Tanzania na laana ya mikopo

Tanzania na laana ya mikopo

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Ni suala la muda tu kabla ya Tanzania kuingia katika klabu ya nchi zinazodaiwa zaidi Afrika na pia duniani (most indebted countries), sawa na DRC, Sierra Leone, Ghana, Angola....Argentina, Lebanon, Venezuela.

Tena kwa kasi hii, hilo laweza kutokea ndani ya miaka mitano ijayo. Kuwa katika kilabu hiyo hakutegeme zaidi kiasi gani unadaiwa, bali uwezo wako wa kulipa kutokana na tija yako.

Ingawaje serikali haiwaambii watu wake, inakadiriwa deni la Tanzania kupita dola bilioni 40 au zaidi ya Shillingi Trillioni 105.

Hiki ni kiasi kikubwa sana cha deni, ukizingatia kuwa katika miaka ya 90 Tanzania iliwahi kuinua mikono juu na kutaka isaidiwe wakati deni lilikuwa dola bilioni 7 tu!

Wakati huo pato letu la mwaka lilikuwa dola bilioni 60 na hivi sasa, wenye matumaini zaidi wanasema ni dola Bilioni 180. Lakini watu wameongezeka maradufu, shillingi imeshuka, kwa hiyo bado ni kama pato la 90's.

Kulipa deni jamani si mchezo, ndiyo maana Waswahili wana msemo: 'kukopa arusi (si harusi) kulipa matanga' Biafsi nilikopa kijideni fulani mwaka 95 na mpaka mwaka jana ndiyo nakimaliza!

Mwaka huu Mwigulu amepanga kulipa sh. Trilioni 13, bilioni 13 kwa madeni, kutoka kwenye bajeti nzima ya sh. Trilioni 44, bilioni 39! Hiki ni kiasi kikubwa tayari cha kulipia deni ukilinganisha kuwa bajeti yetu yoooote ya elimu ni Trillioni 1 bilioni 67. Kwa mwenye akili atauliza kama namna hii tutafikia maendeleo.

Kibaya zaidi, hivi niandikavyo, mikopo ndyo inazidi kuchukuliwa.

Niweke wazi hili: kukopa per se siyo kitu kibaya, na kwa kweli kutokana na mfumo wa dunia, ni lazima serikali ikope, kiasi kwamba usipokopa nchi inaweza kutiwa katika msukosuko na 'mabeberu' wanaoishi juu ya riba za mikopo na hata kupinduliwa. Ukisikia kwa nini Marekai na washirika wanazichukia sana Iran, Cuba na Libya ya Gaddafi, moja ya sababu ni kuwa nchi hizo aidha zilikataa kukopa au zilikopa kidogo sana.

Ninachopinga ni kuwa mikopo mingi ya Tanzania haifuati nidhamu za udhibiti na ulinzi wa fedha, wala haiangalii wala kupanga kuzalisha zaidi kufidia.

Mara nyingi serikali inachukua mkopo kwa mihemuko ya jazba bila hata kujali masharti na riba za mkopo huo. Hata katika maisha ya mtu binafsi, unapochukua mkopo bila ya mipango utapata shida sana na pengine kufilisiwa. Unapochukua mkopo kwa uchache ni lazima ujue:

1- Ni kwa jambo gani?
2-Jee, unachokichukulia mkopo kitaweza kuzalisha na kuurudisha?
3-Kwa muda gani, kwa riba ipi
4- Hilo jambo unalolichukulia mkopo haliwezi kusubiri hadi upate fedha kutokana na uzalishaji wako mwenyewe?

Nikitazama, sioni maswali haya yanajibiwa katika wimbi la mikopo inayochukuliwa hivi sasa. Kibaya zaidi madeni yana athiri thamani ya fedha na thamani ya fedha inaposhuka ndiyo utalipa zaidi, hasa madeni haya yanayochukuliwa kwa fedha za kigeni.

Katika hali nyingi, serikali yetu inachukua madeni kwa sababu ya uvivu wa kufikiria kwa Mawaziri wa Uchumi, kwa hiyo wanaona rahisi kuomba. Ukiongeza na ufisadi na rushwa, nadhani pia kuna imani kwamba tukizidiwa tutaomba tupunguziwe na 'wajomba zetu'. Lakini dunia inakoelekea ni dhahiri haitakuwa kama miaka ya 90.

