Tanzania na Sheria: Rais Mwinyi Aliua Wengi Zaidi!

Tanzania na Sheria: Rais Mwinyi Aliua Wengi Zaidi!

Fundi nakuunga mkono point yako ya wale wanaouliwa wawekwe hadharani ummati wa watu washuhudie...hapo patakuwa patamu kwa mtu akitokea kaua mtu like Ditto, nae atanyongwa Hadharani. Hii inaweza leta disciplne fulan ktk Jamii.

Pia mtu atakae hukumiwa itabidi haki itendeke vilivyo. asije mtu akaonewa ati kwa kuwa masikini, au hana wakili, au akasaidiwa eti kwa kuwa alikuwa mkubwa au Baba yake KIGOGO.

Suala la kusamehe litakuwepo na pia discipline iwepo. mfano mtu akamuua nduguyo kwa gari, ofourse lazima afungwe apate nidham lkn pia ndugu zake walipwe bloody money, either serikali au familia ya muuaji ktk kutaka msamaha kutoka kwa wafiwa.

na kama serikali/mahakama itaamuua kimakosa na hukum ishapita, basi ni haki wafiwa LAZIMA walipwe Pesa za kifuta jasho, ili kiweze kuwafaa watoto, wajane, kulipa madeni etc

KUFUTA Sheria ya Unyongaji si VEMA, Hii itawajengea Kiburi mtu yoyote wakati wowote anaweza kukumaliza, then anajua yeye atakaa Jela, atakaa bure, kula bure, maji, umeme bure etc...bado watakuja ndugu zake kukusalimu.please tusije iona ni ya kikatili.

Apart from that, Wahuni, Majambazi, majangili yanaweza kuchukua deal kwa MAFISADI kuwamaliza wafichua MABOMU...wakijua wao watakamatwa lkn hawatouwaw, atlast itafika wakati wa sikukuu za Mashujaa au Uhuru RAIS na PAROLE TEAM watatoa msamaha.....
 
Fundi nakuunga mkono point yako ya wale wanaouliwa wawekwe hadharani ummati wa watu washuhudie...hapo patakuwa patamu kwa mtu akitokea kaua mtu like Ditto, nae atanyongwa Hadharani. Hii inaweza leta disciplne fulan ktk Jamii.

I was just being sarcastic!
 
Ukweli ni kwamba Tanzania hatua utamaduni wa kutunza kumbukumbu. Si ajabu kesho kutwa mwingine ataibuka na data tofauti kabisa na hizi. Lakini hata kama mwinyi alinyonga walihukumiwa kisheria na sheria za nchi zinaruhusu, kuna tatizo?
 
1. Hili swala la Raisi kuwa Chiefhangman ni ngumu- hata mimi nikiwa raisi kuweka mkono mtu anyongwe ni shida! Maanake huna makosa mengi ya kubambikizwa!

2. Bado sijaelewa ni sababi zipi zilizomfanya AHM na upole wake wote kuwa na mkono mwepesi hivyo!

3. On my view- adhabu ya kifo ifutwe! Manake unless proven 100% kuna wengi tu hata US wamenyongwa kimakosa!
 
Richard,green29,

..Mama aliyeua alikuwa anaitwa Asha Mkwizu Hauli. Mke wa Dr.Hauli.

..Aliyeuawa anaitwa Happiness Senzota.

..Dr.Hauli alikuwa daktari bingwa wa maradhi ya akili Muhimbili.

..Tatizo hapa lilikuwa ukware. Dr.Hauli alikuwa akitembea na Hapiness Senzota huku akiwa na mkewe Asha Mkwizu Hauli.

..Kuna kesi nyingine ya Mama Liundi kunywesha watoto wake watatu sumu. Mama alichanganyikiwa kwasababu ya mumewe kuwa na mabibi nje.

..Watoto wawili walifariki dunia, na mmoja aka-survive.

..Sidhani kama hao Asha Mkwizu Hauli, na Mama Liundi waliuawa.

NB:
..Hii mada inatumika kumpaka matope Mzee Mwinyi.

..Tatizo ni kuwepo kwa sheria ya kunyonga.

