Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini.
Waziri mweny zamana anasemaje ajatoa malalamiko yoyote

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ninakubaliana na wazo hili.

Hakuna sababu muhimu ya kuendelea kuwapapatikia hawa watu.

Dunia inavyogeuka sasa, utegemezi kwao hautakuwa wa lazima sana, kama China, India, Urusi na mataifa mengine yataamua kuachana na mifumo inayotumiwa na hawa wahuni kuendelea kutawala dunia kiuchumi. Teknologia sasa imeenea, haihodhiwi tena na haya mataifa machache.
Mzungu sio kwamba anasema ukweli kuhusu mazingira ila mbinu yake anataka iwe chini yake ili atuburuze kama ilivyo kawaida yao kueneza fitna hadi vita
 
Hawa wanaokuja kujenga hilo bomba wawili wanatokea Ulaya. Mmoja EU mwingine UK sasa wangewauliza kwanza hao halafu wamwendee mchina waulize ni kwa vipi mazingira yatapona.
Mdachi alipoharibu maji ya watu wa Nigeria ya kusini alifanywa nini na je, Nigeria ilisitisha kuuza mafuta yake? Je nigeria iliongea chochote?

Uharibifu wa mazingira tumeufanya sisi kwa mno kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Tuanze sisi bila kusikiliza hao wengine maana hata ukiwaita majina, wenyewe mpaka walipofikia wamepigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakachoka.
Walitumia mkaa wakachoka ndo wakagundua mafuta kwa waarabu ndo ahueni yao na Mwingereza ndo aligundua hayo mafuta na tunaona mwarabu anavyotamba duniani.
Hakuna mwaribifu wa mazingira kama USA je wamemfanya nini?
Aisee hakika umesema ukweli

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NIPALE MUNGU ANAPOKULIPA KWA ULIYOFANYA..! MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI , jamaa lilisema mtanikumbuka.
Mabaado.🤣🤣🤣 nasema Nabadoo! Mpaka mtaaibika.
Korona chali..
Kufoka fokea watu wazima..chali.
Fedha za zuruma..chali
Inchi inakopesheka..chali
Deni himilivu..chali
Tumekusanya zaidi...chali
Chanjo... chali
Dipromasia.. chali.
Kabudi.... chali
Rukuvi....chali
Pole pole...chali

Nabado. Mpaka twende tukatubu chato badara ya kunya juu ya kaburi🤣🤣
 
Sisi tupo kwetu na wao wapo kwao hivyo kupangiana nini cha kufanya ni upotofu usiohimilika.
Wao kwao wana viwanda vikubwa vya kila aina vyevye level ya juu ya water contamination na air pollution vinavyochafua hali ya hewa dunia nzima na nuclear plants ambazo ni critically catastrophic. Kama hoja ni uchafuzi wa mazingira basi ilibidi sisi ndio tuwakemee wao na sio wao watukemee sisi.
Ninachoona hapa wana jambo lao ambalo wanaona sisi tukianza huu mkakati basi wao wataathirika pakubwa, ni kama kilichotokea Libya.
Na naimani sisi kama Tanzania hatutosikiliza na hatutoruhusu hilo jambo kutokea.

Hypocrisy at best.
 
Salaam Wakuu,

Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.

Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania.

View attachment 2358292

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.

Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Sasa watu watamuelewa Magufuli alimaanisha Nini aliposema vita ya UCHUMI NI MBAYA tusubiri ujenzi wa hoja tusikie,maana watu weusi tuna tabia ya kujisahaulisha na hata tusijue kwamba Mzungu hajawahi penda maendeleo ya watu weusi.Na hii Sasa imedhihirika waziwazi.
 
Sisi tupo kwetu na wao wapo kwao hivyo kupangiana nini cha kufanya ni upotofu usiohimilika.
Wao kwao wana viwanda vikubwa vya kila aina vyevye level ya juu ya water contamination na air pollution vinavyochafua hali ya hewa dunia nzima na nuclear plants ambazo ni critically catastrophic. Kama hoja ni uchafuzi wa mazingira basi ilibidi sisi ndio tuwakemee wao na sio wao watukemee sisi.
Ninachoona hapa wana jambo lao ambalo wanaona sisi tukianza huu mkakati basi wao wataathirika pakubwa, ni kama kilichotokea Libya.
Na naimani sisi kama Tanzania hatutosikiliza na hatutoruhusu hilo jambo kutokea.

