SoC02 Tanzania na uwekezaji kutoka Nje

SoC02 Tanzania na uwekezaji kutoka Nje

Stories of Change - 2022 Competition

Chode kanju

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
17
Reaction score
19
Tanzania Na Uwekezaji Kutoka Nje

Katika kipindi cha zaidi ya mwaka cha Serikali ya awamu ya sita, Raisi Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya ziara katika baadhi ya mataifa mbalimbali barani Afrika, Ulaya, Mashariki ya kati, na Marekani. Miongoni mwa nchi alizozizuru ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji, Oman, Misri, Kenya, na Uganda. Ziara hizo kwa kiasi kikubwa zinalenga katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine, kuomba misaada ya kifedha (financial support) kutoka benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa (IMF), msaada ambao unasaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya,na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa miwili ya kimkakati ya reli ya umeme (Standard Gauge Railway) na ule wa bwawa la mwalimu nyerere la kufua umeme (Mwalimu nyerereStiegler’s Gorge Hydroelectric power station), lakini pia ziara hizi zimelenga katika kuitangaza Tanzania kiutalii na kiuwekezaji katika maeneo tofautitofauti kama madini,,kilimo na viwanda.

Nchi nyingi duniani hasa zile zinazoendelea, zenye dhamiraya kufanya mageuzi makubwa kiuchumi, zinautazamauwekezaji kutoka mataifa mengine (Foreign Direct investment) hasa kutoka mataifa yaliyo piga hatua kiuchumi, kama silaha muhimu na chanzo kikuu cha ukuaji wa uchumi, kwa kuchochea uzalishaji wa wingi na ubora wa bidhaa na huduma, kuchangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ajira, kusaidia katika ukuaji wa tekinolojia, lakini pia kuchochoea ushiriki wa kikamilifu katika biashara ya kimataifa hasa kwa kuyauzia kwa wingi bidhaa na huduma mataifa mengine.

Jitihada ambazo serikali ya awamu ya sita inazifanya katika kuwavutia wawekezaji kutoka nje (Foreign Investors) kuja kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo mengi ambayo bado kwa kiasi kikubwa yanahitaji uwekezaji wa nguvu na wenye tija (massive investment) utakaochajiza mageuzi makubwa ya kiuchumini, ni jitihada za kupongezwa sana kwani, ni kupitia uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo, viwanda, madini, nishati, utalii, pamoja na miundombinu ya maji, afya, elimu na usafiri, ndio kutaiwezesha Tanzania kufanya mageuzi makubwa kiuchumi yatakayo akisi upatikanaji wa huduma zote muhimu kwa ubora na kwa gharama nafuu, na kutatua changamoto za ajira itakayo pelekea kukua kwa kipato cha mtu mmoja mmoja kitakacho boresha hali ya maisha (Living standard) kwa wananchi wa hali zote.

Tanzania pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu inayokadiriwa kuwa milioni 60, kuwa mwanachama wa jumuiya mbali mbali za kimataifa kama (EAC na SADC), kuwa lango (Gate way) kwa nchi zisizo kuwa na bahari (Landlocked) kama Uganda, Zambia, DRC, Rwanda, Burundi, na Malawi, pamoja na kuwa na utulivu wa kisiasa, ambayo yote kwa ujumla wake ni miongoni mwa mambo ya msingi sana yanayozingatiwa katika uwekezaji haswa wa viwandani, kwani ndiyo yanayo chochea shughuli za uzalishaji lakini pia kutoa wigo mpana wa soko la bidhaa na huduma ndani pamoja na nje ya nchi. Uwekezaji unazingatia zaidi ya mambo hayo, Tanzania pamoja na kuwa na tunu hizo lakini pia na rasilimali nyengine (natural resources) kama wingi wa madini ya thamani na ardhi yenye rutuba, bado haitoshi kuwashawishi wawekezaji hasa wa nje kuja kuwekeza nchini kama mambo ya ; sera za kifedha (monetary policies) ambazo zinaangazia masuala ya mfumuko wa bei (inflation) na viwango vya kubadilishia fedha (exchange rates), sera za biashara ya kimataifa (international trade policies), sera za kiuwekezaji, masuala ya nishati, miundombinu hasa ya usafirishaji, rasilimali watu (human resources) ambayo ina ujuzi, ubobevu, pamoja na uzoefu, urasimu mwingi (bureaucracy), pamoja na masuala ya rushwa na ubadhilifu yakiwa bado ni changamoto.

Ni dhahiri kwamba Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kufanya Mageuzi ya kiuchumi hasa kupitia uchumi wa viwanda, kwani ina kila aina ya rasilimali muhimu zitakazo pelekea mageuzi hayo. Kukamilika kwa mradi wa bwawa la mwalimu nyerere ambalo linatarajiwa kuzalisha 5,920 GWh kwa mwaka, itatatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya nishati ya umeme, jambo litakalo iwezesha Tanzania kuwa na kila aina ya Viwanda kwani nishati ya kuendesha mitambo ya aina mbalimabli itakuwepo ya kutosha.