..Raisi wa nchi ndiye anayesaini mswaada kuwa sheria. Sheria ya kunyonga ilipitishwa wakati Mwinyi hayuko madarakani.

..Vilevile nasikia kulitokea malalamiko kuhusu kutokutekelezwa kwa hizi hukumu.
 
Mimi nampongeza kwa dhati kabisa Mzee Rukhsa kwa kutekeleza ipasavyo adhabu ya kifo ambayo hadi sasa ipo kwa mujibu wa sheria. Huu ndio utawala wa sheria, na inapaswa kiongozi wa nchi aoneshe mfano. Kama sheria ya nchi inasema muuaji auawe, basi na itekelezwe hivyo. Ikibadilika na kuwa vinginevyo, basi itekelezwe hiyo mpya. Hata hivyo siungi mkono hata kidogo kufutwa kwa hukumu ya kifo, ni hukumu inayowafaa hao wanaotenda makosa yanayoendana nayo. Cha muhimu kuzingatia ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka, na wote wanaofikia katika hatua ya kupata hukumu hiyo wawe wamepata nafasi zote kwa mujibu wa sheria za kujitetea, na iwe imethibitishwa pasi shaka lolote kuwa wana hatia ya makosa hayo. Hatuwezi kuwaacha wauaji wanarandaranda mitaani ati tunajifanya tuna huruma, huruma ya nini? Mbona wao hawatuhurumii? Ati tuwafunge kifungo cha maisha? Kwa nini? Sasa tukimfunga muuaji kifungo cha maisha, aliyeadhibiwa ni yeye au ni sisi? Yaani mtu atuulie watu wetu halafu sie tukamweke mahali tumtunze bure, kula, kulala, kutibiwa, kila kitu bure kwa gharama yetu? Muuaji? Sikubali asilani! Wanyongwe!

Ninawalaumu sana hao kina Mkapa na sasa hivi Kikwete ambao wanasita kuweka saini hao waliohukumiwa wanyongwe. Ina maana hawawaamini majaji waliotoa hukumu hiyo? Wanaogopa nini kuweka hiyo saini? Rais akiweka saini waliotiwa hatiani wanyongwe, si yeye anayewanyonga, ni makosa yao wenyewe kama yalivyothibitishwa na mfumo wa sheria na kuhukumiwa na majaji wasomi na waheshimiwa sana. Sasa rais hofu yake nini? Kwa kutoruhusu unyongaji wa waliokwisha hukumiwa, Marais Mkapa na Kikwete wanaendelea kusababisha mrundikano wa majitu "condemned" huko magerezani, ambako yanaendelea kutamba tu wakati yameangamiza roho za wenzao. Namsihi ndugu Kikwete, afuate utawala wa sheria. Kama sheria inasema huyu anyongwe, basi na anyongwe, tuache huruma za kijinga na za kimdebwedo za kuiga upumbavu wa NGO's zinazotafuta hela za kula kwa kutetea "kuwatunza wahalifu". Hukumu ya kifo si adhabu kwa mhukumiwa (hana nafasi ya kujirekebisha), ni kuondosha kero, kama unavyopalilia kuondoa magugu shambani, ni kufuta mijitu isiyofaa na isiyorekebika kwenye uso wa dunia, ni mijitu isiyofaa ndio maana kule gerezani inaitwa "condemned". Mainjinia wanaelewa jengo wakiliita "condemned" si ati la kufanyia ukarabati kupiga rangi nk, ni la kubomoa! Vivyo hivyo kwa binadamu yeyote anaye-fit katika category ya "condemned". Wewe jitu likivamia nyumbani kwako likaua mkeo na watoto, utapenda likafungwe maisha, ati uendelee kukatwa kodi kulilisha na kulitunza baradhuli hilo? No way!

Mheshimiwa Kikwete, mimi (na ninajua tuko wengine wengi wenye msimamo huu), tunakuomba utimize wajibu wako, weka hiyo saini wa kunyongwa wanyongwe. Tekeleza kiapo chako ulichoapa cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya nchi iliyowekwa kwa mujibu wa sheria, na Mungu atakusaidia.
 
