Womnaofsubstance,
Hapa bibie nashindwa kukubaliana nanyi katika hili..
Mikopo inayopatikana ni lazima tuitumie kwa makini ktk maswala muhimu na sio swala kuweka ktk la uzalishaji tu.. Uzalishaji ni kujumu letu wenyewe wananchi kwa sababu misingi ya uzalishaji ilijengwa pia na itaendelea kujengwa ikiwa tutakuwa makini kupanga priorities zetu..
Ndio tofauti kubwa na Nyerere na viongozi hawa wengine kwani wao wanapangiwa wapi twende wakati sisi hatufahamu tunataka kwenda wapi au huko wanakotupeleka.Tunachoamini ni kwamba lazima huko mbele kuna pepo wakati hatuna mfano hata mmoja wa mtu aliyefanikiwa kwa misaada unayopangiwa masharti..
Mwalimu aliwekesha katika ELIMU, AFYA, MAJI na UMEME, huwezi kunambia hiyo ni sawa na kununua fanicha na kibaya zaidi wengi mnajaribu kupima mwanzo wa mikakati hii miaka ya 70 na 80 ktk mazingira ya leo..Nilikwisha sema hata gari mathlan Mercedes Benz ya mwaka 70 ya 80 ilikuwa tofauti na leo hii hivyo mapungufu ya gari lile wakati ule huwezi kuyalinganisha na gari la leo ili kujenga hoja..
Mbali na yote hayo ni mashirika mangapi ya Umma yalijengwa wakati wa mwalimu pamoja na kwamba mfumo wa siasa haukuwa bora..Ni mashirika mangapi leo hii tumeuza hadi kupanua mfumo wa serikali na kudai mafanikio makubwa ati wakati wa Mkapa mfuko wa hazina ulikuwa umetuna wakati tumeshindwa kuelewa kuwa mavuno yake hayakuzalishwa isipokuwa tumeuza title ya mirathi..
Matatizo ya mikopo yanajulikana dunia nzima kwamba IMF na WB ni vyombo ambavyo vinachota riba kubwa na masharti yake kwa nchi maskini ni magumu sana kuweza kuleta mabadiliko yoyote yake. Ni vyombo ambavyo vinaendeshwa na mashirika makubwa acha mbali nchi tajiri na mara zote wanahakikisha kuwa uti wa mgongo wa uzalishaji wa nchi husika hukamatwa na nchi hizi ikiwa ni pamoja na Mawasiliano, Umeme, Maji, Banks na mengineyo muhimu..
Nyerere alikuwa akikopa fedha nchi tofauti zenye nia ya kuleta m,aendeleo nchini hata kama nchi yenyewe ina mapungufu yake.. Haijalishi fedha kama zinatoka Arabuni, Israel, Nordic, Iran Marekani, Uholanzi au hata hiyo IMF ili tupate kufikia malengo tuliyoweka, na umuhimu wa mikopo hiyo ni lazima kutazama ni vitu gani tuli invest pamoja na kwamba hali yetu ilikuwa duni zaidi..
Leo hii ndugu zangu ikiwa hata Elimu tunaambiwa kwamba:-
About 40 per cent of children on average don`t continue with education despite doing well in their examinations..
Bado tunatafuta mchawi?..Hivi kweli serikali haiwezi kuweka sheria kwamba hata wale wanaoingia shule za kulipia (Private) shule hizi wanalazimika kuchukua wale wananfunzi ambao wameshinda mtihani isipokuwa wamekosa nafasi za kuendelea mbele ktk shule za serikali..Kwa nini tuna treat ELIMU kama ni biashara badala ya elimisha watu kwa mategemeo ya kupata wataalam walioelimika hivyo kurahisisha maendeleo ya nchi!.
I mean jamani hivi kweli bado mnamhitaji Nyerere kuja kuwaambia kwamba ni Ujinga mkubwa kuona mtu aloshindwa mtihani wa darasa la saba kwa mlolongo wa D na F anaingia sekondary na hata Chuo kikuu kuliko yule aliyeshinda vizuri lakini hana uwezo kifedha..Na kibaya zaidi ktk stage zote za ELIMU nchini mwisho wa yote ni asilimia zaidi ya 70 waliohitimu ni kutokana na uwezo wao kifedha badala ya uwezo wao kieleimu!..
Hivi kweli tuna unda Taifa la aina gani kwa kizazi kijacho?..
Bibie mikopo sio dhambi wala sio kitu kisichokubalika isipokuwa ni mikopo ya aina gani inayozungumziwa.
Mara zote ni mikopo ya IMF ambayo haina tofauti kabisa na Credit card na ndio maana watu wanagomba na hizo stategies zinazoambatana na SAP.. lakini hakuna mtu wala nchi iliyoanza kimaendeleo pasipo mikopo inayolenga uwekezaji ktk kile ulichokusudia kukiendeleza...Hata Malaysia na Vietnam waliokuwa nyuma yetu walikopa kwanza kabla hawajatupa magongo hayo ya mikopo...Leo hii wako mbele yetu na wanatucheka kuona bado tunategemea mikopo..
Hivyo swala sio kukopa isipokuwa utaweza vipi kuondokana na mikopo ikiwa wewe mwenyewe hujandai kuondokana nayo!.. ndivyo mataifa yote hufanya hata sisi watu bianfsi wenye vibiashara vyetu mbuzi tunajipanga kuopndokana na mikopo sio swala la kuwa niliwahi kukopa fedha benk kuwa sababu ya Ku fail kwangu..
Maendeleo ni pamoja na kuwa na wasomi wengi na kingozi yeyote anayekoip[a ili kuendeleza elimu nchini sii ujinga hata kidogo..sio lazima kutunisha mfuko wa Hazina uwe ndio manufaa ya mikopo..wakati tuna watu kama Rostam.. Huwezi kuiba ELIMU ya wananchi wako, elimu yao ni mhuri kifuani, haitoki na kwa kuelemika huko ndipo unaweza kuendeleza nchi..