kuanzia awamu ya pili hadi ya nne wamezembea na kuachia mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa Nyerere kwa kujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima yapotee bure sasa hivi tumerudi nyuma zaidi kuliko hata tulipokuwa 1970.
Son:
Unaboronga hapa. Jibu ni lilelile sahihi. Elimu ilikuwa kwa kutumia misaada. Na wahisani walipobadilisha sera zao, tumejamba.
Ilikuwa ni mipango ambayo haiko-sustained na rasimali zetu wenyewe (period, koniec, end of story).
Z10
sasa ilikuwaje Nyerere aliweza kuwashawishi wafadhili au wafadhili kushawishika na sera za nyerere kuhusu "kufuta ujinga" kiasi kwamba walioko madarakani leo hii wameshindwa kufanya hivyo?
Kwanini wakati wa Mwalimu tuliweeza kufikia 90% ya watu wetu kujua kusoma na kuandika lakini leo tuko kwenye 69%? .
So, ni kitu gani kina Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanakikosea ambacho Nyerere alikifanya sahii kwenye kufuta ujinga?
Mwanakijiji:
Mafanikio kwenye afya, elimu yalionekana lakini uchumi haukukua. Hivyo hatukuweza ku-sustain huduma za jamii.
1985 wakati anang'atuka tayari stats za elimu zishaanza kuporomoka. Literacy rate ya 90% ilifikiwa mwishoni mwa 70. Na 1985 ilikuwa kwenye 75%.
Kumbukumbu:
Sasa sijui hicho nikiite nini. Kimsingi umesema wasilaumiwe waliomfuata bali Nyerere kwa vile "hakuacha kitu kinachojitegemea"!
Hii nadharia wahisani waliicha lini? Ni lini wahisani walibadili mipango ya kusaidia elimu, afya na maji?
Ina maana Nyerere na wahisani waliweza kuleta mafanikio katika afya na elimu lakini AHM, BWM, na JMK na wahisani wao wamefeli katika elimu lakini uchumi umekua!
Hili ni dai ambalo nitafurahi kuona ushahidi wake.
Ina maana hata wakati anaondoka bado literacy ilikuwa juu kuliko miaka ishirini ya kusamehewa madeni, soko huru n.k n.k. Nyerere then was a genius linapokuja suala la literacy!
Wakuu,
haya pia ni matokeo ya SAPs za miaka ya 80 ambapo masharti yaliyowekwa na Brettonwood Institutions ( IMF na World Bank)kama njia ya kufufua uchumi yakawa ni kuondoa ruzuku katika huduma za jamii - wananchi wakalazimika kuchangia elimu iliyokuwa inatolewa bure, afya n.k.Wananchi nao hawakuwa wameandalia/wamejiandaa kupokea hali hiyo.Unapopata elimu bure, ni rahisi sana kupeleka watoto shule wakapata anagalau kujua kusoma na kuandika.Inapokuwa kuchangia hadithi inakuwa tofauti na ndiyo maana illiteracy inaongeza kwakiwango cha juu.
Tusisahau pia kuwa Nyerere kwa miaka yote alikua anakataa kukubali dawa hiyo ya IMF/World Bank na hata kuna kipindi wakatofautiana na aliyekuwa Governor wa Benki kuu wa wakati ule - Edwin Mtei.
Wakati wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi- miaka ya katikati ya 80,sera zilibadilika kukawepo na mageuzi makubwa ya kiuchumi ( economic liberalisation) ndipo uchungu wa dawa hiyo ulipoanza kutafuna sekta zote za huduma za jamii.
WomanofSubstance,
..hakuna mtu aliyetushikia kiboko kwenda kuomba msaada wa IMF.
..tulishindwa kujiendesha, tukawafuata IMF na WB, nao waka-prescribe kidonge vya SAP.
NB:
..mpango wa shule za sekondari za kata unarudia makosa yaliyofanyika wakati wa UPE.
