itaziwezesha nchi hizi kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wake huku ikiimarisha nguvu kazi na pato la Taifa.

“ Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi Barani Afrika, na inatarajiwa kufikia ukuaji wa uchumi wa asilimia sita, mwishoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa IMF. Mafanikio haya yanatokana na amani na utulivu uliyopo nchini pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini".

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus Mhe. Dkt Kombos, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua chanya za ukuaji uchumi na kuimarisha uhusiano wa Kimataifa, kwani umesaidia kunufaisha Watanzania na kufungua milango ya fursa kwa mataifa mengine.

Mhe. Kombos amesema Serikali ya Cyprus itaendelea kukuza ushirikiano wake na Tanzania uliodumu kwa zaidi ya miaka 40, kwa kuangalia fursa mpya za ushirikiano zinazozingatia mahitaji ya pande zote na dira za maendeleo endelevu za mataifa hayo.

publer-1752094443223.jpg
publer-1752094444581.jpg
publer-1752094448619.jpg
 
Attachments

  • publer-1752094446061.jpg
    publer-1752094446061.jpg
    88.2 KB · Views: 38
  • publer-1752094449427.jpg
    publer-1752094449427.jpg
    77.2 KB · Views: 40
  • publer-1752094447560.jpg
    publer-1752094447560.jpg
    107.9 KB · Views: 32
  • publer-1752094441574.jpg
    publer-1752094441574.jpg
    66.4 KB · Views: 39
Hahahahahahaaa!
Kuna watu watapata kifaduro wakiona hili maana Ina chuki na mafanikio ya mama Samia hatari. Ilishaanza kuzusha eti Cyprus wanakuja kushughulikia suala la yule chiba na kibaraka wa ubelgiji anayevimbiwa ugali wa Bure Sasa hivi pale sello. Thubutuu, ulaya hao wamekuwa wapumbavu Hadi wafanye hivyo?!!!!
 
Cyprus wameona Tanzania ni shamba la bibi, na wao waje kubun wasichokipanda
 
Manyumbu ni nani? Sidhani kama ni jambo jema kuwaita wananchi wanaobebwa kwenye maroli kwenda kujaza mikutano ya kisiasa manyumbu.

Hata kama wanapewa tuvitu tudogo kama khanga, kofia, t shirts 👕 👕 na sasa baiskeli, neno nyumbu sio la kiungwana hata kidogo
 
Mgeni Humu wewe ee?!! Mbona wanaJF wote humu wanaelewa kuwa a.k.a ya mwanachadema yeyote ni nyumbu.
 
Hahahahahahaaa!
Kuna watu watapata kifaduro wakiona hili maana Ina chuki na mafanikio ya mama Samia hatari. Ilishaanza kuzusha eti Cyprus wanakuja kushughulikia suala la yule chiba na kibaraka wa ubelgiji anayevimbiwa ugali wa Bure Sasa hivi pale sello. Thubutuu, ulaya hao wamekuwa wapumbavu Hadi wafanye hivyo?!!!!
Naona umepagawa sana, tulia utizame mambo yanavyokwenda. Nyumbu ni mnyama asiyekua na akili, wasio na akili ndo hao wanaoswagwa kwenye malori na matrekta kama magunia ya viazi, wengine tuliwazika wakienda Simiyu. Hao ndo nyumbu, nadhan unajijua upo kwenye same group
 
Tehe tehe teheee! Eti 'utizame mambo yanavyokwenda'! Hivi mna mambo gani nyie nyumbu ya kuichenga serikali?!!!!!! Kila hatua yenu watu wanaifahamu kabla hamjakaa kuzungumza.
 
Back
Top Bottom