Tanzania na Qatar watia saini hati za makubaliano kuimarisha biashara na uwekezaji

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania, Zanzibar na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Kwa upande wa Chemba ya Biashara ya Tanzania, mkataba ulisainiwa na Rais wa Chemba hiyo Paul Koyi, huku pia ukisainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour.

Aidha, kwa upande wa Qatar mkataba huo umesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya nchi hiyo Muhammed bin Ahmed Al Kuwari uliofanyika Jijini Doha.

Lengo la Mkataba huo ni kuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Qatar hususan kwenye sekta za utalii, miundombinu, ujenzi wa mahoteli na usambazaji wa gesi.

Mbali na utiaji saini huo, Rais Samia amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali bin Ahmed Al-Kuwari ambapo wamejadili masuala ya kikodi baina ya nchi hizo mbili, uwekezaji, biashara, gesi, ufugaji, utalii na kilimo.

Vilevile, katika mazungumzo ya Rais Samia na Waziri wa Afya wa Qatar, Mhe. Dkt. Hanan Mohamed Al Kuwari wamekubaliana wataalamu wa Tanzania wabadilishane uzoefu kwenye sekta ya afya hasa katika huduma za kibingwa na za dharura.

Rais Samia pia katika ziara yake ya kikazi alifanya mazungumzo na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al Thani, wafanyabiashara wakubwa na kuhudhuria Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliomalizika leo katika Kituo cha Elimu cha Multaqa Jijini Doha.

ZuhuraYunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

1665082432541.png

Attachments

Kuna mikataba inayosainiwa hapa Bongo na mikataba ya kusainishwa huko nje baada ya kuwazungusha kwenye mali kama shetani alivyomzungusha Yesu akitaka ampe mali ili amsujudie. Hawa wa kwetu wana uwezo wa kukataa asali ya Quatar?
 
Mwezi wa pili tulisaini mikataba na UAE wenye thamani ya 17 trillion, je kuna lolote lililoleta matokeo chanya? Au matokeo hasi tu ya loliondo?
 
Ndio mans wale wabunge wa USA walifika Kenya na Rwanda mana hapa tupo bize na waarabu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania, Zanzibar na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Kwa upande wa Chemba ya Biashara ya Tanzania, mkataba ulisainiwa na Rais wa Chemba hiyo Paul Koyi, huku pia ukisainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour.

Aidha, kwa upande wa Qatar mkataba huo umesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya nchi hiyo Muhammed bin Ahmed Al Kuwari uliofanyika Jijini Doha.

Lengo la Mkataba huo ni kuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Qatar hususan kwenye sekta za utalii, miundombinu, ujenzi wa mahoteli na usambazaji wa gesi.

Mbali na utiaji saini huo, Rais Samia amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali bin Ahmed Al-Kuwari ambapo wamejadili masuala ya kikodi baina ya nchi hizo mbili, uwekezaji, biashara, gesi, ufugaji, utalii na kilimo.

Vilevile, katika mazungumzo ya Rais Samia na Waziri wa Afya wa Qatar, Mhe. Dkt. Hanan Mohamed Al Kuwari wamekubaliana wataalamu wa Tanzania wabadilishane uzoefu kwenye sekta ya afya hasa katika huduma za kibingwa na za dharura.

Rais Samia pia katika ziara yake ya kikazi alifanya mazungumzo na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al Thani, wafanyabiashara wakubwa na kuhudhuria Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliomalizika leo katika Kituo cha Elimu cha Multaqa Jijini Doha.

ZuhuraYunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

huu ni ujinga kusaini mikataba na nchi masikini ambazo nazo zinapambana kutoka kuuchumi!!!… Uarabuni ni third world countries hazipo hata kwene nchi zenye uchumi mkubwa wakuweza kuzisaidia nchi kama Tanzania!!…. ameacha kuzifuata nchi kama japani, south korea au Israel kutwa kigulu uarabuni
 
Safi Sana na kazi nzuri Sana inayofanywa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani,Hakika uwekezaji unakwenda kuongezeka Sana hapa nchini Jambo litakaloibua fursa nyingi Sana kwa vijana hasa suala la ajira, lakini pia wigo wa Kodi utaongezeka na kuongezeka kwa mapato ya kikodi yatakayosaidia kuwekeza katika miradi mbalimbali yenye kugusa maisha ya watanzania wanyonge, Hakika mh Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania, Ni Rais aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania, Zanzibar na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Kwa upande wa Chemba ya Biashara ya Tanzania, mkataba ulisainiwa na Rais wa Chemba hiyo Paul Koyi, huku pia ukisainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour.

Aidha, kwa upande wa Qatar mkataba huo umesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya nchi hiyo Muhammed bin Ahmed Al Kuwari uliofanyika Jijini Doha.

Lengo la Mkataba huo ni kuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Qatar hususan kwenye sekta za utalii, miundombinu, ujenzi wa mahoteli na usambazaji wa gesi.

Mbali na utiaji saini huo, Rais Samia amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali bin Ahmed Al-Kuwari ambapo wamejadili masuala ya kikodi baina ya nchi hizo mbili, uwekezaji, biashara, gesi, ufugaji, utalii na kilimo.