..unajua at least Mwalimu tunaweza kumtetea kwamba yeye alikuwa ni mwanzilishi, hakuwa na waliomtangulia ambao angeweza kujifunza toka kwao.
..mpango wa sekondari za kata ukifeli sijui tutakuwa na maelezo na visingizio gani.
Hoja yangu hapa ni deeper; kama kwenye taifa ambalo ujinga umeongezeka lakini linajiona tajiri ja yawezekana Nyerere hakufanya sahihi kufuta ujinga na watu wakawa maskini? Je watu wenye hela mifukoni, Tv, magari, mitumba, internet n.k lakini hawana elimu ya kujua kusoma na kuandika, wanaona umuhimu gani wa kuwa na elimu?
Kama kujua kusoma na kuandika kulituacha tuwe na umaskini chini ya Nyerere, kutokujua kwetu kusoma chini ya kina Mkapa, Mwinyi na sasa JK kunatuletea "utajiri" kuna umuhimu gani wa kujua kusoma?
Yawezekana ndiyo sababu baadhi ya wizi unatokea wakati huu zaidi kuliko wakati wa Mwalimu?
About 40 per cent of children on average don`t continue with education despite doing well in their examinations..
WomanofSubstance,
..hakuna mtu aliyetushikia kiboko kwenda kuomba msaada wa IMF.
..tulishindwa kujiendesha, tukawafuata IMF na WB, nao waka-prescribe kidonge vya SAP.
NB:
..mpango wa shule za sekondari za kata unarudia makosa yaliyofanyika wakati wa UPE.
..unajua at least Mwalimu tunaweza kumtetea kwamba yeye alikuwa ni mwanzilishi, hakuwa na waliomtangulia ambao angeweza kujifunza toka kwao.
..mpango wa sekondari za kata ukifeli sijui tutakuwa na maelezo na visingizio gani.
mimi ninawasikia vizuri sana mnayosema yaliyotokea wakati wa Mwalimu, swali langu ni how can you explain kinachotokea leo hii? Tunapokea misaada zaidi sasa hivi, tumesamehewa madeni tangu 2000, leo hii bado literacy imeshuka hadi 69%. Nyerere ametoka madarakani 1985. Baada yake wamepita marais wa wawili na sasa yupo watatu.
Kwanini, literacy bado iko chini? Kulaumu misaada sidhani kama inaelezea kwani baada ya Mwalimu kuondoka misaada ndiyo iikatiririka kwa kila aina ni mingi mno. Kwanini haielekezwi kwenye kukuza kujua kusoma na kuandika? Tumejenga shule nyingi wakati huu, tuna vyuo vikuu vingi, tuna magazeti, tv, internet, n.k Kwanini literacy bado iko chini.
Jibu lenu ni misaada na Nyerere! Really?
Kuhusu suala lako la kuwepo vyuo, TV na bado kuwa na literacy ya 69%. Kuna mambo mengi ya kuangalia. Mojawapo ni kushindwa kwa sera ya vijiji vya ujamaa.
Mara nyingi tuna-overlook muundo wa vijiji vya ujamaa kusaidia kukuza literacy rate.
Sehemu fulani ya kupungua kwa literacy imesababisha na attendance mbovu ya wanafunzi.
Wakati wa vijiji vya Ujamaa, ilikuwa rahisi kufuatilia jinsi watoto wanavyokwenda shuleni. Nakumbuka baadhi ya wazazi walipelekwa jela kwa kushindwa kupeleka watoto shule.
Sasa hivi kuna watu wamerudia maisha kwenye vijiji vyao vya zamani. Ni nani atakayemlazimisha mtoto anayeishi huko kwenda shule?
Nadhani hii topic tulishaijadili na ZAKUMI NA WoS somewhere here on JF.
