Tanzania na Finland zasaini Hati ya Makubaliano kuendesha mashauriano ya Kisiasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Tanzania na Finland zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) kuhusu kufanya rasmi Mashauriano ya Kisiasa kati ya nchi hizo mbili. Uwekaji saini huo ulifanyika leo tarehe 09 Oktoba, 2024 jijini Helsinki na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwa niaba ya Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Elina Valtonen kwa niaba ya Serikali ya Finland.

Makubaliano hayo yanatoa fursa kwa nchi hizo kuwa na kikao cha Mashauriano ya Kisiasa kwa kupokezana kila mwaka ili kujadili na kukubaliana maeneo ya kipaumbele ya kushirikiana yenye manufaa kwa pande zote mbili.

Soma Pia: Waziri wa Mambo ya Nje, Mahmoud Thabit Kombo awasili Finland kwa ziara ya kikazi

Tukio hilo limehudhuriwa na maafisa wakuu wa pande zote mbili, akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Finland, ambaye makazi yake yako Stockholm Sweden, Mhe. Grace Olotu, Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Theresa Zitting, Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Dkt. Gift Kweka.
 
Tizama mtu mzima kakaa na vibinti eti wana sign mikataba. Mizee imo tu hadi aibu, wakiambiwa watupishe utasikia, eti sisi hatuna adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…