Vilevile, katika mazungumzo ya Rais Samia na Waziri wa Afya wa Qatar, Mhe. Dkt. Hanan Mohamed Al Kuwari wamekubaliana wataalamu wa Tanzania wabadilishane uzoefu kwenye sekta ya afya hasa katika huduma za kibingwa na za dharura.

Rais Samia pia katika ziara yake ya kikazi alifanya mazungumzo na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al Thani, wafanyabiashara wakubwa na kuhudhuria Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliomalizika leo katika Kituo cha Elimu cha Multaqa Jijini Doha.

ZuhuraYunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Tanzania and its semi-autonomous Zanzibar island signed an agreement with Qatar on Thursday to strengthen trade and investment relations and revitalize their long-standing bilateral ties.

The tripartite agreement was signed by the chambers of commerce of Tanzania, Zanzibar, and Qatar, according to a statement issued by Tanzania's Directorate of Presidential Communications.

The agreement, witnessed by Tanzanian President Samia Suluhu Hassan, who is on an official visit to Qatar, is aimed at enhancing trade and investment cooperation and partnership between business communities from the two countries in tourism and hospitality, infrastructure, and energy, the statement said.

It added that the agreement was signed by Mohamed bin Ahmed Twar Al Kuwari, first vice chairman of the Qatar Chamber of Commerce, and Paul Koyi, chairman of Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture, as well as Ali Suleiman Amour, chairman of Zanzibar National Chamber of Commerce.

Meanwhile, President Hassan met with Qatar's Public Health Minister Hanan Mohamed Al Kuwari and agreed to share expertise in emergency and trauma care, the statement said.

Hassan also met with Qatar's Emir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, business leaders, and attended the world innovation summit for health, which concluded on Thursday, it added.

The east African country has a close business relationship with Qatar, with trade exchange between the two countries estimated to have increased significantly in the last five years, according to government records.

In 2020, Tanzania exported goods worth $8.9 million to Qatar. The products exported include fish fillets and sawn wood, the statistics show.
 
Sijuo kama hii mikataba huwa inasaidia kwa kiwango. Imesainiwa mikataba mingi sana ya aina hii, tangu enzi za awamu ya kwanza lakini ukuaji wa uchumi na maendeleo yetu, vyote ni mwendo wa kinyonga.
 
Lakini ni Fursa, Kama tunaitumia ama tusipoitumia ni Sisi, Binafsi nafahamu watu wengi sana wame toka kimaisha kkoo baada ya mama kuzunguka Congo, na Nchi jirani, Machinga anapiga 100K+ kwa siku na Hana hata mtaji kwa hawa majirani zetu.
 
Hivi, umaskini wa watanzania uko wapi hasa? Kwenye kufikiri, kuamua au kutenda?

Maana kama ni rasilimali tunazo za kutosha kulinganisha na hao watu. Au tatizo rangi ya ngozi???

Loh, ama kweli!!!
 
Hivi zile hati za makubaliano ya kibiashara kati ya Tanzania na Oman zimeanza kufanya kazi? Isijekua ni mazoea tu kusaini hati za makubaliano
 
huu ni ujinga kusaini mikataba na nchi masikini ambazo nazo zinapambana kutoka kuuchumi!!!… Uarabuni ni third world countries hazipo hata kwene nchi zenye uchumi mkubwa wakuweza kuzisaidia nchi kama Tanzania!!…. ameacha kuzifuata nchi kama japani, south korea au Israel kutwa kigulu uarabuni
Hii ndio Doha mkuu
main-qimg-29a4be3f8892427e76d77e07f984d783.jpeg

Qatar kwa pato la mtu mmoja mmoja ina Hela kuliko Nchi zote ulizotaja, Kutegemea na kampuni ya utafiti huikosi Qatar kwenye nchi Tajiri duniani na Tafiti nyengine ni nchi Ya kwanza kabisa Duniani.

Pato La mtu mmoja mmoja ni dola 110,000 kwa mwaka na Pato la Nyumba kwa mwezi ni kama dola 25,000.

Sasa ambayo karibia kila Mwezi nyumba inaingiza milioni 50 huoni faida ya kufanya nayo biashara?
 
Kwamba nchi Tajiri zaidi Duniani kwa pato la mtu mmoja mmoja haina issue ina tende tu?
Kwani ukiondoa tende kuna teknolojia gani waliyovumbua hapa duniani??

Hayo mafuta yenyewe wanachimbiwa na Wazungu.
 
Labda wanatuzidi kwenye kuja.mber tu.
Kuna Scientist wengi tu Middle East kuanzia wa zamani Enzi hizo mpaka Sasa. Chimbuko la sayansi ya Vitu vingi ni Huko.

Akili kama yako unadhani wana mafuta tu basi matajiri. Lakini huwezi kufikiria Kuna Nchi kibao duniani zina mafuta ila masikini wa kutupwa mfano mzuri Nigeria.

Hao jamaa wapo vizuri sana, Angalia World cup December utaelewa vizuri.

Sasa hivi Middle East Kuna MA Scientist wakubwa tu wana Vumbuzi nyingi Ambazo zinatumika Duniani Kote.

Mobile 1791.png

Hio ni picha ikionesha ramani ya kampuni mbali mbali na Maabara zao za Utafiti, Kuanzia Microsoft, Oracle, Huawei wote wapo huko wanafanya tafiti ila akili za Lumumba zinaona Tende tu.
 
Back
Top Bottom