Nadhani swala hapa tujiulize, hiyo 90% ya wasomi aliowaacha Nyerere..ilifanya nini kuendeleza elimu? Kwa lugha nyingine kama mtu alikuwa anajua kusoma na kuandika ingekuwa rahisi kumpeleka mtoto shule. Sasa kama watu hawakupelekwa shule perhaps tatizo siyo ujinga wa kutoelewa maana na umuhimu wa elimu bali ni kukosekana kwa uwezo au ni kwamba hataki kumpeleka mtoto shule. Just thinking.
Zakumi, Mwanakijiji et al..hapa tusiwe apologetic. Ukweli ni kwamba elimu yetu Tanzania imezorota sana. Na wala hapa wa kulaumu siyo Nyerere, WB, IMF wala wahisani. Ni sisi kama taifa. Elimu HATUKUIPA na HATUIPI kipaumbele stahiki yake. Mpaka leo angalia bajeti ya elimu ni kiasi gani (% kubwa inaishia kulipa mishahara ya walimu), tujiulize tunawekeza kiasi gani katika utafiti? Tujiulize..serikali inatoa support kwa raia wa ngapi kila mwaka kwenda kwenye "cutting age institutions" kupata ujuzi? JAMANI hapa ukweli ni kwamba Nyerere alifanikiwa kwa sababu Elimu aliipa kipaumbele. Nukta. Huduma za msingi zilifanikiwa-(mpaka kwetu tukawa na matank ya maji) kwa sababu hizi huduma zilipewa kipaumbele. Simply say..we invested in these critical areas. Na wala siyo swala la wahisani wala nini. KAMA alivyosema Mwanakijiji leo tunapokea misaada mingi sana. Kama tungeamua kuwa na vipaumbele na kuwekeza hizo pesa, hakika..tusingeulizana haya maswali hapa.
Leo serikali iikisema kwamba elimu inapewa priority stahiki. I can assure you..hizi statistics zitabadilika ghafla. Na tunarudi kwa waungwana hapa ambao wamekuwa wakisisitiza kwamba Serikali yetu haina vipaumbele. Huwezi tegemea tuwe na takwimu safi wakati tunawekeza zaidi katika kununua mashangingi, rada, ndege ya raisi, kuiba EPA, mikataba mibovu na kukarabati ikulu kila mwaka. Where are our priorities? Kwa umri wangu na uelewa wangu huu..sijawahi kuona nchi inayoendelea bila kuwa na vipaumbele. We simply lack priorities which reflect our needs. na tunapokuwa na hivyo vipaumbele...ni kama usiku na mchana..maana ha-reflect matatizo yetu.
All in all, sisi kama taifa ndo wa kurudi kwenye drawing board. Tujiulize vipaumbele vyetu ni vipi. Leo tunaongelea MDGs kwamba ndo vipaumbele vyetu. Lakini naomba niwe tofauti na wengi humu na kwingineko. attainment za hizi MDGs si rahisi kutuondolea umasikini. Precisely because, hizi ni priorities zilizo tungwa New York na akina Jeffrey Sachs..akina Kikwete wakaenda kusaini tuu. Sidhani kama tungekaa chini..tusingekuja na vipaumbele vinavyo reflect mazingira yetu. Na asikudanganye mtu..mataifa 190 na ushee..hatuwezi kuwa na goals zinazofanana..wote tuna matatizo..lakini yanatofautiana...Huwezi kuniambia mahitaji ya elimu Burundi ni sawa na New Zealand..ingawa hawa viongozi wote wali-endorse hizo MDGs..ni usanii mtupu. Na kibaya zaidi..wanataka tu-achieve hizi MDGs wakati pesa hakuna..perhaps tungekuwa na za kwetu..ingekuwa rahisi kujiwekea realistic budget...I will be pleasantly surprised kama hizi MDGs zitatuondolea matatizo katika nyanja husika.