Serikalai ya jamhuri ya muunggano wa Tanzania pamoja na kuweka nguvu ya kutosha katika kuhakikisha utekelezaji na ukamilifu wa miradi mbalimbali ya kimkakati hasa ule wa reli na wa bwawa la mwalimu nyerere, iweke nguvu ya kutosha katika maboresho ya sera na mipango yake itakayo shawishi uwekezaji hasa ule wa kutoka nje kwa kuwawekea mazingira rafiki hasa katika sekta ya kilimo na viwanda kwani ni sekta ambazo zinategemeana sana, kuendelea kwa sekta ya kilimo ndio kuendelea kwa sekta ya viwanda ambayo inalenga katika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali lakini pia kwa kuzalisha bidhaa nyengine muhimu zisizotokana na sekta ya kilimo .

Takwimu zinaonesha kuwa pamoja na kuwa sekta inayo chukuliwa kama uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, lakini ni chini ya 24% pekee ya ardhi yenye rutuba (arable land) ndio inatumika katika shughuli zote za kilimo nchini Tanzania. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani uwekezaji wa kutosha unahitajika katika sekta hii, kwani Tanzania ina takribani nusu (49.7%) ya eneo lake lote ambalo ni ardhi yenye rutuba inayo ruhusu kilimo cha mazao mbalimbali. Sekta ya kilimo ambayo imeajiri watanzania zaidi ya 70% ni eneo la kimkakati sana, hivyo serikali ina kila sababu ya kuchukua hatua za makusudi hasa za maboresho ya kisera zitakazo wavutia wawekezaji wengi kutoka nje kuja kuwekeza katika sekta hii kwa kiwango kikubwa (large scale agriculture) kwa kutumia njia za kisasa za kilimo cha aina zote za mazao ya biashara, nafaka, mbogamboga na matunda yatakayochochea ukuaji wa uchumi kwa kutoa ajira za kutosha kwa watanzania, kuihakikishia Tanzania kushiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa ya uuzaji wa aina zote za mazao zenye ubora, lakini pia kwa kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda ambayo ndio ndoto ya muda mrefu kwa kuhakikisha upatikanaji wa malighafi zote muhimu kwa gharama nafuu.

Sekta ya viwanda nayo pia haifanyi vizuri nchini Tanzania, licha ya kuwa eneo linaloaminika kuwa kitovu cha ukuaji wa uchumi wa nchi yeyote. Kuzorota kwa ukuaji wa sekta hii nchini inasababishwa na sababu nyingi hasa za nishati, miundombinu ya usafirishaji, kutokufanya vizuri kwa sekta nyengine hasa ya kilimo. Kuelekea mageuzi ya kiuchumi Serikali haina namna nyengine zaidi kuweka sera na mikakati itakayo chajiza maendeleo ya sekta ya Viwanda.

Tanzania bado haijachelewa kuwa kama Japani, Ujerumani na Uchina ya barani Afrika kwa kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kupitia uchumi wa viwanda. Kwanza ihakikishe miradi yote hasa ile ya kimkakati ambayo haipo katika hatua mbaya ya utekelezaji wake, inakamilika ndani ya muda uliokusudia, lakini pia kufanya maboresho hasa ya kitaasisi (Institutional stability reforms) ambayo yatahakikisha Tanzania haiyumbishwi katika Dira na dhamirayake yakimaendeleo. Ubora wa taasisi ndio utahakikisha muendelezo wa kisera na Dira (policy consistency) hata kama Serikali itakuwa chini ya maraisi tofauti. KuitangazaTanzania pekee haitoshi, maboresho katika maeneo mengine nyeti pia ni vitu vya kuzingatia, muwekezaji hawezi wekeza sehemu ambayo inakila aina ya changamoto itakayo kwamisha mafanikio ya uwekezaji wake.

Mbwana Kanju Salim (Quantitative Economist)
Kanjuchode@gmail.com

0655510642
 
Upvote 2
Habari yako Chode Kanju

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Shukran sana kiongozi
 
"Serikali iweke nguvu ya kutosha katika maboresho ya sera na mipango yake itakayo shawishi uwekezaji hasa ule wa kutoka nje kwa kuwawekea mazingira rafiki.....

serikali ina kila sababu ya kuchukua hatua za makusudi hasa za maboresho ya kisera zitakazo wavutia wawekezaji wengi kutoka nje kuja kuwekeza....."


WAUMINI wa Kikwete economics wamerudi:

likiizo za kodi kwa wafanyabiashara wa kigeni, gawio la mirahaba, ajira kuchukuliwa na wageni, kupokwa mashamba, kutandikwa viboko na wachina, vitalu vya uwindaji kwa Waarabu, sumu za madini kwenye mito, mikataba ya capacity charge ya umeme, bandari kavu za makatibu wa CCM, bandari mbichi za Wachina, uwizi na ujambazi wa mikataba.
 
Ungeweka na kaumbea au useme tetesi,wabongobwanapenda umbea.
 
Back
Top Bottom