SoC02 Tanzania na uchumi

SoC02 Tanzania na uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

KHALFAN CHETU

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
10
Reaction score
10
Kwa kutumia Upeo wa kati wa Ufahamu kuhusu Uchumi kwa Mujibu wa tunaowaita Wabobezi wa Masuala ya Uchumi, Tunautafsiri Uchumi kama ifuatavyo,UCHUMI ni Mahusiano yaliyopo kati ya Uzalishaji, Biashara na Fedha zinazopatikana.

Tafsiri hiyo ni kwamujibu wa Kamusi ya OXFORD, TOLEO LA SITA. Lakini kwa kutumia Upeo wa Juu unaohitaji Uzoefu zaidi kuliko Nadharia, UCHUMI ni uwezo wa hali ya TAIFA/MWANADAMU kujitosheleza kwa kiwango kikubwa kupitia RASILIMALI NGUVU(..Akili na MWILI..), MALI ASILI na MAZINGIRA, Ambapo kwa Mtu mmoja mmoja inahitajika Afya, Maarifa na Fursa kama Nguzo za Uchumi wake, ilihali Kitaifa itahitaji Sera Bora, Tafiti za Kutosha, Miundombinu na Uzalendo kama Nguzo Mama za Uchumi wa Nchi.

Kwa kuyaelewa hayo, tutaweza kutambua kuwa Uchumi upo ndani ya PEMBE TATU kuu sawa inayojengwa na MTU,TAIFA na UCHUMI wenyewe. Uchumi wa MTU unatokana na Shinikizo la Mahitaji yake kwa Msaada wa Shauku ya Kujitosheleza aliyonayo,ilihali Uchumi wa TAIFA unatokana na Mahitaji ya Kikanda kwa Msaada wa Mifumo na Usimamizi wa Serikali. Ieleweke kuwa Uchumi wa Mtu unaweza usitegemee UCHUMI WA TAIFA,Lakini Uchumi wa Taifa ukautegemea moja kwa moja Uchumi wa Mtu. Na Uchumi unaweza kuwepo pasina FEDHA,Ila FEDHA bila Uchumi ni kitendawili.

Ndio maana hata kabla ya Ujio wa Matumizi ya Fedha,Uchumi wa Mwanadamu ulitazamwa kupitia Shughuli alizokua akizifanya, Mali alizozimiliki na Urahisi uliopo katika kujipatia Mahitaji yake Muhimu. Na Uchumi wa Mataifa ulipimwa kwa Mazingira Rafiki ya Maeneo yaliyoruhusu shughuli kama Uwindaji, Uokotaji(..Gathering..),Uvuvi na mambo kama Usalama na kadhalika.

Tukija sasa kwenye Dhana Halisi ya UCHUMI WA TANZANIA baada ya Utangulizi wenye Muktadha wa Tafsiri pana ya Uchumi, Tunapata kuelewa kuwa Mifumo na Sera za Taifa kwenye maswala ya Kiuchumi haina Afya kwa Mustakabali mwema wa Taifa letu kwasababu Serikali na Taifa kwa Ujumla inaitazama FEDHA kama MTAMBO MAMA wa Mashine iitwayo Uchumi ndio maana tukotayari kupokea FEDHA kidogo na MISAADA huku tukiyaachilia MADINI.

Lakini kama haitoshi tupo tayafi kuziruhusu BIDHAA zinazoweza kuhatarisha Afya ya Binadamu ambayo ni kati ya Nguzo za za Uchumi wa Mtu mmoja mmoja ili tu Serikali iongeze MAPATO ya Taifa. Mfano; Bidhaa kama Kuku wa Madoli,Vinywaji vyenye Kemikali,Mayai ya Kizungu,Sigara na Pombe na bidhaa zenginezo. Na hiyo inatoa Taswira ya kwamba hapa Tanzania,Uchumi unatafsirika kupitia Nadharia zinazotazamwa kuwa ni za Kisomi zisizo na Uhalisia kamili kwasababu zimetolewa na kukubaliwa na Watu wenye Upeo wa Kati wa kutathmini Mambo.

NJIA KADHAA ZA KUKUZA UCHUMI WA NCHI YA TANZANIA NI:-
(1) Ili kuukuza Uchumi wa Taifa la Tanzania kwanza ni lazima tuhakikishe tunatengeneza Mazingira Rafiki kwa Watu kujipatia Mahitaji yao ya Msingi pasina Utegemezi nje ya Jamii tuliyopo. Na hapo ndipo mwanzo wa kuutazama Uchumi si tu kama Kiwango cha Fedha kwenye Benki kuu bali kama Uzalishaji toshelevu wa Mazao ya Chakula,Ufugaji Bora,Ulinzi na Usalama,Afya za Watu,Utamaduni na Maadili pamoja na Miundombinu.

(2) Serikali ihakikishe Mtaala Wa Elimu unatoa Ujuzi kwa Watoto na Vijana ngazi ya Awali mpaka Chuo ambao utaendana na Mazingira pamoja na Mahitaji ya Jamii yetu ya Kitanzania. Kwasababu Uchumi wa Nchi unajengwa na Watu.

