Tanzania na uganda zasaini makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa

Tanzania na uganda zasaini makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Bukoba

Tanzania na Uganda zimetia saini makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili.
Snapinsta.app_466356618_1076447693718941_6022671571979826944_n_1080.jpg
Makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa mwisho wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Wataalamu (JTC) kati ya nchi hizo kilichokuwa na lengo la kujadiliana namna ya kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda.

Utiaji saini makubaliano hayo ulifanyika katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kati ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansour na Bi Jacqueline Banana Wabyona ambaye ni Mkuu wa ujumbe wa wataalamu kutoka nchini Uganda.
Snapinsta.app_466368375_1738686083651180_4881061320577177669_n_1080.jpg

Snapinsta.app_466108055_1082015196457847_1825406873991265971_n_1080.jpg
Wakati wa utiaji saini makubaliano hayo, viongozi wote wawili walionesha kuridhishwa na namna wataalamu wa nchi hizo mbili walivyoshiriki majadiliano ya pande hizo mbili na hatimaye kufanikisha kusainiwa kwa makubaliano kati ya Tanzania na Uganda.

Kikao cha Kamati ya pamoja cha wataalamu wa Tanzania na Uganda (JTC) kilianza tarehe 5 Novemba 2024 mkoani Kagera ambapo kimejadili mambo mbalimbali ha uiamarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo.

Mpaka wa Tanzania na Uganda una urefu wa takriban km 397.8 ambapo kati ya hizo km109 ni nchi kavu , km 42.8 ni sehemu ya mto kagera na km 246 ni sehemu ya ziwa victoria.

Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Afrika kuwa, ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za Afrika iwe imeimarishwa.
 
Back
Top Bottom