PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesaini hati tatu za makubaliano ya ushirikiano wa kielimu na Urusi zitakazowezesha kubadilishana wataalamu, kuimarisha tafiti za pamoja na kuongeza fursa za elimu ya juu kwa wanafunzi wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema mafanikio hayo yametokana na ziara ya kihistoria ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, iliyofungua fursa mpya katika sekta za elimu, sayansi na teknolojia.
Prof. Mkenda amesema makubaliano ya kwanza ni kati ya Wizara ya Elimu ya Tanzania na Wizara ya Elimu ya Urusi, yakilenga kubadilishana walimu na wataalamu, kuendesha semina za pamoja pamoja na kufundisha lugha za Kiswahili na Kirusi katika nchi hizo mbili.
Amesema makubaliano ya pili yanahusisha Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha RUDN, ambapo wanafunzi wa Tanzania watapata fursa ya kusoma Shahada ya Kwanza ya Teknolojia ya Anga kupitia mfumo wa shahada pacha, wakisoma miaka miwili Tanzania na miaka miwili Urusi.
“Programu hii itatumia mtaala wa viwango vya kimataifa. Wanafunzi wataanza masomo kwa lugha ya Kiingereza nchini Tanzania na kujifunza lugha ya Kirusi kabla ya kuendelea na masomo yao nchini Urusi,” amesema Prof. Mkenda.
Makubaliano ya tatu kati ya DIT na Chuo Kikuu cha RUDN yanahusu programu za Shahada ya Uzamili, ambapo wanafunzi watasoma katika nchi zote mbili na kutunukiwa shahada zinazotambulika kimataifa, huku ushirikiano huo ukifungua fursa zaidi za utafiti na ubunifu.
Aidha, Prof. Mkenda amesema Chuo Kikuu cha RUDN kimeahidi kutoa ufadhili wa masomo 10 kwa wanafunzi wa Kitanzania kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended DS/AI+.
Mafanikio hayo yanafuatia ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi mapema mwezi huu, iliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kielimu kati ya Tanzania na Urusi. Katika ziara hiyo, Rais Samia pia alitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha RUDN kwa kutambua mchango wake katika uongozi na maendeleo ya kimataifa.