Cha muhimu kuzingatia ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka, na wote wanaofikia katika hatua ya kupata hukumu hiyo wawe wamepata nafasi zote kwa mujibu wa sheria za kujitetea, na iwe imethibitishwa pasi shaka lolote kuwa wana hatia ya makosa hayo.

Hapa ndipo kwenye matatizo. Anayethibitisha hivi nani? hata huko marekani watu kibao wamekuwa exonerated na DNA baada ya kusota muda mrefu? Tutawarudisha vipi wale tuliowanyonga kwa makosa? Wote tunajua kuwa mwenye pesa na influence hanyongwi. Wanaonyongwa ni hao wezi wa kuku ambao kil kukicha tunawatia kiberiti. Hatujuilizi kuwa mbona bado kuku wanaibiwa? Tuangalie matatizo yaliyomo katika jamii yetu hadi kupelekea watu kufanya vitu kama hivi. Wale ambao watathibitishwa kuwa hawana nafasi katika jamii yetu watupwe hukp, lupango na ufunguo tuupoteze. Nani mwenye akili yake timamu atataka kuzeekea ukongo? Adhabu ya kifo haina nafasi katika jamii yeyote iliyostaarabika.
 
Hapa ndipo kwenye matatizo. Anayethibitisha hivi nani? hata huko marekani watu kibao wamekuwa exonerated na DNA baada ya kusota muda mrefu? Tutawarudisha vipi wale tuliowanyonga kwa makosa? Wote tunajua kuwa mwenye pesa na influence hanyongwi. Wanaonyongwa ni hao wezi wa kuku ambao kil kukicha tunawatia kiberiti. Hatujuilizi kuwa mbona bado kuku wanaibiwa? Tuangalie matatizo yaliyomo katika jamii yetu hadi kupelekea watu kufanya vitu kama hivi. Wale ambao watathibitishwa kuwa hawana nafasi katika jamii yetu watupwe hukp, lupango na ufunguo tuupoteze. Nani mwenye akili yake timamu atataka kuzeekea ukongo? Adhabu ya kifo haina nafasi katika jamii yeyote iliyostaarabika.

Fundi Mchundo samahani sikubaliani na wewe hata kidogo. Yaani unamaanisha kuwa kwa vile kuna matatizo katika kutekeleza adhabu basi ifutwe? Ni adhabu ipi utekelezaji wake hauna matatizo? Hata hao wanaofungwa vifungo vya miezi mitatu, mwaka mmoja kuna baadhi ambao wanakuwa wameingia hatiani kwa kasoro zilizo katika utekelezaji wa sheria zaidi kuliko uzito wa makosa, sasa nao adhabu ifutwe basi! Waachiwe waende nyumbani, kwa kuwa kuna kasoro katika kufikia uamuzi na kutekeleza adhabu! Hata watu matajiri wenye pesa zao wakiiba, au wakijeruhi hawafungwi, tunajua hilo na huwa tunaona, kwa hiyo unataka kusema hii inahalalisha kuondoa adhabu ya kifungo kwa watu wote kwa kuwa wapo ambao hata wakiiba hawafungwi? Matokeo yake tutafuta adhabu zote basi! Hapana ndugu yangu, tuondoe kasoro hizo za kiutekelezaji, adhabu iendelee. Mwuaji naye anyongwe, full stop. Siku serikali itakapotamka inataka kuondoa adhabu hiyo, mimi na wenzangu wengi tu tutaitisha maandamano ya kushinikiza adhabu hiyo iendelee kuwapo, inawastahili hao wenye makosa ambayo imetungiwa. Unasema adhabu ya kifo haina nafasi katika jamii iliyostaarabika? Sasa huko chenye nafasi ni nini, watu kuuawa na wahalifu, halafu waathirika wa mauaji wanalazimika kuendelea kuwatumikia wauaji kwa kodi zao? Huo ndio mdebwedo ninaozungumzia na sitaki kuuona kwenye nchi yetu. Huko walikofuta adhabu ya kifo kwa lengo la kuwaridhisha mafia wanaotetea wahalifu wenzao, kuna wananchi wengi sana wanaopinga hali hiyo na wanataka adhabu hiyo irejeshwe. Bahati mbaya mafisadi wakishashika nchi basi na hao mafia wanapata utetezi wa kudumu. Yale majimbo ya Marekani ambako adhabu ya kifo inaendelea, waungaji mkono wa adhabu hiyo wanaendesha mapambano sambamba na watetezi wa wahalifu wanaotaka ifutwe. Kama unadhani wanaounga mkono hukumu ya kifo ni wachache, tembelea tovuti hii: http://www.prodeathpenalty.com/.

