Tanzania na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zimejipangaje kudhibiti madhara ya ndege zisizo na rubani endapo zitapotea njia na kuja ukanda huu?

Tanzania na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zimejipangaje kudhibiti madhara ya ndege zisizo na rubani endapo zitapotea njia na kuja ukanda huu?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Iran ameingia vitani na Israel kwa kurusha ndege zisizo na rubani zaidi ya 50. Pamoja na kuwa tupo mbali upo wakati vyombo na silaha za kivita ukosea target au ulazimishwa kuelekea uelekeo usio sahihi.

Natambua hapo katikati kutoka Iran hadi Afrika Mashariki kuna Mataifa Mengi lakini mengi yao hayana utulivu wa kijeshi kukabiliana na madhara ya vita.

Ningependa kufahamu ni kwa namna gani Tanzania na nchi za Afrika Mashariki zimejianda kukabiliana na madhara ya vita hii? Tupo kimya au tumejiandaa?

Eneo la pili, Vita hii inaweza pia ikaathiri usafiri wa meli katika bahari ya hindi; je serikali itaendelea na matumizi makubwa iliyonayo kwa sasa ya kuandaa matamasha na Chawa kulipwa kodi zetu au wamejiandaa kukata matumizi?

Eneo la tatu; vita hii inakwenda kutingisha uchumi wa Marekani na Mataifa mengine duniani ikiwemo IMF; je tumejiandaaje kipindi cha bajeti kupunguza matarajio ya utegemezi kwa misaada ya kimataifa?

Inshort vita hii ni sawa na COVID , je yapo wapi maandalizi ya kimkakati kwa miaka miwili au mitatu mbele?
 
Swali zuri, lakini haya ni mambo ya kijeshi, hivyo wewe kama raia timiza wajibu wako mambo ya ngoshwe Waachie wenyewe kina Ngengemkeni.
 
Acha woga, ndege badala kudondoka Israel ijie idondoke Tanzania...madhara mengine tujiandae hasa ya kiuchumi . ..wanaosimama uchumi wako na vita ya uraisi 2025. Hayo ya uchumi mtajijua wenyewe saiv wanajadili umbea wa usaliti
 
Back
Top Bottom