Tanzania na Uganda zatajwa kushiriki majaribio ya chanjo ya HIV

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
905
Reaction score
1,540
Tanzania na Uganda zimetajwa kuwa kati ya nchi nne za Afrika kushiriki kwenye majaribio ya chanjo ya virusi ya UKIMWI, ikiwa ni sehemu ya jaribio la kwanza barani Afrika kujaribu chanjo mbili mpya dhidi ya VVU. Imearifiwa kuwa tayari majaribio yameanza wiki hii nchini Uganda na Afrika Kusini. Kwenye majaribio hayo chanjo mbili za mchanganyiko zitatolewa ili kuona kama zinaweza kuweka kinga kwa watu walio katika hatari ya kuambukizwa. Moja ya chanjo hiyo itakuwa ni kidonge cha kila siku.

Chanjo hizo mbili zimejaribiwa kwa usalama katika majaribio ya kimatitabu yaliyopita barani Afrika, Ulaya na Amerika. Kwenye majaribio ya sasa zaidi ya watu 1,600 wenye umri kati ya umri wa miaka 18 na 40 wanatarajiwa kushiriki katika majaribio yatakayofanyika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo nchini Uganda, Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini. Utafiti huo unafadhiliwa na Ushirikiano wa Majaribio ya kimatibabu ya Nchi za Ulaya na kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya.

Chanzo cha taarifa: Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa

Mwisho nimeongeza PDF ya Utafiti wa PrEPVacc kwenye bandiko hili; ambayo ni muhimu kufungua na kusoma.
Screenshot 2020-12-21 at 07.58.01.png

===============

Utafiti huu wa PrEPVacc ni nini?

PrEPVacc ni vitu viwili:

Ni kupima kama aina mbili za mchanganyiko wa chanjo ya majaribio zinaweza kukinga dhidi ya VVU. Aina zote hizi mbli za mchanganyiko tayari zilishajaribiwa kwenye tafiti za kitabibu na zimeonyesha usalama wake na kwa wakati huo huo, inapima aina mpya ya dawa kinga ya VVU (PrEP) dhidi ya dawa kinga ya VVU (PrEP) inayotumika sasa.

Utafiti uko wapi?

Utafiti huu unapangwa kufanyika kwenye vituo vitano katika nchi 4: Masaka, Uganda; Mbeya, Tanzania; Dar-es-Salaam, Tanzania; Maputo, Msumbiji na Durban, Afrika Kusini.

Chanjo ya VVU ni nini?

Chanjo inafundisha mwili kujikinga dhidi ya maambukizi fulani au kupigana na ugonjwa kwaajili ya kukuweka na afya njema. Dunia bado haina chanjo inayo kinga VVU iliyosajiliwa. Ili kutengeneza chanjo, watafiti wanahitaji kuipima kwa watu, ili kugundua kama itaweza kusaidia kukinga au kupigana na VVU. Inatolewa kwa sindano.

Dawa Kinga ya VVU ya Kumeza (Oral PrEP) ni nini?

Dawa Kinga ya VVU (PrEP) ni matumizi ya dawa za kufubaza VVU kwa watu wasio na maambukizi ya VVU ili kupunguza hatari yao ya kupata maambukizi ya VVU. Dawa Kinga ya VVU imeonyesha kuzuia VVU na inapatikana duniani kama kidonge.

Utatoa mchango gani kwa kushiriki?

Kuna njia nyingi za kuzuia VVU, ila kila mwaka maambukizi mapya yanaendelea kuripotiwa. Ushiriki wako na jitihada zako zitasaidia kujibu maswali mawili kwa taarifa ambazo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi mapya kwenye jamii yako.

• Tutaweza kusema iwapo utengenezwaji wa aidha ya mchanganyiko miwili ya chanjo ya kuzuia VVU inafaa au la

• Tutaweza kusema kama aina mpya ya dawa kinga ya VVU (PrEP) inakubalika, ni salama na ina ufanisi kama aina ya dawa kinga ya VVU ya kumeza inayotumika kwa hivi sasa na wanawake pamoja na wanaume

Wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 18–40 wenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU wanaalikwa kushiriki kwenye utafiti wa PrEPVacc.