Hivyo, Watanzania tujiandae kuja kuamka siku moja na kustukia mali zetu zote, yakiwemo madini mbali mbali, mafuta yatakayogunduliwa, gesi, Hellium, misitu na hata wanyama wetu wamekwisha uzwa, nasi tumeambukia madege ya Air Tanzania ambayo hatutaweza hata kuyarusha!

====

Pia soma:

- Ghamara za kulipa Deni la Serikali zimepanda kufikia Tsh. Trilioni 13.13 kutoka Tsh. Trilioni 10.48

- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
 
Ni hatari kubwa sana, watu watakuja kukamuliwa kodi mapaka wanyooke
 
Ni suala la muda tu kabla ya Tanzania kuingia katika klabu ya nchi zinazodaiwa zaidi Afrika na pia duniani (most indebted countries), sawa na DRC, Sierra Leone, Ghana, Angola....Argentina, Lebanon, Venezuela...
Tena kwa kasi hii, hilo laweza kutokea ndani ya miaka mitano ijayo. Kuwa katika kilabu hiyo hakutegeme zaidi kiasi gani unadaiwa, bali uwezo wako wa kulipa kutokana na tija yako.
Ingawaje serikali haiwaambii watu wake, inakadiriwa deni la Tanzania kupita dola bilioni 40 au zaidi ya Shillingi Trillioni 105. Hiki ni kiasi kikubwa sana cha deni, ukizingatia kuwa katika miaka ya 90 Tanzania iliwahi kuinua mikono juu na kutaka isaidiwe wakati deni lilikuwa dola bilioni 7 tu! Wakati huo pato letu la mwaka lilikuwa dola bilioni 60 na hivi sasa, wenye matumaini zaidi wanasema ni dola Bilioni 180. Lakini watu wameongezeka maradufu, shillingi imeshuka, kwa hiyo bado ni kama pato la 90's.
Kulipa deni jamani si mchezo, ndiyo maana Waswahili wana msemo: 'kukopa arusi (si harusi) kulipa matanga' Biafsi nilikopa kijideni fulani mwaka 95 na mpaka mwaka jana ndiyo nakimaliza!
Mwaka huu Mwigulu amepanga kulipa sh. Trilioni 13, bilioni 13 kwa madeni, kutoka kwenye bajeti nzima ya sh. Trilioni 44, bilioni 39! Hiki ni kiasi kikubwa tayari cha kulipia deni ukilinganisha kuwa bajeti yetu yoooote ya elimu ni Trillioni 1 bilioni 67. Kwa mwenye akili atauliza kama namna hii tutafikia maendeleo.
Kibaya zaidi, hivi niandikavyo, mikopo ndyo inazidi kuchukuliwa.
Niweke wazi hili: kukopa per se siyo kitu kibaya, na kwa kweli kutokana na mfumo wa dunia, ni lazima serikali ikope, kiasi kwamba usipokopa nchi inaweza kutiwa katika msukosuko na 'mabeberu' wanaoishi juu ya riba za mikopo na hata kupinduliwa. Ukisikia kwa nini Marekai na washirika wanazichukia sana Iran, Cuba na Libya ya Gaddafi, moja ya sababu ni kuwa nchi hizo aidha zilikataa kukopa au zilikopa kidogo sana.
Ninachopinga ni kuwa mikopo mingi ya Tanzania haifuati nidhamu za udhibiti na ulinzi wa fedha, wala haiangalii wala kupanga kuzalisha zaidi kufidia. Mara nyingi serikali inachukua mkopo kwa mihemuko ya jazba bila hata kujali masharti na riba za mkopo huo. Hata katika maisha ya mtu binafsi, unapochukua mkopo bila ya mipango utapata shida sana na pengine kufilisiwa. Unapochukua mkopo kwa uchache ni lazima ujue:
1- ni kwa jambo gani?
2-Jee, unachokichukulia mkopo kitaweza kuzalisha na kuurudisha?
3-Kwa muda gani, kwa riba ipi
4- Hilo jambo unalolichukulia mkopo haliwezi kusubiri hadi upate fedha kutokana na uzalishaji wako mwenyewe?
Nikitazama, sioni maswali haya yanajibiwa katika wimbi la mikopo inayochukuliwa hivi sasa. Kibaya zaidi madeni yana athiri thamani ya fedha na thamani ya fedha inaposhuka ndiyo utalipa zaidi, hasa madeni haya yanayochukuliwa kwa fedha za kigeni.
Katika hali nyingi, serikali yetu inachukua madeni kwa sababu ya uvivu wa kufikiria kwa Mawaziri wa Uchumi, kwa hiyo wanaona rahisi kuomba. Ukiongeza na ufisadi na rushwa, nadhani pia kuna imani kwamba tukizidiwa tutaomba tupunguziwe na 'wajomba zetu'. Lakini dunia inakoelekea ni dhahiri haitakuwa kama miaka ya 90.
Hivyo, Watanzania tujiandae kuja kuamka siku moja na kustukia mali zetu zote, yakiwemo madini mbali mbali, mafuta yatakayogunduliwa, gesi, Hellium, misitu na hata wanyama wetu wamekwisha uzwa, nasi tumeambukia madege ya Air Tanzania ambayo hatutaweza hata kuyarusha!!
Ndugai hakueleweka, akapoteza na Uspika wa Bunge,
Nchemba anakwambia deni ni Himilivu, na bado tunakopesheka,
 