Napenda kumnukuu mmoja wa watetezi maarufu wa hukumu hiyo ambaye namwunga mkono moja kwa moja, anaitwa John McAdams:
"If we execute murderers and there is in fact no deterrent effect, we have killed a bunch of murderers. If we fail to execute murderers, and doing so would in fact have deterred other murders, we have allowed the killing of a bunch of innocent victims. I would much rather risk the former. This, to me, is not a tough call."

Napenda kuitafsiri nukuu hiyo kwa kiswahili, maana huo hasa ndio msimamo wangu pia:

"Tukiwanyonga wauaji na bado ikawa haijasaidia kuzuia (mauaji) tutakuwa tumeua genge la wauaji. Tukishindwa kuwanyonga wauaji ilhali kufanya hivyo kungewazuia wauaji wengine (kufanya mauaji), tutakuwa tumeruhusu mauaji ya halaiki ya wahanga wasiokuwa na hatia. Ni bora kuwanyonga wauaji(potelea mbali isiposaidia). Hili, kwangu, si wito mgumu "
 
Wanaounga mkono adhabu ya kifo ni wengi kwa sababu inakidhi kiu chetu cha kisasi. Hao unaowaita wauaji una hakika gani na hilo? Msimamo wangu na wenzangu tunaopinga adhabu hii ni kuwa haiwezi kutendeka kwa haki. Watoto wa wakubwa wangapi wameua na wanaendelea kupeta? huko marekani inajulikana wazi kuwa rangi ya mtu anayeshutumiwa kutenda kosa, rangi ya mtu aliyetendewa kosa na uwezo wa kipesa wa mshitakiwa vyote vinachangia katika utekelezaji wa adhabu hii. Si wanaofungwa miezi mitatu tu, kuna watu wamefungwa miaka 15 na zaidi ambao wamekuja kugundulika baadaye kuwa walikuwa hawana hatia. Hawa wangenyongwa ingekuwaje? Cha msingi ni kuwa adhabu ya kifo ni final. Hapo mtakapogundua fulani amenyongwa kwa makosa mtafanya nini? Au mtaenda kuomba radhi kaburini kwake? Hapa kwetu ambako nyenzo za kufanyia uchunguzi ni duni, wangapi wataonekana wana hatia baada ya kupata kibano cha mapolisi? Ni wangapi wamebambikiwa kesi za maada baada ya kukosana na wenye vyombo vya usalama? Tusisahau vilevile kuwa hii hukumu si kwa ajili ya wale waliopatikana na hatia ya mauaji tu. Inatumika vile vile kwa kile kinachoitwa treason. Wote tunajua uwezekano wa kutumia hii sheria kuwaondoa wale wanaoonekana ni tishio kwa serikali tawala. Hilo la kuwa hukumu hii ni detterent sio kweli. Nitarudia swali langu la awali, kama kweli kuua mhalifu ni detterent, mbona wizi wa kuku unaendelea pamoja na juhudi zote za wananchi kuwatia kiberiti vibaka? Adhabu hii inatumika kuwavuga wananchi ili watawala wasiwajibike na basic needs za watawaliwa. Mimi msimamo wangu ni ule ule. Adhabu hii haina nafasi katika jamii yeyote inayojiona imestaarabika.
 
Mzee hata sikunotisi... nilidhani ni browser yangu, naona mafisadi wameingilia hata jina langu.. daymn you mafisadi.. leave me alone!