Unaweza kushiriki kama:

• Una afya njema

• Una umri wa miaka 18–40 siku ya mchujo

• Una utayari na una uwezo wa kutoa ridhaa kushiriki kwenye utafiti huu

• Una utayari na unaweza kuja katika mahudhurio yote na kufanyiwa kipimo cha VVU na kutoa damu, mkojo na sampuli nyingine kwa wakati zinapohitajika

Afya na haki za washiriki zitalindwa vipi?

Wakati wote tutawapa washiriki taarifa kamili kuhusu utafiti kabla mshiriki hajajiunga kwenye utafiti, ili uweze kutupa ridhaa ya kushiriki.

Washiriki wana haki ya kujitoa kwenye utafiti wakati wowote.

Kipindi cha utafiti, wafanyakazi wa kliniki watawafuatilia washiriki ili kuhakikisha kwamba chanjo na dawa kinga dhidi ya VVU hazisababishi matatizo yoyote ya kiafya.

Wafanyakazi wa utafiti pia, watawasaidia washiriki kuripoti matatizo yoyote ya kijamii ambayo wanapata kutokana na kuwepo kwenye utafiti.

Usalama wa washiriki upo chini ya uangalizi wa timu inayofuatilia usalama na bodi ya kujitegemea ya ufuatiliaji wa usalama ambayo mara kwa mara huangalia taarifa za kiafya za washiriki na kuamua kama ni salama kuendelea na chanjo na dawa kinga ya VVU.

Kamati ya maadili ya kitaasisi inapitia na kufuatilia mpango wa utafiti kwa kila kituo kinachofanya utafiti huu, pamoja na taarifa inayotolewa kwa watu kuhusu utafiti huu, maendeleo ya utafiti, na matatizo ya kiafya ya washiriki. Kamati hii ya maadili pia huangalia kama haki za washiriki zinaheshimiwa.

Kila kliniki ya utafiti ina bodi ya ushauri wa jamii. Wajumbe wake ni watu wa mahali hapo hapo ambao wanashauri watafiti na kuleta wasiwasi na masilahi ya jamii na washiriki wa utafiti kwa watafiti.
 
Attachments

Naona wazee wa pin kali wanavyofurahia hii habari
Habari za namna hii Zipo tangu miaka ya 70 na zitaendelea kuwepo kwasababu NI MIRADI YA WATU !

Na atakayegundua Tiba Atauwawa haraka sana kwasababu HIV project ni Business! (Biashara)
Unadhani wanasayansi miaka yote hiyo wakiamua wanashindwa?
Jibu ni kwamba hawawezi coz Biashara
 
Kama kweli vile
 
Nimekuelewa. Nikikumbuka habari za Thabo Mbeki kupinga kupumbazwa na ugonjwa huu na yule Rais wa Gambia aliyegundua dawa na kilichofuata kwa waafrika hawa.
 
Habari za namna hii Zipo tangu miaka ya 70 na zitaendelea kuwepo kwasababu NI MIRADI YA WATU !

Na atakayegundua Tiba Atauwawa haraka sana kwasababu HIV project ni Business! (Biashara)
Unadhani wanasayansi miaka yote hiyo wakiamua wanashindwa?
Jibu ni kwamba hawawezi coz Biashara
Sijui kama ni kweli au si kweli, sio lengo langu kupinga.. ila tambua na hili pia;

Virusi ni changamoto mno kupata chanjo au dawa kwakuwa chanjo au dawa hutengenezwa kudhibiti umbo flani la kimelea(bakteria,kirusi au fangas) lakini tofauti na bakteria na fangas, virusi vyenyewe hujibadili umbo mara kadhaa kwa sekunde au kuzalisha virusi tofauti(variants) mamilioni kwa sekunde. Itaandaliwa dawa ya kumdhibiti kirusi wa umbo hili, kabla hujapewa tayari ana umbo jingine!

