KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
1. 1961-1984 President Mwalimu Nyerere - Alinyonga wananchi 10.
2. 1985-1995 President Ali Hassan Mwinyi - alinyonga wananchi 72.
3. 1995-2005 President Ben Mkapa - Alinyonga wananchi 0.
4. 2005-2008 President Jakaya Kikwete - Amenyonga 0.
Mkuu, mnyongaji huwa anonymous kama sikosei. Labda tungetumia "aliidhinisha kunyongwa". Ni wazo tu hasa kutokana na uzito wa kitendo chenyewe.
Hukumu ya kifo inapaswa kuondolewa katika sheria zetu kwa sababu si ya kiutu. Viongozi wetu wanao utu, na ndio maana hawaidhinishi kwa kiwango chake utekelezaji wa hukumu hiyo.
Wakuu ninawasikia wote, again swali langu lingine ni kwa nini under Mwinyi, walionyongwa ni wengi kuliko awamu zote, ina maana kipindi hicho ndicho ujambazi au uhalifu ulizidi mno, au ndicho kipindi sheria ilikuwa ikifuatwa kwa msumeno, au ulikuwa ni uzembe wa kutofuata sheria?
Actually, hii sheria ya kuua tunatakiwa tuifute haraka sana, haina maana hata kidogo wala sio utanzania kabisa!
Kitila tunasema kuua kwa kunyongwa hadi kufa ifutwe lakini kua hili la Mafisadi kutuua pole pole hadi tufe unasemaje ? Maana ndiyo wanapamba moto kutuua Watanzania tufanyeje sasa ?
Kumbukumbu nilizonazo mimi ni kwamba Mwinyi alinyonga watu 89 na sio 72 mtu wangu.Magereza yanayohifadhi wafungwa wa kunyongwa ni mengi sana hapa TZ,na tatizo lililopo ni utekelezaji wa adhabu hiyo.
Mimi nahisi huyu mzee alikuwa anatekeleza sheria, tofauti na hao wengine ambao inaonekana wanauma na kupuuliza. Coming to think again about this mzee, I think he was more serious than we have always thought of him! Huyu mzee inawezekana kaifanyia TZ mambo ya maana kuliko hao tunaowasifia kila kukicha!
Naungana na wengi kuwa Mwinyi alikuwa serious na Ofisi kwani hata baada ya mauaji kule Shinyanga yeye aliwajibika jinsi ilivyotakiwa bila kulazimishwa. ninani leo anathubutu ya Mzee Ruksa???Kumbukumbu nilizonazo mimi ni kwamba Mwinyi alinyonga watu 89 na sio 72 mtu wangu.Magereza yanayohifadhi wafungwa wa kunyongwa ni mengi sana hapa TZ,na tatizo lililopo ni utekelezaji wa adhabu hiyo.
1. 1961-1984 President Mwalimu Nyerere - Alinyonga wananchi 10.
2. 1985-1995 President Ali Hassan Mwinyi - alinyonga wananchi 72.
3. 1995-2005 President Ben Mkapa - Alinyonga wananchi 0.
4. 2005-2008 President Jakaya Kikwete - Amenyonga 0.
Mkuu, mnyongaji huwa anonymous kama sikosei. Labda tungetumia "aliidhinisha kunyongwa". Ni wazo tu hasa kutokana na uzito wa kitendo chenyewe.
Hukumu ya kifo inapaswa kuondolewa katika sheria zetu kwa sababu si ya kiutu. Viongozi wetu wanao utu, na ndio maana hawaidhinishi kwa kiwango chake utekelezaji wa hukumu hiyo.
Sasa tuamini lipi kwenye hizi statistics!
Source: http://www.handsoffcain.info/bancadati/schedastato.php?idcontinente=25&nome=tanzaniaRecords collected by the LHRC show that since independence in 1961, 238 people (232 men and 6 women) were executed after being convicted of murder. The number of executions between 1961 and 1995 amounted to 9.3 per cent of death row prisoners who were hanged
Wewe unanichekesha unauliza walinyongwa kwa makosa gani kwani ili mtu a qualify kunyongwa anatakiwa awe na kosa gani mkuu???Hapa kuna utata mkubwa. Wakati Nyerere anaondoka mwaka 1985 alipata nafasi ya kuzungumza katika hotuba yake ya kuagana, nadhani alikuwa na maafisa wa Magereza.
Alisema kati ya mambo magumu ambayo Rais anaweza kufanya na yamo ndani ya wajibu wake ni kutoa uamuzi wa kutekeleza hukumu ya kunyongwa.
Akasema kuwa ndani ya miaka yake zaidi ya 20 kama Rais aliruhusu watu wawili tu wanyongwe. Kuna yule aliyemuua Dr. Kleruu na mtu mwingine (sikumbuki jina lake mara moja).
Sasa leo tunaambiwa watu kumi walinyongwa wakati wa utawala wa Mwalimu, kuna mtu anatakiwa kutuambia ni kina nani hao na kwa makosa gani? Yawezekana tukapata majibu ya kina Kassim Hanga...
Pole sana ,kumbe uncle yalimkutawengi walihukumiwa kunyongwa. Sasa sina uhakika kama wanaohukumiwa katika mahakama za kijeshi (kama aliyemuua mjomba wangu) hukumu zao za kunyongwa nazo ni lazima zipate baraka za Rais (theoretically yes) au ndiyo jeshi likisema unanyongwa ndiyo unanyongwa?
Mkuu, Kassim Hanga ni nani na alifanya nini? Na huyo Othman Shariff ni nani na alifanya nini?Data zinatia shaka.Kama kuna majina yatajwe.Kuna mtu mwingine mbali na Kassim Hanga kwa jina Othman Shariff ambaye alikuwa mjumbe wetu UN.
Huyo mke wa mzungu alikuwa race ipi?No. siyo Kassim Hanga. Kuna yule Mzungu mmoja alimuweka mkewe kwenye gari halafu akaisukuma kwenye milima huko kusini na mkewe akafa na yule bwana akadanganya kuwa kapata ajali na akaenda kudai Insurence akalipwa pesa nyingi sana.Nasikia Mwalimu aliita mpaka Scotland Yard kufanya uchunguzi na yule mzungu alibainika na alinyongwa.Ni wakati tu tumepata Uhuru. Je, mpo hapo? Kwa hiyo Mwalimu alisaini watu wawili tu wanyongwe na siyo kumi.Mafisadi wanampakazia bwana.au watupe orodha ya hawo kumi basi.