Hypocrisy at best.
Akina January makamba walitumwa na hao hao wenye pua ndefu kipindi cha ujenzi wa mradi wa Umeme wa Julius Nyerere power plant Hadi Magu akaamua kumtumbua mtu.Leo wamekija kivingine.
 
Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini.
Mungu wabariki Wazungu
 
Unaikumbuka gesi ya Mtwara ambayo watu waliuawa na wajawazito kutumbuliwa mimba ? hiyo gesi uliwahi kuiona ?
Chozi la mnyonge malipo kwa Mungu baba. Unakumbuka korona ilivyowatafuna!? Bado hawajastuka subiri waendeleze kiburi, wivu na umwamba wao, rungu lingine linawasubiri.
 
mshana jr nikajua umekuja na suluhisho lakini naona nawewe umekuja na kebehi za ovyo ! Kwanza bunge letu sio la mchongo ni bunge halali, kama nilamchonga hamia hata kenya usiitusi nguo unayolalia
 
Aisee hakika umesema ukweli

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wasiwasi wa watu wa EU ni kwamba sisi ndo tuliokuwa tumebaki na viumbe ambao wametoweka kwenye ulimwengu wa sehemu nyingine nyingi bali wamebaki kwenye michoro na carves.
Uliona tulipojenga barabara ya kutoka Rusahunga kwenda Bukoba wanyama waliokuwa wanapita toka magharibi kwenda mashariki waliacha sababu ya jinsi barabara ilivyotenga pori. Tulizoea kupita tunaona twiga na tembo wakipita sasa hivi huwezi sababu ya korongo kubwa hawawezi kupanda au kushuka. Hiyo ndo sababu kubwa ambayo hata mimi ninawasi wasi nayo.
Kama mradi wa ujenzi wa bomba atapewa mchina basi ujue wanyama watatengwa maana hatajali ikologia ya nchi. Tutaweza kukosa mapato tokana na watalii ingawa isiumize wengi maana hatufahamu ni kiasi gani utalii unaiingizia nchi na mwananchi wa kawaida anafaidikaje.
 
Akina January makamba walitumwa na hao hao wenye pua ndefu kipindi cha ujenzi wa mradi wa Umeme wa Julius Nyerere power plant Hadi Magu akaamua kumtumbua mtu.Leo wamekija kivingine.
Makamba, Nape, Na Yule mzee aliyesema umeme wa maji umepitwa na wakati, ni wakupimwa utendaji wao wa akili
 
Wasiwasi wa watu wa EU ni kwamba sisi ndo tuliokuwa tumebaki na viumbe ambao wametoweka kwenye ulimwengu wa sehemu nyingine nyingi bali wamebaki kwenye michoro na carves.
Uliona tulipojenga barabara ya kutoka Rusahunga kwenda Bukoba wanyama waliokuwa wanapita toka magharibi kwenda mashariki waliacha sababu ya jinsi barabara ilivyotenga pori. Tulizoea kupita tunaona twiga na tembo wakipita sasa hivi huwezi sababu ya korongo kubwa hawawezi kupanda au kushuka. Hiyo ndo sababu kubwa ambayo hata mimi ninawasi wasi nayo.
Kama mradi wa ujenzi wa bomba atapewa mchina basi ujue wanyama watatengwa maana hatajali ikologia ya nchi. Tutaweza kukosa mapato tokana na watalii ingawa isiumize wengi maana hatufahamu ni kiasi gani utalii unaiingizia nchi na mwananchi wa kawaida anafaidikaje.
Mbona wao hawakujali kuhusu wanayama wakati wanajiletea maendeleo, Afrika sio mbuga ya wanyama, kuna binadamu wanaotaka maendeleo pia
 
Back
Top Bottom