Tanzania na Uganda zatajwa kushiriki majaribio ya chanjo ya HIV

Sawa ! Lakini utafiti wa kwetu tumefanyia kazi kwa kiwango kipi ?
MFANO NI JINSI NIMR WALIVYOTENGENEZA DAWA LISHE YAKUPAMBANA NA MATATIZO YA CORONA NA "KUPATA SHUHUDA NYINGI"

Tukatae na hili, tutumie tiba za asili.

Tujali vya kwetu.
 
kwaio katika mwaka unameza vidonge 365? biashara tu hio
 
Ile chanjo waliyochanjwa polisi iliishia

Kwa ufupi jitihada hizi utafiti wa kinga zilianza mwishoni mwa miaka ya 1980 kwenye nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako chanjo mpya ya majaribio ilianza 1987. Chanjo iliyofanyiwa utafiti na kujaribiwa ilikuwa HIV-1 ambayo ni mkakati wa gharama nafuu zaidi kwa kinga na udhibiti wa maambukizo ya HIV-1 duniani na Tanzania kwa jumla. Tangu wakati huo zaidi ya aina 30 tofauti za chanjo zimejaribiwa zaidi ya mara 100 katika awamu I/II kwa kushirikisha watu wengi wa kujitolea wasio na maambukizo ya VVU. Utengenezaji wa chanjo hufanyika kwa awamu. Kuna awamu moja hadi tatu na nchi zimo kwenye awamu tofauti.

Nchini Tanzania kuna maeneo matatu ya mradi wa kutayarisha majaribio ya kitabibu ya chanjo ambayo ni Muhimbili, Mbeya na Hospitali ya KCMC Moshi. Kazi ya utayarishaji wa chanjo nchini Tanzania ilijumuisha kufanya kazi na makundi rika ya polisi Dar es Salaam na makundi rika ya jamii Mbeya pamoja na kujenga uwezo tangu mwaka 1994. Mpango wa HIV wa Jumuiya ya Ulaya ulisaidia utafiti wa Vaccine Immunogenicity (Awamu I/II) nchini Tanzania tangu mwaka 2004. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya TACAIDS: www.tacaids.go.tz
 
I assume this is another fake news since source imetoka radio China
 
Ile chanjo waliyochanjwa polisi iliishia wapi.


UTAFITI WA MUHAS WAONYESHA CHANJO DHIDI YA VVU NI SALAMA TUTAUPINGA NAO ?​

Akiwasilisha matokeo hayo, Profesa wa Mikrobiolojia na Immunolojia MUHAS, Eligius Lyamuya, amesema chanjo hiyo iliyofanyiwa majaribio imetengenezwa nchini Sweden na wataalam wenzao ambao wanashirikiana nao katika masuala ya tafiti; "Tumeifanyia utafiti chanjo hii tuliangalia iwapo ni salama na iwapo ina uwezo wa kuchangamsha ile kinga ya mwili kutengeneza viashiria vya kinga na iwapo ina uwezo wa kutengeneza chembe chembe hai za mwili. "Au uwezo wa kutengeneza molecular mbalimbali ambazo zinaashiria hii inaweza kuwa zinahusika katika kinga dhidi ya chanjo ambayo imetolewa." Hivyo, tumebaini chanjo hii ni salama na wote waliochanjwa hakuna ambaye amepata madhara yoyote hadi sasa wako vizuri," alisema.

Chanjo dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) inayofanyiwa majaribio nchini Tanzania ni salama na ina uwezo wa kuufanya mwili kutengeneza viashiria vya kinga.Hata hivyo hiyo haimaanishi chanjo hiyo ni kinga dhidi ya Maambukizi ya Virusi (VVU) hivyo, matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), yamebainisha. UTAFITI WA MUHAS WAONYESHA CHANJO DHIDI YA VVU NI SALAMA


I assume this is another fake news since source imetoka radio China
Tunashindwa nini kutembelea vituo vya utafiti huu unaofanyika Tanzania ?
Utafiti huu unakufanyika kwenye vituo vitano katika nchi 4: Masaka, Uganda; Mbeya, Tanzania; Dar-es-Salaam, Tanzania; Maputo, Msumbiji na Durban, Afrika Kusini. Nimeweka pdf ili kupata maelezo ya kwenye chapisho la kwanza katika bandiko hili na rejeja kwa kubofya link Tanzania na Uganda zatajwa kushiriki majaribio ya chanjo ya HIV
 
Hapo lengo si kupata hiyo chanjo, lengo ni kumegewa fungu nono toka WHO ili waweze kuzitafuna, ni hilo tu; otherwise chanjo ikipatikana biashara si ndio inakuwa imefika mwisho? Sasa nani atakubali biashara yake ife
 
Mbona corona wameipata?
 

Ni nani anapewa chanjo ... mtu asiye na virus au mwenye virus
Je lengo ni kujua kama virus vinakufa kwa hiyo dawa au virus havimpati aliyekunywa hiyo dawa
Je kama mtu akinywa dawa akaenda kupima nguvu ya virus na dawa isifanye kazi, atafidiwaje?
 
Ni nani anapewa chanjo ... mtu asiye na virus au mwenye virus
Je lengo ni kujua kama virus vinakufa kwa hiyo dawa au virus havimpati aliyekunywa hiyo dawa
Je kama mtu akinywa dawa akaenda kupima nguvu ya virus na dawa isifanye kazi, atafidiwaje?
Umesoma pdf hapo juu marxlups ? Maelezo yanajitosheleza !
 
Kabla ya kupinga utafiti huu wa PrEPVacc ni vema tujikumbushe historia za chanjo kama Polio, Ndui, Dondakoo, Pepopunda, Surua, Kifaduro, HPV kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kubofya link chini
World Health Organization (WHO)​


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…