Tanzania na Uganda ndio nchi pekee zilizopigana vita Africa

Tanzania na Uganda ndio nchi pekee zilizopigana vita Africa

Sangarara, hakuna vita iliyowahi kupiganwa kati ya Tanzania na Uganda. hakuna kabisa na tusipotoshane hapo. Wewe tatizo lako maneno yako mia ya uwongo unachomeka maneno maneno mawili ya ukweli. Naomba usahihishe, Vita unayozungumzia ilikuwa kati ya Tanzania dhidi ya Idd Amin Dada na siyo vita kati ya Tanzania na Uganda. Umesema, waganda hawajawahi kupigana vita dhidi ya Tanzania sasa kwa nini unaendelea kupotosha? kwa usahihi ungesema JKN alipotangaza vita hakusema anawatangazia vita waganda, hakusema waganda wamemfanyia chochote kibaya bali alisema atamg'oa Idd Amin Dada. Wakumbuka aliposema, "sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo na uwezo wakumpiga tunao"? Ukirejea Enzi hizo za vita waweza baini kuwa lengo la vita ilikuwa kumuondoa Idd Amin madarakani na kimsingi asingekimbia angeuawa huyu Amini wetu. Naamini waweza rekebisha kumbukumbu na historia yako sasa. Lakini hii vita ya kumpiga Amin ilitugharimu sana. Tatizo nyie waTz mnashabikia ya wengine huku kwenu kunaungua.
 
Back
Top Bottom