Tanzania na EU kuendelea kushirikiana kuimarisha amani na usalama Maziwa Makuu

Tanzania na EU kuendelea kushirikiana kuimarisha amani na usalama Maziwa Makuu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Johan Borgstam, katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungmzo yao Viongozi hao kwa pamoja wamejadili hali ya usalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu na juhudi za zinazochukuliwa katika kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.

Mhe. Balozi Kombo ameishukuru Umoja wa Ulaya kwa kuguswa na hali ya usalama katika ukanda huo na kuiomba EU kusaidia nchi zinazokumbwa na migogoro ya kivita, kwa kutoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi walioko kwenye kambi mbalimbali.

Kadhalika, Waziri ameomba Umoja wa Ulaya kuongeza juhudi zake katika kusaidia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika jitihada zao za kutafuta suluhisho la kudumu kwa migogoro ya kisiasa na kiusalama katika eneo hilo.

Pia, Mhe. Balozi Kombo amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kuendelea kushirikiana na wadau wa kimataifa katika kuimarisha juhudi za amani na usalama, kupitia mazungumzo na masuluhisho ya kidiplomasia ili kutatua changamoto zilizopo.

Naye , Bw. Borgstam ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya unaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya kisiasa na kiusalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu, hususan katika nchi zinazokumbwa na changamoto za kisiasa na kiusalama kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza mashauriano na ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika masuala ya amani na usalama kwa mustakabali wa Ukanda wa Maziwa Makuu.
 

Attachments

  • FB_IMG_1741626238381.jpg
    FB_IMG_1741626238381.jpg
    34.7 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626229491.jpg
    FB_IMG_1741626229491.jpg
    34.9 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626225137.jpg
    FB_IMG_1741626225137.jpg
    43.8 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626223171.jpg
    FB_IMG_1741626223171.jpg
    44.8 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626234177.jpg
    FB_IMG_1741626234177.jpg
    31.9 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626227066.jpg
    FB_IMG_1741626227066.jpg
    39.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626231833.jpg
    FB_IMG_1741626231833.jpg
    39.3 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626236115.jpg
    FB_IMG_1741626236115.jpg
    27.5 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1741626240338.jpg
    FB_IMG_1741626240338.jpg
    45.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom