Tanzania na Shirikisho la Urusi kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi na Kimaendeleo

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Tanzania na Shirikisho la Urusi zimekubaliana kuimarisha ushirikiano kidigitali katika sekta za Uchumi na maendeleo ili kukuza maendeleo endelevu kwa manufaa ya wanandchi wa pande zote.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mbunge), alipokutana na ujumbe kutoka Ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Uchambuzi, kutoka Ofisi ya Rais wa Urusi, Bw. Denis Agafonov.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo yenye maslahi ya pamoja, yakiwemo ya kidigitali, elimu, afya, madini, teknolojia, biashara, uwekezaji, uvuvi, uchumi wa buluu, utalii, usafirishaji, viwanda, kilimo na nishati.

Ushirikiano huo unalenga kuchochea uwekezaji endelevu, kulinda usalama wa nishati na chakula, pamoja na kukuza matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuleta maendeleo ya wananchi wa pande zote.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao hicho, Mkuu wa Msafara, Bw. Denis Agafonov, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wake, uliowezesha ujumbe huo kukutana na wadau wa sekta mbalimbali na kujadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

IMG-20261001-WA0083.jpg
IMG-20261001-WA0074.jpg
IMG-20261001-WA0073.jpg
IMG-20261001-WA0076.jpg
IMG-20261001-WA0075.jpg
IMG-20261001-WA0079.jpg
IMG-20261001-WA0085.jpg
IMG-20261001-WA0080.jpg
 
Attachments

  • IMG-20261001-WA0081.jpg
    IMG-20261001-WA0081.jpg
    124.5 KB · Views: 12
  • IMG-20261001-WA0086.jpg
    IMG-20261001-WA0086.jpg
    162.9 KB · Views: 8
  • IMG-20261001-WA0078.jpg
    IMG-20261001-WA0078.jpg
    91.5 KB · Views: 10
  • IMG-20261001-WA0077.jpg
    IMG-20261001-WA0077.jpg
    93 KB · Views: 12
  • IMG-20261001-WA0084.jpg
    IMG-20261001-WA0084.jpg
    169.6 KB · Views: 9
  • IMG-20261001-WA0082.jpg
    IMG-20261001-WA0082.jpg
    137.5 KB · Views: 11
Tanzania na Shirikisho la Urusi zimekubaliana kuimarisha ushirikiano kidigitali katika sekta za Uchumi na maendeleo ili kukuza maendeleo endelevu kwa manufaa ya wanandchi wa pande zote.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mbunge), alipokutana na ujumbe kutoka Ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Uchambuzi, kutoka Ofisi ya Rais wa Urusi, Bw. Denis Agafonov.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo yenye maslahi ya pamoja, yakiwemo ya kidigitali, elimu, afya, madini, teknolojia, biashara, uwekezaji, uvuvi, uchumi wa buluu, utalii, usafirishaji, viwanda, kilimo na nishati.

Ushirikiano huo unalenga kuchochea uwekezaji endelevu, kulinda usalama wa nishati na chakula, pamoja na kukuza matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuleta maendeleo ya wananchi wa pande zote.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao hicho, Mkuu wa Msafara, Bw. Denis Agafonov, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wake, uliowezesha ujumbe huo kukutana na wadau wa sekta mbalimbali na kujadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

View attachment 3682335View attachment 3682337View attachment 3682338View attachment 3682339View attachment 3682340View attachment 3682341View attachment 3682342View attachment 3682344
well done Tanzania and Russia:KasugaYeah:
 
Back
Top Bottom