Hali ni hiyo hiyo kwa virusi vya Mafua(Influenza) na Korona(Juzi nchini Uingereza kumegunduliwa umbo jipya(new variant) ya korona na kuzua hofu kuwa chanjo iliyogunduliwa inaweza kuwa kazi bure na nchi nyingi zimeanza kuzuia wasafiri kutoka Uingereza sababu ya watoto wapya wa korona kuenea kwa kasi Uingereza!)
 
Tangu lini pre-exposure prophylaxis (PrEP) ikawa chanjo, acha kulisha watu matango pori basi. Hizo ni dawa ambazo wanameza wale ambao wako kwenye risk kubwa ya kuambukizwa, mfano ma-barmedi ili wasipate dalili za ugonjwa.
 
Mswahili kaambiwa kuna chanjo ya Corona kapuuza, lakin kwa uroho wa vitu vitamu kaambiwa kuna chanjo ya Ukimwi kafurahia kwa kuwa anajua kapata '9 December' yake ya kufurahia ngono
 
Nimeishia kusoma hapo waliposema moja ya chanjo hiyo ni vidonge vya kunywa kila siku.

We all gonna die someday.
Kutokana na maelezo ya mtoa mada ni kuwa chanjo itawahusu walio kwenye hatari zaidi,sasa kama wewe una mke na umetulia utameza kinga ya nini?ila kama bado uko kwenye list ya walio kwenye hatari ya kupata maambikizi,huwezi kukwepa kidonge kila siku...
 
Tanzania na Uganda zimetajwa kuwa kati ya nchi nne za Afrika kushiriki kwenye majaribio ya chanjo ya virusi ya UKIMWI, ikiwa ni sehemu ya jaribio la kwanza barani Afrika kujaribu chanjo mbili mpya dhidi ya VVU. Imearifiwa kuwa tayari majaribio yameanza wiki hii nchini Uganda na Afrika Kusini. Kwenye majaribio hayo chanjo mbili za mchanganyiko zitatolewa ili kuona kama zinaweza kuweka kinga kwa watu walio katika hatari ya kuambukizwa. Moja ya chanjo hiyo itakuwa ni kidonge cha kila siku.

Chanjo hizo mbili zimejaribiwa kwa usalama katika majaribio ya kimatitabu yaliyopita barani Afrika, Ulaya na Amerika. Kwenye majaribio ya sasa zaidi ya watu 1,600 wenye umri kati ya umri wa miaka 18 na 40 wanatarajiwa kushiriki katika majaribio yatakayofanyika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo nchini Uganda, Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini. Utafiti huo unafadhiliwa na Ushirikiano wa Majaribio ya kimatibabu ya Nchi za Ulaya na kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya.

Chanzo cha taarifa: Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa

Mwisho nimeongeza PDF ya Utafiti wa PrEPVacc kwenye bandiko hili; ambayo ni muhimu kufungua na kusoma.
View attachment 1655789

===============

Utafiti huu wa PrEPVacc ni nini?

PrEPVacc ni vitu viwili:

Ni kupima kama aina mbili za mchanganyiko wa chanjo ya majaribio zinaweza kukinga dhidi ya VVU. Aina zote hizi mbli za mchanganyiko tayari zilishajaribiwa kwenye tafiti za kitabibu na zimeonyesha usalama wake na kwa wakati huo huo, inapima aina mpya ya dawa kinga ya VVU (PrEP) dhidi ya dawa kinga ya VVU (PrEP) inayotumika sasa.

Utafiti uko wapi?

Utafiti huu unapangwa kufanyika kwenye vituo vitano katika nchi 4: Masaka, Uganda; Mbeya, Tanzania; Dar-es-Salaam, Tanzania; Maputo, Msumbiji na Durban, Afrika Kusini.

Chanjo ya VVU ni nini?

Chanjo inafundisha mwili kujikinga dhidi ya maambukizi fulani au kupigana na ugonjwa kwaajili ya kukuweka na afya njema. Dunia bado haina chanjo inayo kinga VVU iliyosajiliwa. Ili kutengeneza chanjo, watafiti wanahitaji kuipima kwa watu, ili kugundua kama itaweza kusaidia kukinga au kupigana na VVU. Inatolewa kwa sindano.