Mkjj au umeshajiunga na chama cha mafisadi na unataka kutuonyesha jinsi ulivyo mnazi hata jina umelitia hiyo rangi inayoumiza macho?...🙂
 
Bado nasisitiza kuwa adhabu kutokutekelezwa kwa haki si kigezo cha kufuta adhabu hiyo. Suluhisho la tatizo hilo la haki litafutwe ndani ya mfumo huo wa haki na adhabu iendelee kwa wanaostahili. Labda tunaweza kurekebisha sheria kuhusu ni nani anayestahili adhabu ya kifo, lakini si kuifuta hukumu hiyo. Kwa mfano, kuwapa wanaopatikana na hatia ya uhaini adhabu ya kifo, hilo kwa maoni yangu si sawa kwa kuwa uhaini kama kosa ni relativistic, haini wa leo anaweza kuwa shujaa wa kesho, kwa sababu mifumo ya kisiasa si suala la kudumu. Kwa hapo nasema ni sawa hawa wakapewa kifungo na si kuuawa, na hivyo kwa mwathirika huyo siku ukiwepo mfumo wa kisiasa unaokubaliana na mawazo yake anaweza kuwa huru tena. Lakini kwa makosa mengine, impact zake ni absolute, na hakuna siku itabadilika ionekane vinginevyo. Mfano jambazi anayevamia nyumbani kwako na kubaka mkeo, kuua wanao na kukujeruhi vibaya, sidhani kama kuna siku ati jamii itaona alifanya vema! Kwa hao na wengine wa namna hiyo, adhabu yao iendelee kuwa kunyongwa, hakuna sababu ya kumuonea huruma wakati yeye hana huruma hata kidogo.

Hivi majuzi hapa nilikuwa naangalia documentary fulani ya BBC yenye kichwa "Behind Bars", mwandishi alitembelea jela maarufu ya wafungwa hatari huko Marekani na kuhojiana na wafungwa. Hivi unajua kuna mfungwa mmoja alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 451 na vifungo vya maisha 11 kwa kupatikana na makosa mengi ya utesaji na mauaji, ambako katika mauaji 11 alitiwa hatiani. Huyo jamaa anasema hajutii alichokifanya, ni maisha tu. Na anasema hata hapo jela ni maisha tu, kwani ana uhakika wa kupata kila anachokihitaji bila kuwa na mashaka ya kupoteza kazi, anadai "I'm gonna be taken care of until I die!" Sasa mizigo kama hii ya nini, jitu uaji, bado linatamba jela kwa kodi za walewale waliouliwa ndugu zao! Serikali inayokubali hali kama hii ni serikali iliyokosa ustaarabu, ni ya kijambazi na kimafia! Watu wanaostahili hukumu ya kifo wauawe, basi. Hakuna kubembelezana sijui haki na mijitu ambayo sisi haitutendei haki! Hao wanatakiwa wawe pruned off, wiped out of the surface of the earth. Basi.

Marekebisho stahiki yafanyike, haki izingatiwe, na hukumu ya kifo iendelee kuwapo kwa wote wanaostahili.
 
JokaKuu,

Ahsante sana kwa msaada wako sasa naweza kukumbuka jambo hili kwa usahihi.

Kwa kweli jambo lile likitutisha sana hasa sisi tuliokuwa darasa moja na mmoja wa watoto wa marehemu. Hasa baada ya kusikia kuwa mabaki ya marehemu Happiness yalikutwa kwenye bustani nyuma ya nyumba ya dakta Hauli!

Ilikuwa ni "experience" ambayo huwa naikumbuka.

Sasa hili la pili kihusu Mzee Mwinyi, naelewa kwamba watu wanajaribu kumpaka matope mzee huyu lakini ukweli unabaki palepale kwamba kaondoka bila madoa makubwa ya kutisha.

Nakumbuka Mzee Mwinyi kulipokuwa na hafla pale uwanja wa taifa, alikuwa akiingia alipata kushangiliwa na watu na baadae baadhi ya viongozi wengine walikuwa wakiingia uwanja ulibaki kimya kwa mshangao-kwa muda hivi!

Halafu mwisho Jokakuu, je idara ya takwimu hapo TZ ipo vipi? Kwa sababu nafikiri wote hapa tulijaribu kuchangia hii mada tumepungukiwa baadhi ya hizi "data" kama hizo ulizoleta.
 
