Tanzania na sera za uwekezaji

Tanzania na sera za uwekezaji

Kijiji Chetu

Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
7
Reaction score
0
Nimerudi tena mwanakijiji, mbuga zangu kuzinyatia
Siwahukumu wa magharibi, hata wale wa ghuba,
kukicha mitutu wanaikoki, wanyama wangu kuwaua,
Sheria ni kwa sisimizi, kwa tembo eti huzikwa,
Nasema haiingiii akilini, waporaji kupewa mbuga,
Tanzania umekosa vingi, hata mapori unawekeza?

Mwisho wa siku watatimka, nyasi na mchanga kutuachia,
Watoto wangu watakuja lia, hata vitukuu wataja shangaa,
Washindia shuka kutimliwa,eti loliondo wameivamia,
Mwanakijiji kukicha ninalia, watunga sera wanachechemea,
Masikio yao wameyaziba, huku mwanakijiji nikiteketea,
Tanzania umekosa vingi, hata mbuga unawekeza?

....................... n.k
 
Back
Top Bottom