Naamini huko mbeleni tutakuwa na wakati mgumu sana.
 
Serikali iliingia deni likiwa trillion 70 saiv trillion 105? Mkuu
 
Marekebisho hapo uchumi wetu ni USD 79B (2024) sio 180B.
Nilisema: 'wenye matumaini zaidi'. Kutokana na usiri mkubwa na hata kuzuga wakati mwingine kunakofanywa na Waziri mwenye mamlaka imekuwa vigumu kupata rekodi sahihi. Hili ni sual ambalo nchi za wenzetu ni kuvuta simu tu na kumpigia ofisa, wala si Waziri, mhusika wa Idara, atakuambia kwa ukweli na uaminifu. After all, ni faida kwa nchi kusema ukweli katika suala hili. Ila kwetu linatumika kisiasa kumfanya Waziri au rais aonekane afanya vizuri! Pammmmmmmmmmmmmbaf!
Google utaona mkanganyiko mkubwa ulioko! Kuna wengine hadi sasa wanaweka GDP ya Tanzania ni 65 billion. Nimeona mkuu!
 
Ni suala la muda tu kabla ya Tanzania kuingia katika klabu ya nchi zinazodaiwa zaidi Afrika na pia duniani (most indebted countries), sawa na DRC, Sierra Leone, Ghana, Angola....Argentina, Lebanon, Venezuela.

Tena kwa kasi hii, hilo laweza kutokea ndani ya miaka mitano ijayo. Kuwa katika kilabu hiyo hakutegeme zaidi kiasi gani unadaiwa, bali uwezo wako wa kulipa kutokana na tija yako.

Ingawaje serikali haiwaambii watu wake, inakadiriwa deni la Tanzania kupita dola bilioni 40 au zaidi ya Shillingi Trillioni 105.

Hiki ni kiasi kikubwa sana cha deni, ukizingatia kuwa katika miaka ya 90 Tanzania iliwahi kuinua mikono juu na kutaka isaidiwe wakati deni lilikuwa dola bilioni 7 tu!

Wakati huo pato letu la mwaka lilikuwa dola bilioni 60 na hivi sasa, wenye matumaini zaidi wanasema ni dola Bilioni 180. Lakini watu wameongezeka maradufu, shillingi imeshuka, kwa hiyo bado ni kama pato la 90's.

Kulipa deni jamani si mchezo, ndiyo maana Waswahili wana msemo: 'kukopa arusi (si harusi) kulipa matanga' Biafsi nilikopa kijideni fulani mwaka 95 na mpaka mwaka jana ndiyo nakimaliza!

Mwaka huu Mwigulu amepanga kulipa sh. Trilioni 13, bilioni 13 kwa madeni, kutoka kwenye bajeti nzima ya sh. Trilioni 44, bilioni 39! Hiki ni kiasi kikubwa tayari cha kulipia deni ukilinganisha kuwa bajeti yetu yoooote ya elimu ni Trillioni 1 bilioni 67. Kwa mwenye akili atauliza kama namna hii tutafikia maendeleo.