Hukumu ya kifo iendelee kuwapo Tanzania kwani wanaostahili kuipata bado wapo. Pengine tunaweza kujadili makosa ambayo mkosaji anastahili kuhukumiwa kifo, lakini si ati hukumu hiyo kufutwa. Hukumu ya kifo ni hukumu halali kabisa. Someni zaidi hapa chini iwasaidie katika kufikiri (hii ni maalumu hasa kwa kuelimisha wanaopinga hukumu hiyo wasitupeleke kubaya, penye kulea mihalifu isiyorekebika!). Hii insha nimeinakili kutoka http://www.rajuabju.com/, simjui mwandishi, nimependa tu mawazo yake.

An issue that has continually created tension in today's society is whether the death penalty serves as a justified and valid form of punishment. Whenever the word "death penalty" comes up, extremists from both sides start yelling out their arguments. One side says deterrence, the other side says there's a potential of executing an innocent man; one says justice, retribution, and punishment; the other side says execution is murder. Crime is an evident part of society, and everyone is aware that something must be done about it. Most people know the threat of crime to their lives, but the question lies in the methods and action in which it should be dealt with. In several parts of the world, the death penalty has been apportioned to those who have committed a variety of offenses from the time of ancient Babylon to present-day America. The Roman Empire made use of the death penalty liberally, as did the Church of the Middle Ages. As history tells us, capital punishment, whose definition is "the use of death as a legally sanctioned punishment," is an acceptable and efficient means of deterring crime. Today, the death penalty remains an effective method of punishment for murder and other heinous crimes.

There is debate over the morals and effectiveness of such a harsh sentence. Most commonly, the death penalty is challenged as a violation of the Eighth Amendment, which says that the U.S. cannot use "cruel and unusual" punishment. Due to the fact that "punishment" is a legal infliction of suffering, it must be somewhat "cruel.” As for being unusual, it is anything but, due to the long history of its usage. People will plunder, take advantage of others, and commit crimes as long as it is in their best interest to do so. The purpose of our entire criminal justice system is to protect the rights of life, liberty, and property for all its citizens. To do this, the punishment for crime must be harsh enough to deter potential criminals. Under this mindset, the death penalty makes perfect sense. Here is a punishment that truly makes a criminal pay for his crime, stops the criminal from committing it again, and deters other criminals from committing the same crime.

The punishment for murder is getting to be shorter and shorter. A judge could sentence a man to life in prison. That same man could be out of jail with 15 years. How has life in jail become known as ten to fifteen years? If the judge says life with no parole, then the criminal could stay in jail a bit longer, but that would mean the state and it's voters would have to take care of the prisoner for twenty to twenty five years. How can we trust the murderers and thieves of our country to a judicial system that will either let them out in ten years or have us take care of them for twenty years, and then let them go? The criminals do not fear the punishment anymore, because they know they will not die. Punishment is meant to give justice to the wrongdoer and to keep him from doing it again. I am not saying we execute all of the criminals in the world, but it has to remain an option for the courts to use and to scare the criminals of the country. Many criminals don't fear the judicial system. They know that they will get out in ten years if they murder someone. They are not afraid of jail or their punishment. How can we force them to stop killing or stealing if they are not afraid of the punishment we give them. Most rational men are afraid of death. They don't want to die. There are also men that don't fear death, but enjoy killing. They must be controlled, but if they are sentenced to life, they are soon free to kill again. Again, I am not saying we should kill all the men in jail and any other criminal in the world. That is not the answer either, but we must have the death penalty as an option so that they will be afraid to break the law, and to control those who don't fear death but love to break the law.

