Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Tanzania na Qatar kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kimkakati
Tanzania na Qatar zinakusudia kuimarisha ushirikiano katika maeneo muhimu, ili kukuza biashara na uwekezaji kwa misingi ya amani, usalama, na maendeleo endelevu ya wananchi wa pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ameyasema hayo 30 Julai, 2025 katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi.
Mazungumzo yao yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, ikiwemo kusainiwa kwa Hati za Makubaliano katika sekta mbalimbali ikiwemo Biashara na Uwekezaji.
Kwa upande wake, Balozi Al Marekhi, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano mzuri na kusisitiza kuwa, Qatar inathamini uhusiano huo wa kirafiki, huku akimkaribisha Waziri Kombo kufanya ziara nchini Qatar ili kuendeleza na kutekeleza yale yaliyojadiliwa kwa maslahi mapana ya Tanzania na Qatar.