Tanzania na Kenya tumeweka ruzuku kwenye mafuta. Rais Museveni asema hiyo haisaidii yeye ataka Magari ya Umeme

Tupe sababu mkuu!
Kila kilomita 100 lazima ukachaji na charge kwa gari used yaweza tumia masaa mawili kuchaji hiyo gari.Hivyo mwenye nalo ahakikishe chaji ikiisha ana muda wa kwenda kushinda sehemu ya kuchaji minimum masaa mawili

Safari ndefu hayafai.Fikiria kila kilomita 100 unaenda kuchaji unakaa masaa mawili kuhubiri lijae chaji .Safari ya kwenda Mbeya kilomita 800 utahitaji njiani kila kilomita 100 uende kuchaji masaa mawili hadi kufika Mbeya utahitaji kutumia masaa 14 njiani kwenye vituo vya kuchaji tu ili safari yako ufikie Mbeya.Hivyo badala ya kutumia masaa 12 kwa gari ya petrol gari ya umeme.utatumia madaa 26. Yale 12 ya safari jumlisha 14 ya kuchaji njiani.Kwa hiyo ukiondoka Dar es salaam saa 12 asubuhi mfano leo utafika Mbeya saa mbili asubuhi Kesho. Mchana wote utakuishia njiani na usiku wote utakuishia njiani saa mbili asubuhi ndio utawasili Mbeya mjini
 
Mzee mwenzangu gari zinatofautiana Range. Iko Tesla inatembea kilometre 500 kwa single charge. Ina maana kwa vituo vya kuchaji unaweza ukatembea Dar-Iringa ukachajisha. Mfumo ukiwa wa fast charge ni ndani ya nusu saa unakuwa na 80% ya charge tayari. Unamalizia safari yako hadi Mbeya
 
Dogo kachukua betri inatembeza km 400 ila kuchaji ni masaa 6
 
Bei ya gari za Tesla umeziona?
 
Dogo kachukua betri inatembeza km 400 ila kuchaji ni masaa 6
Hamna gari hivyo kwenye za umeme zilizoko sokoni.Kwa sababu ndio kanunua .Atembelee kwanza ahakiki!! Huyo aliyemuuzia ikimzimikia porini kabla haijafika hata kilomita 200 ikamzimikia katikati ya mbuga yenye simba ndipo ataelewa hiyo chaji inatembea kilomita ngapi
 
Hivi Uganda si wanachimba mafuta?
Hadi wanajenga bomba kuuza nje mafuta kupitia Tanga,
Imekuwaje tena? Afrika tuna safari ndefu sana, tukifika tumechoka sana,
Hata huko kwa wazungu ambako teknolojia ipo juu na mafuta bei nafuu bado wanapambana na kutumia teknolojia ya umeme, wewe unaponda wazo la museven kisa uzee mh!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…