While attorneys are protecting the rights of the accused, the family of the victim often gets lost in the legal proceedings. While the accused is protected by laws and is the center of the scuffle between various lawyers, the mourning family receives little more than the media circus for their grief. They receive inadequate compensation for their loss, but with a death penalty, they can at least be assured that that person who murdered their loved one will never kill again. Capital punishment should remain in use and delivered more frequently. Only too often are death penalties reduced to life sentences or less and more condemned inmates die in death row than by execution. The effectiveness of capital punishment rests largely on the willingness of officials to use it liberally and thus exerting the power of the government. This penalty would serve as a deterrent of violent crimes and restore justice. Increased use would prod people to stay away from violent crimes. Would-be criminals would think twice before committing an offense punishable by death, and because of this, societies would gain a sense of "moral security.” As we can see from previous civilizations such as the Babylonian and Roman Empires, death penalty is effective and much more efficient than spending millions of society’s tax dollars to upkeep their prison stay. Killers who have showed themselves capable of savage brutality need to be prevented from repeating their crimes and act as a lesson to others. Capital punishment is the most effective way.

Given the benefits of capital punishment, it is hard to imagine why anyone would be against it, but there are several arguments against the death sentence that need to be addressed. Opponents of the death penalty point out that there is a possibility of wrongly executing an innocent man. Of course, there is a possibility of wrongly sending an innocent man to prison, or wrongly fining an innocent man, but they contend that because of the finality and severity of the death penalty, the consequences of wrongly executing an innocent person are much more wrong. There has never been any proof of an innocent man being executed, although there are some studies that show in a few cases, there is a possibility that someone was wrongly executed. Our judicial system takes many precautions to ensure that the rights of the innocent are protected. In order to understand this, one must look at the complex process required to convict someone of first-degree murder and get him sentenced to death. First a person is arrested and given an attorney. Evidence must be presented proving beyond a reasonable doubt that the defendant committed first degree murder. The defendant must have been in a clear state of mind. After a five to six week trial, the defendant goes on to a second trial to decide whether he deserves the death penalty. Again, a full trial is held. Defense presents evidence on why this murderer does not deserve to die. After this occurs and the murderer is sentenced to die, his case is automatically appealed to the state Supreme Court. After that, he may file a number of different appeals. Finally, about ten years later, after every legal attempt and delay tactic has been exhausted, the murderer is executed. As should be evident from this complex process, every reasonable precaution is taken to ensure that no innocent man is executed.

Although it is very unlikely that an innocent person would be executed, the question arises about whether the execution of an innocent man is a strong enough argument to abolish the death penalty. Before deciding, one must remember the lives that the death penalty saves. Repeat murderers are eliminated, and potential murderers are deterred. As mentioned earlier, one must consider the victims as well as the defendant. Is it worth it to lose forty-five innocent lives so that no innocent person is executed? This practice is considered acceptable. Risking the possibility that someone might be wrongly executed is worth it to save the lives of thousands of innocent people who might be the next victims of murder.

A second argument against the death penalty is discrimination. Eighty-two percent of all murder victims are white and thirteen percent are black. This is about a 6:1 ratio. Opponents of the death penalty, such as the NAACP, argue that the system values white lives more than black lives. If this is true, one has to wonder why whites represent fifty-five percent of those executed and blacks thirty-nine percent, when blacks have committed forty-nine percent of all murders, and whites thirty-nine percent from 1976-1994. Successful prosecutions depend on the nature of the crime and not the race of the victim. The reason that whites are overwhelmingly the victims in death row cases is that whites are overwhelmingly the victims in capital crimes. The death penalty is not racist and does not violate the cruel and unusual punishment clause.

Capital punishment has proven to have good benefits upon the country in determining the consequences that criminals deserve. This is needed to ensure the safety and moral values of society. If this is the case, there is no need for us to consider the expenses involved in the death penalty. Certainly human lives are more important, for it may easily be yours. We should not abolish capital punishment, but hold our country accountable for properly exercising the death penalty upon those who deserve it.


Works Cited


Anonymous: "Death Penalty and Sentencing Information in the United States." Internet.

"Death Penalty Statistics," North Carolina Attorney General's Office. 1997.

Nancy Jacobs, Alison Landes, and Mark A. Siegel. Capital Punishment, Cruel and Unusual?. Wylie: Information Plus, 1996.