Hivyo basi, mchawi siyo Nyerere wala IMF. Ni sisi tunavyopanga mipango yetu. Nadani tufike point tuache kutafuta mchawi kwa makosa yetu wenyewe. Next month ni bajeti..mtaniambia elimu tumeipa kiasi gani na ukarabati wa Ikulu tumetenga ngapi. Thats our state of affairs. Sad but true.
Kusema kwamba Nyerere anahusika na hii current state of our education "we are just losing both of our moral and intellectual bearing.
................Hivyo mtu akileta mada kuhusu mafanikio yaliopatikana wakati wa Nyerere ni lazima tueleze makosa. Kwa sababu kama mafanikio hayo hayakuwa ya nguvu za gas basi yangeendelea kuwepo........
..If you don't learn from your past mistakes, you are likely to repeat them. Ndugu yangu Jokakuu na mimi tunamwita Nyerere pioneer au Mwanzilishi. Likehood ya pioneer ku-introduce failure ni kubwa sana kuliko wanaomfuatia.
Mkuu wangu nchi kama China walikuwa ranked chini ya 50 after the collapse of Cold war, Russia ilikuwa nchi ya 40 kiuchumi baada ya kuvunjika kwa USSR na kuundwa kwa Russia federation, leo hii Russia ni nchi ya 7 na China inakimbilia kuwa Super power, tena basi wote hawa bado kabisa wanatukuza mazuri yote yaliyotokana na Uongozi uliotangulia badala ya mabaya ya viongozi kwa sababu wamepata jawabu na mbinu za kujiendeleza sio kutokana na kuchunguza mabaya.
Mkuu wangu tunapojifunza kutokana na makosa yaliyopita ni muhimu sana kufahamu jawabu la makosa yale na sio kuyasoma makosa yenyewe ili upate jawabu kutokana na makosa yenyewe..Mfano 2+2=5, ni makosa na huwezi kujifunza lolote kutokana na maandishi haya zaidi ya kutafuta mbinu zinazotakiwa upate jawabu lililokuwa sawa na utarudi tu kutazama makosa uiloyafanya baada ya kufahamu kwa nini 2+2=4..
Bob, hili ndo somo ambalo watanganyika hatujawahi kubahatika kulielewa.
Tuzidi kupambana iko siku kitaeleweka.
Its completely unfair kulaumu ujamaa kwa failure katika sector ya elimu tuliyonayo leo. Kwa hiyo sasa tuseme hata huduma za hospitali na maji...mbona wakati huo wa ujamaa maji yalikuwa yanafika vijijini? kipi kimefanya maji yakakauka kwenye mabomba? After all mabomba yalikuwepo tayari...sasa sjui tutalaumu Nyerere..wakati alishafanya kazi kubwa ya kuunganisha mabomba..kitu ambacho sisi tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha maji yanazidi ku-flow. Hilo tuu. Hapana, kama anavyosema Bob Tatizo tunalo sisi wenyewe. Hainingii akilini leo Kikwete anashindwa kushughulikia tatizo la umeme..anabaki analaumu mikataba ya IPTL na mengineyo..wakati angeangalia ni wapi kosa lilipofanyika..na kurekebisha hiyo mikataba.
The 69% is simple logic! There is no connection between academic achievement and anything! Being a bright child in school does not provide you a scholarship! Finishing on top of your class does not provide you a job! Doing research does not give you a voice! There are no awards for outstanding students! No celebration for intellegence!
In short the system of reward and punishment in education is not working. Going to school is a procedure which finds no significancy attachment between academic and chances of success! You could get a job even if you flank your exams. You became a ministry of natural resources even if you have studied art! Specialization is not full respected. Where there is a country crisis, political commitee hold more power more than field experties! what do we expect!
Nchi inaenda kimishemishe tu! So, why should one toil while there are other avenues for success! Until we find that link between education and people well being, until we make education as a main avenue for success, center for development plan and the only route for addressing inequalities the literacy rate will keep falling down.