(3) Pia, Serikali ihakiishe inalinda na kusaidia kuboresha Afya za Watu wake, kwasababu FEDHA/UCHUMI wa Taifa hauna Maana kama Afya za Watu ni mbovu, hivyo Serikali haipaswi kukubali kila Bidhaa au Mambo yanayotoka Nje ya Jamii yetu ili kuwalinda Raia wake dhidi ya Athari za Kimwili na Kisaikolojia.

Kwasababu hata Adam na Hawa, walipewa Afya kama Mtaji namba Moja,Maliasili kama Mtaji namba Mbili kisha Maarifa kama mtaji namba Tatu,Na hiyo ndio haswa maana ya Uchumi Wa Mtu wenye Taswira ya Nguvu, Umiliki na Elimu. Kwahiyo Fedha isiifanye Serikali kuyaharibu Maarifa,Afya na Maliasili kama ambavyo Wanyama na Madini yanavyosafirishwa kiholela.

(4) Pia Serikali ni lazima ihakikishe kuwa Upatikanaji wa Ajira kwa Vijana waliohitimu ni toshelevu.

(5)Serikali inapaswa ihakikishe pia inatengeneza na kuunda SHERIA zenye Umadhubuti dhidi ya Wafanya biashara ili iendeshe Uchumi kwa Mantiki zaidi kuliko kwa mihemko ya kihisia ili kuondoa Migogoro ya Wananchi dhidi ya Serikali na Migogoro Nafsi itakayowatafuna Wananchi. Mfano; Swala la Wamachinga limeendeshwa Kihisia zaidi kuliko Kimantiki kwasababu kama NIA ni kukuza Uchumi kwanini iwe halali kuwaondoa Wajasiriamali wadogo hata wale walio Nje ya Miji kwenye maeneo yao ya biashara...? Je kama huyu mfanyabiashara haukumtengenezea Mazingira rafiki ya Soko la bidhaa wala kumpatia Mtaji,inawezekanaje Umtoe Nje ya Mstari wake wa Utafutaji kwa kisingizio cha kuyapendezesha MAJIJI....?. Ifike Mahala Serikali ielewe kuwa Uchumi Imara unajengwa na Wanachi wenyewe na si Muwekezaji.

(6)Serikali pia inapaswa ihakikishe kuwa Uzalendo unaonekana kupitia Usimamizi na Ufuatiliaji wa namna Watumishi wanavyowajibika katika Sekta mbalimbali kwa Uweledi lakini pia kuhakikisha kuna Udhibiti wa Rasimali za Ndani na Upotevu wa Fedha za umma kwenye Maeneo mbalimbali ya Utumishi. Kama vile kwenye Sekta ya Utalii dhidi ya Ujangili na Usafirishaji Wanyama Pori.

(7)Lakini pia jambo la msingi ambalo Serikali inaweza kulifanya ni kutengeneza Utaratibu ikiwa kabisa wanaona wameshindwa kumaliza Tatizo la Ajira,Ijaribu kutengeneza Miradi tofautitofuati kisha kila Mradi waukabidhishe kwa Wahitimu watano watano ili wauendeshe kwa Usimamizi na Uangalizi wa Serikali yenyewe mpaka Miradi itakapoanza kuzaa Matunda.

Mfano; Serikali inaweza kutenga Miliono 5 mpaka 10 kwa kila kikundi cha Watu 10 kufungulia Mradi/Biashara ya pamoja kama Usafirishaji wa mazao,Mifugo,kufungua Migahawa,Biashara za Usafirishaji, Huduma ya kuosha Magali,Huduma ya kusagisha Nafaka,Magari na Mashine za kulimia na kadhalika. Kisha Faida itakayokua ikipatikana itumike kama Marejesho ya Mkopo kidogo kidogo kwa Serikali na nyengine Iwanufaishe Wanakikundi na Utanuzi wa mradi mpaka Deni litakapokwisha na kumilikishwa Mradi moja kwa moja chini ya Usimamizi wa Serikali kwa Asilimia 100. Naamini kama ambavyo imewezekana kuwapatia Vijana hawa Mikopo ya Chuo basi hata mikopo ya kufanyia Miradi pia inawezekana kabisa wakapatiwa kama Serikali ikiamua.

Kama ambavyo Uchumi bila Watu ni Fumbo, hata Sera zisizo na Uhalisia hugeuka Gumzo, hivyo Serikali ihakikishe inaweka Mifumo wezeshi kwa kila Eneo la wazalishaji na kila Eneo la Wajasiriamali. Hiyo ni kwasababu, Mustakabali wowote ule katika Taifa unatokana na Umadhubuti wa Viongozi au Udhaifu wao kupitia Usimamizi na Maamuzi wanayoyatoa.

2022-08-14 16.49.36.jpg
2022-08-14 16.49.36.jpg
 
Upvote 0
Wakipatikana viongozi bora wanaojali maslahi ya nchi na sio maslahi yao binafsi basi uchumi ni rahisi kukua
 
Wakipatikana viongozi bora wanaojali maslahi ya nchi na sio maslahi yao binafsi basi uchumi ni rahisi kukua
Kabisa yani,Viongozi wasio na Ubinafsi huwapiga Raia Mihuli ya Upendo na Uzalendo hata kwenye Vipindi Vigumu
 
Back
Top Bottom