Lowe, Wesley. "An Essay by Wesley Lowe.” Email
 
tusidanganyane. kuna watz kibao kutoka makabila ya wachagga wahaya na wanyakyusa (makabila yaliyoiona ekimu mapema) waliuwa na wengine kuikimbia nchi wakati wa Nyerere bila hata kufikishwa mahakamani.
nyerere alikuwa dictator na ndiyo maana akaongonza nchi kwa kudumisha fikra zake alizozihita sahihi "zidumu fikra sahihi za mwnyekiti"
 
Wakuu heshima mbele, nimekutana na hii katika kupitia pitia historia ya siasa na sheria zetu, kwamba according to the dataz za sheria, rais mstaafu Mwinyi, ndiye aliyeidhinisha zaidi kunyongwa kwa wananchi wahalifu kuliko marais wengine wote tuliowahi kuwa nao, yaaani kuanzia wa awamu ya kwanza I mean Mwalimu, na orodha ni kama ifuatavyo:-

1. 1961-1984 President Mwalimu Nyerere - Alinyonga wananchi 10.

2. 1985-1995 President Ali Hassan Mwinyi - alinyonga wananchi 72.

3. 1995-2005 President Ben Mkapa - Alinyonga wananchi 0.

4. 2005-2008 President Jakaya Kikwete - Amenyonga 0.

Binafsi, hii imenipa maswali mengi sana kuliko majibu, la kwanza na muhimu kwangu kuliko mengine, ni hivi kweli toka tupate uhuru miaka 45 iliyopita, kweli taifa letu limetoa wavunja sheria 82 tu wa kufikia level ya kunyongwa? Mimi nilifikiri wanapaswa kuwa wengi zaidi, I mean je hii inaweza kuwa ni sababu moja wapo ya wananchi na viongozi kutoheshimu sheria zetu au?


Source: Waziri Sheria Bunge Lililopita.
 
kama unavyojiuliza maswali mengi,hata mimi ninayo maswali. Hii sheria ya kunyonga kweli ina chembechembe za haki ndani yake?
Nakumbuka kisa cha mhanga mmoja wa sheria hii(sio mtanzania)Siku na saa ya kunyongwa kwake ilipowadia alisema hivi:
Leo hii ninauliwa kuthibitisha kwamba kuua kwa wengine ni halali kwa wengine ni haramu.
Nashawishika kusema kumuua mtu hata kama ni kwa mujibu wa sheria si haki,na kwa maana hiyo hukumu ya kumnyonga mwalifu kifo hafai.
 
Nadhani hapo swala ni utaratibu. Mahakama Kuu inafanya kazi yake ya kutoa hukumu na baada ya kumhukumu mtu kunyongwa mpaka afe hupelekwa Dodoma kwenda kusubiri mkono wa Rais, yaani Rais aidhinishe hiyo hukumu ya mtu kunyongwa mpaka akufe.

Kinachotokea sasa hivi, nadhani hizi kelele za wana harakati zimewafanya waheshimiwa wawe wazito kumwaga wino kuidhinisha kunyongwa kwa mhusika.

Ukweli ni kwamba gereza la Isanga limejaa wafungwa wanaosubiri kunyongwa lakini wahusika (Rais) hawajamwaga wino. Kwa hiyo, tofauti na hisia yako, wako wengi waliohukumiwa kunyongwa mpaka wafe lakini wakuu wa kaya hawajamwaga wino.

Kuna uwezekano kwamba huko mbele hukumu zao zinaweza kubadilishwa na kuwa vifungo vya maisha. Pia kuna uwezekano hukumu za kunyonga zikabadilishwa.

Ili kupata jibu sahihi la swali lako, Mbunge huyo alitakiwa kuuliza, je, mpaka sasa kuna watanzania wangapi walishahukumiwa kunyongwa na wanagapi kati yao bado wanasubiri ama wameishanyongwa tayari. Hapo ndiyo ungeweza kupata takwimu za watu waliopata kibano cha hukumu za kunyongwa.
 
Actually, hii sheria ya kuua tunatakiwa tuifute haraka sana, haina maana hata kidogo wala sio utanzania kabisa!
 
Sheria ya kunyonga, au kuua kwa namna nyingine, ni ya kipuuzi. It is illogical. We neither rob robbers nor rape rapists; why murder murderers?
 
Back
Top Bottom