Kibaya zaidi, hivi niandikavyo, mikopo ndyo inazidi kuchukuliwa.

Niweke wazi hili: kukopa per se siyo kitu kibaya, na kwa kweli kutokana na mfumo wa dunia, ni lazima serikali ikope, kiasi kwamba usipokopa nchi inaweza kutiwa katika msukosuko na 'mabeberu' wanaoishi juu ya riba za mikopo na hata kupinduliwa. Ukisikia kwa nini Marekai na washirika wanazichukia sana Iran, Cuba na Libya ya Gaddafi, moja ya sababu ni kuwa nchi hizo aidha zilikataa kukopa au zilikopa kidogo sana.

Ninachopinga ni kuwa mikopo mingi ya Tanzania haifuati nidhamu za udhibiti na ulinzi wa fedha, wala haiangalii wala kupanga kuzalisha zaidi kufidia.

Mara nyingi serikali inachukua mkopo kwa mihemuko ya jazba bila hata kujali masharti na riba za mkopo huo. Hata katika maisha ya mtu binafsi, unapochukua mkopo bila ya mipango utapata shida sana na pengine kufilisiwa. Unapochukua mkopo kwa uchache ni lazima ujue:

1- Ni kwa jambo gani?
2-Jee, unachokichukulia mkopo kitaweza kuzalisha na kuurudisha?
3-Kwa muda gani, kwa riba ipi
4- Hilo jambo unalolichukulia mkopo haliwezi kusubiri hadi upate fedha kutokana na uzalishaji wako mwenyewe?

Nikitazama, sioni maswali haya yanajibiwa katika wimbi la mikopo inayochukuliwa hivi sasa. Kibaya zaidi madeni yana athiri thamani ya fedha na thamani ya fedha inaposhuka ndiyo utalipa zaidi, hasa madeni haya yanayochukuliwa kwa fedha za kigeni.

Katika hali nyingi, serikali yetu inachukua madeni kwa sababu ya uvivu wa kufikiria kwa Mawaziri wa Uchumi, kwa hiyo wanaona rahisi kuomba. Ukiongeza na ufisadi na rushwa, nadhani pia kuna imani kwamba tukizidiwa tutaomba tupunguziwe na 'wajomba zetu'. Lakini dunia inakoelekea ni dhahiri haitakuwa kama miaka ya 90.

Hivyo, Watanzania tujiandae kuja kuamka siku moja na kustukia mali zetu zote, yakiwemo madini mbali mbali, mafuta yatakayogunduliwa, gesi, Hellium, misitu na hata wanyama wetu wamekwisha uzwa, nasi tumeambukia madege ya Air Tanzania ambayo hatutaweza hata kuyarusha!
tena wa pesa x
 
Kibaya kinachonifanya nibubujikwe na machozi ni hela hizo kutofanya mambo ya maana isipokuwa ni kuibwa,posho,mashangingi na ujingaujinga mwingine nadhani moja ya mambo yanayoyafanya Mataifa kama China kuendelea ni sheri zake kali kwa watu wapumabvu wanaoendekeza maufisadi
 
Serikali iliingia deni likiwa trillion 70 saiv trillion 105? Mkuu
Chukua takwimu zangu, achana na Trab na Trat! Si unaona shilingi iinavyo slide, dola haipatikani, kodi,tozo vimeshamiri...,.wangefanya hivyo ingekuwa deni leto ni 70 T pekee? Hujiulizi nini kinachosababisha taharuki yote hii ya kuchukua mikopo? Moja ni 'kumkopa Paulo ili kumlipa John' ! Ya kuambiwa changanya na zakoooo!
These guys have messed us up big time. Not only you but perhaps your grand children. I wish Tanzania were like Kenya, Burkina Faso or Mali! Anyway, as you're stoic, prepare to die with 'tai shingoni'!
 
Mbaya zaid pamoja na mikopo yote hiyo ila maisha yanazidi kuwa magumu kwa wananchi pia kuongezeka kwa Kodi na tozo Kila sehemu sasa unabaki unaniuliza hizo pesa wanazifanyia nini kama sio kula viongozi na familia zao?
 
Back
Top Bottom