Dawa Kinga ya VVU ya Kumeza (Oral PrEP) ni nini?

Dawa Kinga ya VVU (PrEP) ni matumizi ya dawa za kufubaza VVU kwa watu wasio na maambukizi ya VVU ili kupunguza hatari yao ya kupata maambukizi ya VVU. Dawa Kinga ya VVU imeonyesha kuzuia VVU na inapatikana duniani kama kidonge.

Utatoa mchango gani kwa kushiriki?

Kuna njia nyingi za kuzuia VVU, ila kila mwaka maambukizi mapya yanaendelea kuripotiwa. Ushiriki wako na jitihada zako zitasaidia kujibu maswali mawili kwa taarifa ambazo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi mapya kwenye jamii yako.

• Tutaweza kusema iwapo utengenezwaji wa aidha ya mchanganyiko miwili ya chanjo ya kuzuia VVU inafaa au la

• Tutaweza kusema kama aina mpya ya dawa kinga ya VVU (PrEP) inakubalika, ni salama na ina ufanisi kama aina ya dawa kinga ya VVU ya kumeza inayotumika kwa hivi sasa na wanawake pamoja na wanaume

Wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 18–40 wenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU wanaalikwa kushiriki kwenye utafiti wa PrEPVacc.

Unaweza kushiriki kama:

• Una afya njema

• Una umri wa miaka 18–40 siku ya mchujo

• Una utayari na una uwezo wa kutoa ridhaa kushiriki kwenye utafiti huu

• Una utayari na unaweza kuja katika mahudhurio yote na kufanyiwa kipimo cha VVU na kutoa damu, mkojo na sampuli nyingine kwa wakati zinapohitajika

Afya na haki za washiriki zitalindwa vipi?

Wakati wote tutawapa washiriki taarifa kamili kuhusu utafiti kabla mshiriki hajajiunga kwenye utafiti, ili uweze kutupa ridhaa ya kushiriki.

Washiriki wana haki ya kujitoa kwenye utafiti wakati wowote.

Kipindi cha utafiti, wafanyakazi wa kliniki watawafuatilia washiriki ili kuhakikisha kwamba chanjo na dawa kinga dhidi ya VVU hazisababishi matatizo yoyote ya kiafya.

Wafanyakazi wa utafiti pia, watawasaidia washiriki kuripoti matatizo yoyote ya kijamii ambayo wanapata kutokana na kuwepo kwenye utafiti.

Usalama wa washiriki upo chini ya uangalizi wa timu inayofuatilia usalama na bodi ya kujitegemea ya ufuatiliaji wa usalama ambayo mara kwa mara huangalia taarifa za kiafya za washiriki na kuamua kama ni salama kuendelea na chanjo na dawa kinga ya VVU.

Kamati ya maadili ya kitaasisi inapitia na kufuatilia mpango wa utafiti kwa kila kituo kinachofanya utafiti huu, pamoja na taarifa inayotolewa kwa watu kuhusu utafiti huu, maendeleo ya utafiti, na matatizo ya kiafya ya washiriki. Kamati hii ya maadili pia huangalia kama haki za washiriki zinaheshimiwa.

Kila kliniki ya utafiti ina bodi ya ushauri wa jamii. Wajumbe wake ni watu wa mahali hapo hapo ambao wanashauri watafiti na kuleta wasiwasi na masilahi ya jamii na washiriki wa utafiti kwa watafiti.
Meko akiiona hii ataifuta.

“Au nasema uwongo ndugu zangu????”
 
Ushahidi kama weka hapa
Habari za namna hii Zipo tangu miaka ya 70 na zitaendelea kuwepo kwasababu NI MIRADI YA WATU !

Na atakayegundua Tiba Atauwawa haraka sana kwasababu HIV project ni Business! (Biashara)
Unadhani wanasayansi miaka yote hiyo wakiamua wanashindwa?
Jibu ni kwamba hawawezi coz Biashara
Weka hapa ushahidi dmkali au dhana za kufikirika ?
 
Back
Top Bottom